Washa Carina kufukuzana na Vogie kama utaweza,au jaribu kuupita umri wa baba yako kama utaweza,ila unaweza kuufikia umri alionao taratibu na yeye akawa tayari keshatangulia mbele za haki,nchi za ulaya ndugu zilishatangulia kitambo na zimekua huru mamia ya miaka,utalingana nao wewe?lazima ikuchukue muda kufikia hapo,hata watu wao jinsi walivyo na akili na ubunifu wa mambo ni tofauti na jamii ya Africa hata wewe ni shahidi,mi nafanya kazi shilika la kusaidia maendeleo ya jamii yetu najua tukoje katika jamii,huwezi nidanganya kitu,bila juhudi zako binafsi maisha ya raha utayaona kwa wenye bidii tu na kuishia kulalamika bila sababu ya msingi,najua unaheshimu ufikiliacho lakini ukweli ndo huo,buni vitu,fanya kwa bidii na maalifa uone kama hutatoka na wewe ukiugua uende ukatibiwe ulaya!
Ila wote tutafika safari tuendayo na hatutaachana mbali, nchi za Asia unazizungumziaje?Afrika kusini?haya sema kuhusu ndugu zetu wakenya ambao kiumri ni wadogo zetu?lazima ifike mahali tupiganie maslahi bora kwa wananchi,inawezekana,pamoja na kufanya kazi,lakini mazingira mazuri ni lazima ili kazi tunazofanya ziwe na tija.Tafiti kuhusu maendeleo ya China,Korea kusini,na India,halafu jiulize sisi waafrika tuna nini?je!haiwezekani kabisa kuacha Ubinafsi na Ufisadi kwa maslahi ya wananchi?hata hao kina mama pia wanafanya kazi,ila,katika level gani?masoko ya bidhaa zao yakoje?mazingira ya kazi yakoje?wewe una elimu na unafanya kazi,sasa sio wote wenye elimu na kazi km yako,exposure hana,utafutaji wake mgumu,akienda hospitali ndo kama hivyo,je!bado itamwambia asilalamike kweli?najua kuna mambo makubwa bado hatujayafikia,ila haya madogo ni ya muhimu sana ili wapiga kura wako angalau wapate nafuu kwa kukuchagua wewe.