Maisha baada ya kumzika mwanangu

Mtoto wa kiume wewe jikaze ndio sifa kuu.
 
Pole sana ndugu. Maisha ndivyo yalivyo na kukata tamaa haikubaliki. Jipe Moyo, huu ni wakati unapohitaji kusali na kuomba zaidi msaada wa Mungu.

Hali yako inanikumbusha hali iliyomkuta baba yangu mzazi alipofiwa na mke wake (mama yangu mzazi). Alikata tamaa kabisa mpaka siku moja akatamka wazi kuwa ni bora afe tu kuliko kubaki peke yake. Alikuwa tayari hata kunywa sumu na tulifanya kazi ya ziada kumshawishi na kumsihi aachane na mawazo hayo na hatimaye alituelewa. Sasa amerudi hali ya kawaida.

Hata wewe hatimaye utakuwa sawa. Nakuombea Mungu akupe faraja unayohitaji sana kipindi hiki.
POLE SANA!
 
Kijana wangu amelazwa regency hospital kwa matibabu, yaani hapa nilipo nipo ovyo ovyo tu, katoto kenyewe ka moja yaani.
 
Pole sana man, maumivu ni part ya maisha tu.
Na hapo ndipo akili yako inabidi iwaze jinsi ya kuondokana na hiyo sonona, usitegemee saana kama kuna mtu atakuja kukuondolea hiyo kitu mkuu.

Jitahidi usahau hiyo kitu, bado kuna watu wanahitaji huduma yako kwa namna moja ama nyingine, usiwaze kuhusu kufa mkuu tafadhari saana.
 
Umezungumza jambo zito sana, Mungu atusaidie. Mtoto anaumiza sana maana faraja yake akiwa ndani ya nyumba huwa ni ya kipekee sana
 
Mkuuu polee sana mkuuu

AAA njia pekee mkuu inayoweza kukutoa katika hali hiyo mkuu.

Ni weka nguvu zako katka Ibada mkuu.
And usimame kwelikweli na Mungu.

Kataa hiyo hali ya kutaka kufa mkuu wangu asee Mwenyenzi Mungu anamakusudi na Maisha yako Mkuu wangu.

Na kuna kusudi la Mungu kukuacha wewe na akamchukua Binti yako.

Mwisho Sali sana ukiamini Mungu pekee anawaza kukupa Faraja na kukutoa katka hali hiyo mkuu wangu

Polee sana mkuuu wanguu
 
Mshukuru Mungu kwa uzima ambao hata wewe unao,hapa ninapo-type nina jamaa zangu wawili mmoja mke amefanyiwa upasuaji akafariki kamuachia kichanga mwengine mke ametoka japo hajaamka ila mtoto haja-survive.

Tunajua matatizo hayafanani pole sana acha maisha yaendelee huna namna
 
Usife moyo ndg,matatizo
hutupata sisi wanadamu,
Yesu alisema kupitia;
Yohana 16:33b
"Ulimwenguni mnayo dhiki,
lakini jipeni moyo,mimi
nimeushinda ulimwengu"
Piga moyo konde,
Mungu atakusaidia.
Ukipata nafasi sikiliza wimbo
huu;
Shida za Dunia by Josee
Chameleon.
 
Just come nitakusaidia

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Mungu akure nguvu uweze kupita kipindi hiki .muda utakuponya
 
Pole sana brother! Jikaze kiume, utapata watoto Mungu ni mwema.
 
Kijana wangu amelazwa regency hospital kwa matibabu, yaani hapa nilipo nipo ovyo ovyo tu, katoto kenyewe ka moja yaani.
Pole mkuu, endelea kuomba sana Mungu amsimamie! Apone haraka! Inaumiza sana! Kipindi kile mimi nililia mno. Mpaka nikawa nagoma hata kupokea simu za watu!
 

Nature haitokani na uzembe.
Alikufa kwa uzembe wa wahudumu wa afya na sio nature.

#YNWA
 
Usilie mpaka ukamkufuru Mungu.

Hata ukifa hautakutana na binti yako, , ona hili neno

Mathayo 22: 30 b ....... bali huwa kama malaika mbinguni.

Jaribu pia kutafuta nyumba uhamie sehemu nyingine.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…