Maisha baada ya kufa

Maisha baada ya kufa

Kuna pepo na kuna moto

Maisha ya Watu wa Peponi (Ahli Jannah)

Sifa Kuu za Peponi:

Neema zisizoisha: Kuna mito ya asali, maziwa, mvinyo usioharamisha, na maji safi (Qur’an 47:15).

Makazi bora: Nyumba za dhahabu na fedha, zenye mito inapita chini yake (Qur’an 18:31).

Chakula na matunda: Watapata matunda ya kila aina, na vyakula wanavyovitamani (Qur’an 36:57).

Mavazi: Nguo za hariri na mapambo ya dhahabu na lulu (Qur’an 22:23).

Furaha na amani ya milele: Hawatashuhudia huzuni, maumivu, wala ugonjwa (Qur’an 35:34-35).

Watakuwa pamoja na jamaa zao walioamini: (Qur’an 52:21).

Kilele cha neema: Ni kumwona Mwenyezi Mungu (Hadith – Sahih Muslim).



---

2. Maisha ya Watu wa Motoni (Ahli Jahannam)

Sifa Kuu za Moto wa Jahannam:

Adhabu kali: Moto mkali sana kuliko wa duniani (Qur’an 70:15-16).

Vyakula vibaya: Watakula mti wa Zaqqum, vyakula vya moto, na kunywa maji ya moto yanayochemka (Qur’an 37:62-67).

Nguo za moto: Nguo zao zitakatwa kutoka kwa moto na maji ya moto yatamwagwa vichwani mwao (Qur’an 22:19-20).

Maumivu ya kimwili na kisaikolojia: Ngozi zao zitachomwa mara kwa mara na kubadilishwa ili waendelee kuadhibiwa (Qur’an 4:56).

Majuto yasiyo na msaada: Watapiga kelele, wataomba msaada, lakini hawataokolewa (Qur’an 23:106-108).

Kutengwa na rehema ya Allah: Hawatapata furaha, msamaha wala matumaini.
Hao wengine eti watakuwa wanaomba kwaya ,kusifu na kuabudu na kustarehe japo hawajaelezq watastarehe vipi 😆😆
 
Usilete hadithi za kufirika wewe, ukifa umekufa tu kama wanyama wengine na unapotea humuhumu duniani, hakuna maisha tena! Acha kudanganya watu
 
Maisha baada ya kifo ni story za uongo.
Furahia maisha hapa duniani kadri uwezavyo kabla hujafa, ukishakufa kila kitu kwako kimekufa.

Kama usivyojua chochote cha kabla ya kuzaliwa kwako, pia hutajua chochote baada ya kufa kwako.
 
Usilete hadithi za kufirika wewe, ukifa umekufa tu kama wanyama wengine na unapotea humuhumu duniani, hakuna maisha tena! Acha kudanganya watu
Jitihada za ubongo wa binadamu kukataa mwisho wa maisha yake hupelekea kutengeneza nadharia nyingi za kila aina: mbinguni/peponi, jehanamu, kuzaliwa tena (reincarnation) na kadhalika. Akili haitaki kuamini ukweli inabuni hadithi za kujifariji!!
 
Back
Top Bottom