Once it was AK 47s and now it's Machine Guns!. These inconsistencies are not good at all.
Kwenye bandiko langu kuhoji the role of dereva wa Lissu kwenye tukio hili.
Dereva wa Lissu ndiye aliyewaona washambulizi, na ndiye aliyesema Bunduki zile ni AK.47, nikauliza mtu wa kawaida asiyejua mambo ya silaha anazijuaje AK. 47?, kwa sababu sisi Tanzania, hatuzitumii ?.
Kwenye haya yanayosemwa na Lissu kuhusu shumbulizi lile, kuna mengine ya kweli na mengine ya uongo. Kwa kuanzia idadi ya risasi, kama polisi wetu ni makini, wameokota maganda na wamehesabu matundu sskwenye gari. Taarifa ya ni risasi ngapi, za silaha za aina gani should have been easily clarified na polisi wetu.
Taarifa ya ni risasi ngapi zilimuingia Tundu Lissu, hii ni taarifa ya kidakitari, atakuwa alipigwa full body exray pale Dodoma hospital, walitibu matundu yote ya risasi, walizichomoa walizoweza lakini zilingia ngapi wanajua, kwanini hawasemi.
Uongo always unakuwa defeated na ukweli, kwa nini jeshi letu la polisi halijasema kitu, hivyo all the info kuhusu shumbulizi lile zinazo trend kwenye international circles ni from s single source Tundu Lissu na dereva wake, hivyo hata wakisema uongo au kuongezea chumvi, itaonekana huo ndio ukweli wenyewe, kwa nini jeshi letu la polisi, limeshikwa na ganzi na kigugumizi cha ajabu kuzungumzia tukio hili?.
Hoja ya kumsubiria Lissu na dereva wake wahojiwe, doesn't hold water, jee wote wangeuwawa kwenye tukio, uchunguzi usingefanyika kwa sababu hakuna shuhuda?.
Lissu ameshambuliwa vibaya kwa nia ya kumuua, kwa sasa ana ehueni ila bado anahitaji compassion, ila kwa vile mwenyewe anaongea sana, na vitu vingine haviko very straight, ikitokea tuu mtu objective kuhoji lolote alilosema Lissu huchelewi kunyooshewa vidole humu.
Huu ukimya huu...
P.