Ms Judith
JF-Expert Member
- Dec 24, 2010
- 2,563
- 936
mwandosya ni waziri wa maji, yeye na mkurugenzi wake wako ofisi moja wakitofautiana majukumu tu. huko same wameongozana halafu mkurugenzi anajifanya kumwambia waziri wake juu ya hazina ya maji. alishindwa kumwambia ofisini na waziri atembelee kujionea hadi waongozane wote na kufanya maigizo mbele ya wananchi? aou ni mipango ya per diem imeshika kasi?
habari kamili hii hapa chini:
Serikali yatangaza eneo la Sterling kuwa Hifadhi Send to a friend
Thursday, 27 January 2011 20:59
0
digg
Mkurugenzi msaidizi anayeshughulikia rasilimali ya maji katika Wizara ya Maji, Lister Kongola (kushoto) akimweleza Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya kuhusu umuhimu wa eneo la Sterling wilayani Same ambalo limegunduliwa kuwa na rasilimali kubwa ya maji ardhini juzi. (Picha na Daniel Mjema)
Daniel Mjema, Same
WAZIRI wa Maji, Profesa Mark Mwandosya, ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro kulitangaza eneo la Sterling lililogundulika kuwa na rasilimali nyingi ya maji chini ya ardhi kuwa eneo la Hifadhi.
Agizo hilo la Profesa Mwandosya alilitoa juzi katika mji wa Same baada ya kuelezwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali za Maji kutoka Wizara ya Maji, Lister Kongola kuwa eneo hilo limegundulika kuwa na hazina ya maji.
Kongola alisema eneo hilo lenye ukubwa wa kilometa za mraba kati ya 15 na 20 linapaswa kuhifadhiwa.
Mkurugenzi huyo msaidizi alisema utafiti wa kitaalamu umebainisha kuwa visima hivyo viwili vinavyochimbwa vina uwezo wa kutoa maji yenye ujazo wa mita kati ya 50-60 na eneo hilo ni mkombozi wa tatizo la maji Mji wa Same.
Baada ya kupokea maelezo hayo na baadaye kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uwanja wa Kwasakwasa, Profesa Mwandosya alisema kuwapo kwa eneo la Sterling ni Mungu ameipendelea Same.
Waziri Mwandosya aliiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Same kuhakikisha eneo hilo ambalo baadhi ya wananchi walipimiwa viwanja na kuanza ujenzi, halivamiwi na maeneo ambayo hayajajengwa hayajengwi tena.
Hivi ni lazima hawa watu wakajenge juu ya eneo lenye chanzo cha maji?, wapimieni wananchi maeneo mengine lile liwe eneo la hifadhi na kwa hili lenye maslahi ya wengi naomba watu wachache watusamehealisisitiza waziri.
Profesa Mwandosya aliitaka Halmashauri hiyo ya Same kuanzisha mchakato wa kisheria wa kulitangaza eneo hilo kuwa hifadhi kwa kutumia sheria ndogo za Halmashauri na wakikwamba wawasiliane na wizara kwa msaada zaidi.
Awali akitoa taarifa ya Halmashauri kwa waziri, Mhandisi wa wilaya hiyo, Fimbo Mtango alisema ingawa mahitaji ya maji katika mji wa Same ni meta za ujazo 4,500 kwa siku, kwa sasa upatikanaji wake ni meta za ujazo 750 tu.
Kutokana na kushuka huko kwa uzalishaji wa maji, mapato yanayokusanywa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Same(Sauwsa) yameshuka kutoka Sh12 milioni kwa mwezi hadi kufikia Sh9 milioni.
source: Serikali yatangaza eneo la Sterling kuwa Hifadhi