moyafricatz
JF-Expert Member
- Nov 27, 2015
- 2,900
- 4,865
Mtoa mada ni msabato.
Source ya hii habari wapi kamanda?Hapo awali kupitia ushahidi wa maandiko matakatifu tuliona kuwa Ibilisi hakuwa na makao ya kudumu katika sehemu ambapo yapo makao rasmi ya Mungu Mkuu huko mbinguni. Bali tuliona kuwa yeye na malaika waliokuwa chini yake waliishi katika mbingu nyingine. Na walikwenda katika makao ya Mungu kwa sababu maalum, yaani kwa ajili ya kazi yao rasmi ya kuendesha nyimbo za sifa za utukufu kwa wakati wa ibada kuu ya Mungu Muumbaji.
Tuliona pia kuwa Ibilisi aliishi katika mbingu nyingine na ya chini kihadhi ukilinganisha na ile ya Muumbaji. Kwa hiyo basi upande wangu nilijenga dhana ya kuwa huenda sehemu hiyo mbingu alipoishi Ibilisi na malaika waliokuwa chini yake ilikuwa ni katika sayari ya Mars.
Aidha, tulikuja kuona ukweli ya kwamba Mungu kwa asili ya ukuu wa mamlaka yake, asingaliweza kukubali makazi yake rasmi yawe sehemu ambapo ungefanyika uasi wa kiumbe ambacho alikiumba Yeye mwenyewe na kwa utashi wake.
Ushahidi wa maandiko unatupa ushahidi ya kuwa jaribio lolote lile la kutaka kuendesha vita na Mungu huwa linamalizika kabla hata vita yenyewe kuanza.
Ukweli juu ya jambo hili tunaweza kulipata kupitia unabii kuhusu hatma ya vita vya Armageddon kama vile ifuatavyo;
UFUNUO 19
19 Kisha, nikaona yule mnyama pamoja na mfalme wa dunia na askari wao wamekusanyika pamoja kusudi wapigane na yule aliyekuwa ameketi juu ya farasi pamoja na jeshi lake. 20 Lakini huyo mnyama akachukuliwa mateka pamoja na nabii wa uongo aliyekuwa akifanya miujiza mbele yake. Huyo mnyama pamoja na huyo nabii walitupwa wote wawili, wakiwa wazimawazima, ndani ya ziwa linalowaka moto wa madini ya kiberiti. 21 Majeshi yao yaliuawa kwa upanga uliotoka kinywani mwa yule anayepanda farasi. Ndege wote wakajishibisha kwa nyama zao.
Namba 3 kupitia tafsiri za kimaandiko huwakilisha jambo ambalo lipo chini ya mamlaka ya kimbingu ambalo hudumu katika muda mfupi na hatimaye kwenda kufikia ukamilifu wake wote kama vile ambavyo lilikusudiwa. Ndivyo ambavyo ilipangwa kwa uasi wa asili wa Ibilisi.
Kwanza alijaribu kuendesha vita dhidi ya Mungu wake katika ulimwengu wa kiroho, ambapo malaika watakatifu walipambana naye na kumshinda.
Pili ataendesha vita kupitia wanadamu wakiwa katika ulimwengu wa kimwili kama vile ambavyo tumeona katika rejea ya Ufunuo 19 napo atashindwa kwa mara nyingine.
Na ili akapate kudhihirisha uovu wake atapata nafasi ya tatu, mara baada ya kutoka kifungoni kwa miaka 1,000 ataendesha vita vingine ya kimwili akiwaongoza tena wanadamu. Ataongoza vita nyingine dhidi ya Mungu akiwa na jeshi la wanadamu wote waovu waliowahi kuishi duniani ambao wote watafufuliwa na kupewa muda mfupi mno wa kuishi tena na ili wote wathibitishe uovu wao kuwa wanamtii Ibilisi. Nukuu ifuatayo inaweza kutupa tafakari zaidi;
UFUNUO 20
7 Wakati miaka 1,000 itakapotimia, Shetani atafunguliwa kutoka gerezani mwake.
8 Basi, atatoka nje, ataanza kuyapotosha mataifa yote yaliyotawanyika kila mahali duniani, yaani Gogu na Magogu. Shetani atawakusanya pamoja kwa ajili ya vita; nao watakuwa wengi kama mchanga wa pwani.
9 Walipita katika nchi yote, wakaizunguka kambi ya watakatifu na mji wa Mungu aupendao. Lakini moto ulishuka kutoka mbinguni, ukawaangamiza.
10 Naye Ibilisi aliyekuwa anawapotosha, akatupwa ndani ya ziwa linalowaka madini ya kiberiti, walimo yule mnyama na yule nabii wa uongo, nao watateswa mchana na usiku, milele na milele.
Sasa baada ya kuona maandiko matakatifu yanatupa fununu zipi juu ya sehemu ya mbingu ambapo Ibilisi aliishi hapo awali. Sasa hebu tugeukie maandiko yake yeye mwenyewe na tuone yanatuambia nini juu ya jambo hili. Nafikiri wengi wetu wamekwipata taarifa ya sanamu ya mnyama iliyowekwa katika ofisi za makao makuu ya UN. Ni sanamu mfano wa chui mwenye mabawa, mwenye kinywa mfano wa simba na miguu mfano wa dubu.
Kiunabii mnyama kuwa na mfano wa simba huwakilisha dola ya kale ya Babeli ya kale na mfumo wa ibada zake za sanamu za kipagani, dubu huwakilisha dola ya kale ya Umedi & Uajemi na ibada zake za kipagani za kimajini na chui huwakilisha dola ya Kiyunani na ibada zake za kipagani za kimizimu.
Tunaweza hapa kujifunza kupitia mafunuo ya imani hizi za kipagani ili kujenga msingi wa kimaandiko, kifalsafa na imani za kidini. Jambo hili linathibitika katika kipindi cha dola ya kale ya Rumi na na ushawishi wake katika elimu ya sasa iliyopo duniani. Na ni hapa ndipo tunapata ukweli mwingine kuwa huenda ni kweli Ibilisi aliishi katika sayari ya Mars kabla ya kufukuzwa huko.
Elimu ya sasa hutuambiaa sayari ya Mars ama Mirihi kwa lugha yetu nzuri ya Kiswahili ipo umbali wa kilomita zipatazo milioni 54.6 kutoka ilipo sayari yetu nzuri ya dunia ama maili milioni 34.
Kihistoria na kisayansi sayari ya Mars ina muonekano wa rangi nyekundu, na kutokana na imani za kale za kipagani rangi hii ilihusishwa na matambiko ya damu na hivyo kuonekana inamwakilisha mungu wa mabaya kwa wa Wababeli wa kale, lakini Wamedi & Waajemi pamoja na Wagiriki waliona Mirihi kama mwakilishi wa mungu wa vita yaani "Ares" na jina hili likaja kupokewa na Warumi wa kale, huku nao wakiitafsiri sayari hii kuwa ni mungu wao wa vita mwenye hamu, uchu ama kiu kubwa ya kumwagika kwa damu.
Jina la mwezi wa tatu, yaani Machi limetokana na heshima ya Warumi kwa mungu Mars. Imani zote za dini za kale zilimpa sifa ya kipekee Mirihi kama mungu mwenye ujanja, hila na kiu ya damu ambaye hupenda machafuko na hatimaye kuleta matokeo ya vita.
Tunapata elimu nyingine ya kipagani kuwa Ares alishiriki katika Vita vya Trojan iliyotokea huko mbinguni ambapo alipambana na Athena na kushindwa katika vita hii. Tunaona ya kuwa Athena alikuwa na sifa tofauti kabisa na Ares kwa kuwa alitambulika kama mungu mwaminifu, mwadilifu na mwenye busara ambaye akilazimika kupigana, yeye hupigana vita vya haki na vya kimkakati.
Kwa hiyo maandiko matakatifu na mafundisho vyote hukubaliana ya kuwa vita katika ulimwengu wa kiroho vilitokea mbili. Naye Mungu mtenda haki alimshinda mungu muovu. Lakini mafundisho ya kipagani humtaja kwa uwazi mungu huyo muovu kwa alama ya sayari ya Mars ama Mirihi.
Mkuu Dumas, mbona vyanzo vya habari ni vingi tu!? Mada ya yangu itapata mashiko tu kama itakuwa "critized" kupitia watu wadadisi na wenye ufahamu mzuri. Mimi sina uelewa wa kina wa kiimani nje ya Ukristo.Source ya hii habari wapi kamanda?