Maisha baada ya Kustaafu

ibby

JF-Expert Member
Mar 20, 2017
415
584
Habar Zenu waheshimiwa:

Nianze na Wanaume wenzangu, tufanye kazi kwa bidii tutafute hela ili uzee wetu tuwe na uwezo wa kujitegemea. Hakikisha kwenye uzee wako una pesa zako mwenyewe za kukufanya usurvive. Sahau kuhusu watoto, na mama yao kwamba watakutunza. Wewe ndiye stranger pekee kwenye hiyo familia unayoiita ya kwako. Hiyo nyumba ni ya huyo mwanamke na watoto wake. Not yours.!*

*Babu yangu aliniambia kwamba mwanaume aliyeoa ni sawa Tingatinga, ambalo linatengeneza Barabara, lakini ikishakamilika linabebwa juu juu kwenye Lori na kuondolewa, eti likitembea litaharibu barabara. Yani barabara ambayo Tingatinga lenyewe limeitengeneza haliruhusiwi kutembea juu yake.*

*Vivyo hivyo kwa mwanaume aliyeoa. Atajinyima, atajishughulisha, atajizuia kufanya anasa, atakopa, atavaa mitumba ili tu watoto wake waishi vizuri, wale vizuri na kusoma shule nzuri. Siku hizi urithi pekee uliobaki ni elimu bora coz mashamba ziliishaga. Lakini pamoja na yote hayo, bado ukizeeka hao watoto sio wako, ni wa mama yao. Wewe watakuita "Kamzee".*

*Watoto wakiwa na umri wa miaka 10 ndipo mama yao anaanza kuwajaza taarifa zisizovutia kuhusu wewe. Kadri wanavyokuwa ndivyo wanavyoelezwa mambo mengi. Wakifika utu uzima atawaambia "isingekua mimi hamgesoma, yeye alikua ni pombe tu na wanawake" Ukisikia hivyo ujue tingatinga limemaliza kazi yake sasa linakaribia kuondolewa barabarani.*

*Watoto wanapoanza kazi, mzee anakua amestaafu. Wanapokuja kutembelea wazazi, wakiondoka wanampa baba elfu 5 mbele ya mama. Halafu wanaenda jikoni na mama, wanampa hela kwa siri bila mzee kujua. Wakiondoka mama anamfuata mzee na kumwambia sukari imeisha. So ni suala la mzee kuamua kutoa ile elfu 5 aliyoachiwa na watoto ikanunue sukari, otherwise anywe chai isiyo na sukari. Hii ni moja ya sababu inayowafanya wazee kufa mapema baada ya kustaafu na kuacha wake zao Wajane.*

*Nimeshuhudia wazazi wenye watoto ng'ambo wakimchukua mama yao akaenjoy life majuu, na kumuacha baba yao nyumbani akilisha Ng'ombe wao wawili, na kutafuta chakula cha kuku.!*

*Wanaume work hard and save something for yourself at old age. Tafuta pesa kwa bidii, wape watoto elimu bora, wape mahitaji yao muhimu, jenga nyumba nzuri waishi vizuri, lakini ukizeeka dont expect too much from them. Enjoy maisha ya uzee kwa pesa zako mwenyewe ulizochuma ujanani.*

Asantenii
 
Upo sawa kabisa. Usitegemee msaada toka kwa vijana wa enzi hizi. Wao pia wanakuwa na familia zao na maisha ni magumu.
 
50yrs to come sijui watoto zetu watakuwa na muda wa kukaa na sisi kama siku hizi tu INSTAGRAM NA FACEBOOK zinapewa airtime kuliko mzazi.
 
Habar Zenu waheshimiwa:

Nianze na Wanaume wenzangu, tufanye kazi kwa bidii tutafute hela ili uzee wetu tuwe na uwezo wa kujitegemea. Hakikisha kwenye uzee wako una pesa zako mwenyewe za kukufanya usurvive. Sahau kuhusu watoto, na mama yao kwamba watakutunza. Wewe ndiye stranger pekee kwenye hiyo familia unayoiita ya kwako. Hiyo nyumba ni ya huyo mwanamke na watoto wake. Not yours.!*

*Babu yangu aliniambia kwamba mwanaume aliyeoa ni sawa Tingatinga, ambalo linatengeneza Barabara, lakini ikishakamilika linabebwa juu juu kwenye Lori na kuondolewa, eti likitembea litaharibu barabara. Yani barabara ambayo Tingatinga lenyewe limeitengeneza haliruhusiwi kutembea juu yake.*

*Vivyo hivyo kwa mwanaume aliyeoa. Atajinyima, atajishughulisha, atajizuia kufanya anasa, atakopa, atavaa mitumba ili tu watoto wake waishi vizuri, wale vizuri na kusoma shule nzuri. Siku hizi urithi pekee uliobaki ni elimu bora coz mashamba ziliishaga. Lakini pamoja na yote hayo, bado ukizeeka hao watoto sio wako, ni wa mama yao. Wewe watakuita "Kamzee".*

*Watoto wakiwa na umri wa miaka 10 ndipo mama yao anaanza kuwajaza taarifa zisizovutia kuhusu wewe. Kadri wanavyokuwa ndivyo wanavyoelezwa mambo mengi. Wakifika utu uzima atawaambia "isingekua mimi hamgesoma, yeye alikua ni pombe tu na wanawake" Ukisikia hivyo ujue tingatinga limemaliza kazi yake sasa linakaribia kuondolewa barabarani.*

*Watoto wanapoanza kazi, mzee anakua amestaafu. Wanapokuja kutembelea wazazi, wakiondoka wanampa baba elfu 5 mbele ya mama. Halafu wanaenda jikoni na mama, wanampa hela kwa siri bila mzee kujua. Wakiondoka mama anamfuata mzee na kumwambia sukari imeisha. So ni suala la mzee kuamua kutoa ile elfu 5 aliyoachiwa na watoto ikanunue sukari, otherwise anywe chai isiyo na sukari. Hii ni moja ya sababu inayowafanya wazee kufa mapema baada ya kustaafu na kuacha wake zao Wajane.*

*Nimeshuhudia wazazi wenye watoto ng'ambo wakimchukua mama yao akaenjoy life majuu, na kumuacha baba yao nyumbani akilisha Ng'ombe wao wawili, na kutafuta chakula cha kuku.!*

*Wanaume work hard and save something for yourself at old age. Tafuta pesa kwa bidii, wape watoto elimu bora, wape mahitaji yao muhimu, jenga nyumba nzuri waishi vizuri, lakini ukizeeka dont expect too much from them. Enjoy maisha ya uzee kwa pesa zako mwenyewe ulizochuma ujanani.*

Asantenii
Nimefurahishwa sana na thread yako hii. Unajitambua na unaelewa ukweli wa maisha ya kinafiki ya ndoa zetu.
Mwanaume kufanywa sperm donor kwenye mji wake!
Watoto wakoseapo, tusi la ghadhabu hutukanishiwa baba yao mzazi, " utakuwa lijinga kama baba yako".
Vyote vilivyopo, nyumba na rasilimali zingine eti ni kwa ajili ya watoto!
Ni mengi ya hovyo mno tutendewayo wanaume kwenye ndoa ambayo mengine haujayaongelea.
Big up sana.
 
Ukweli mchungu huu asee. Ila unaweza kusababisha vijana waona kama ndio hivyo bora kula maisha tu akizeeka poa tu akifa poa tu.

Ila mzee dingi ukijipanga una kimango chako cha kueleweka baada ya kistaafu au uzeeni mbona kila mtu atakushobokea asee.

Tujipange mda huu tukiwa na nguvu jamani.
 
Umeongea ukweli, ila wadingi wengne wanazngua sana somtymz hawafikirii watoto watakua sikumoja na kukumbuka ya zamani
 
Nimesoma kwa makini sana,,Bila shaka mleta uzi ni Mchagga!

Hiyo ndio hali halisi ya wazee wengi (ME). Laikini hali kama hiyo inasababishwa na mtindomaisha wa wazee wenyewe enzi ya ujana/utuuzima wao.

Mfano; Baba anatoka asubuhi watoto wamelala anarudi usiku wamelala..hapo hata mama akiwaambia anawalea mwenyewe ni lazima watakubali.

Baba hana muda wa kukaa na watoto na kuongea nao na kuonyesha upendo wake kwa wanawe..hakuna jambo la muhimu na la maana kama kukaa na mtoto/watoto na wakakuzoea na kupata kauli za faraja kama vile; Pole, Hongera, Usijali, Ninakupenda n.k....Hapa ndiko akina mama wanakotupigia bao maana wao ndio wimbo wao kila siku. Wanaume wengi wetu muda wote ni wakali na tunaonekana tumekunja ndita usoni kiasi kwamba tukiingia tu watoto wanakimbia kama vile nyumbani ameingia mwendawazimu. Mama kwa kuona hilo ikitokea mtoto amekosa, badala ya yeye kumwadhibu anamwambia, 'Ngoja baba yako aje utakoma" Kwa hali hiyo anazidi kujenga uadui kati ya baba na watoto.

Mleta uzi kama ulivyosema, ni bora tukajiwekea akiba yetu wenyewe itusaidie kwa wakati huo, ila akiba nzuri iweke mioyoni mwa watoto wako nje na hapo hata hiyo akiba watatafuta namna ya kuichukua hata ikibidi kwa kuitoa roho yako.

Kuna mzee mmoja wa Kisonjo aliniambia, Watoto wakikua(watu wazima), oa mke mwingine maana mke wako naye atakuwa ameolewa na wanawe.
 
ndo uhalisia wa maisha tunayo eshi kwa sasa japo ni vigumu kujuwa wala kuona ukweli yakubidi uwe na jicho la tatu!!wangereza wanasema:Work hard like slave to live like a king "mimi ni MBurundi kaka ila tanzania nyumban na nawapenda watanzania pia!!

Back
Top Bottom