Maige: Majungu CCM yameniondoa uwaziri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maige: Majungu CCM yameniondoa uwaziri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OSOKONI, May 29, 2012.

 1. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #1
  May 29, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,798
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  BAADA ya kimya cha muda mrefu tangu ang'olewe katika nafasi ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige ameibuka na kueleza kuwa moja ya sababu ya kuondolewa kwake kwenye nafasi hiyo ni majungu ndani ya chama chake CCM na kuonya, hali hiyo ikiendelea chama hicho kitakufa.

  Hii ni kauli ya kwanza kwa Maige kuitoa hadharani akizungumzia kuondolewa kwake kwenye nafasi hiyo tangu Rais Jakaya Kikwete alipofanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri Mei 4, mwaka huu yaliyomng'oa Mbunge huyo wa Msalala.

  Jana, Maige akiwa mjini Kahama katika mkutano wake na viongozi wa CCM wa Wilaya hiyo na Mkoa wa Shinyanga, baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili katika jimbo lake, alionya kwamba kwa hali hiyo, CCM kinaelekea kubaya.

  Katika mkutano huo uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa CCM akiwamo Mwenyekiti wa Mkoa, Hamis Mgeja, Maige alisema baadhi ya wanaCCM wamekuwa vinara wa kushabikia majungu aliyoyaita ya ‘kipumbavu' badala ya kutembelea wananchi na kujua matatizo yao. Akaonya: "Majungu ya kipumbavu ya aina hiyo, yatasababisha chama kife."

  Alisema kitendo cha baadhi ya wanachama wa CCM kushabikia kuondolewa kwake kwenye uwaziri, kinaonyesha jinsi gani ambavyo wameonyesha kuwa na uelewa mdogo wa kisiasa akisema walidhani wanamkomoa... "Kumbe wanajikomoa wenyewe."

  Alihoji ni lini CCM kimefanya mkutano kwenye jimbo lake licha ya kuwa na nyenzo zote za usafiri ikiwemo magari na pikipiki lakini, Chadema wasiokuwa hata na baiskeli wameweza kupita jimbo zima wakifanya mikutano yao na kugawa bendera zao kama njugu.

  Alisema endapo majungu hayo yataendelea kitakufa na kuongeza kuwa wazee zaidi ya 300wa jimbo lake wamemfuata wakimtaka awaeleze anahama lini CCM ili wamfuate atakapokwenda.

  Hata hivyo, Maige alisema alitumia busara zaidi kuwatuliza na kuwapa pole kwa yaliyomfika ya kuzushiwa tuhuma kwenye wizara kwa lengo la kumchafua.

  Ailipua Kamati ya Maliasili
  Akizungumzia Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, Maige alisema taarifa yake rasmi haiendani na ile iliyosomwa bungeni hali ambayo alidai ilikuwa na lengo la kumng'oa kwenye uwaziri.

  Maige alishangaa kuona Mwenyekiti wa Kamati hiyo na Mbunge wa Kahama, James Lembeli akimzushia kile alichokiita taarifa hiyo ambayo si kweli akisema madai yaliyokuwemo yalifanyiwa uchunguzi wa kina lakini, kwa kuwa ilikuwa imepangwa kwa lengo la kumng'oa ilitekelezwa.

  Alimtaka Lembeli warejee kwenye meza ya mazungumzo yenye kuwaletea maendeleo wananchi wa Kahama: "Baada ya kutekeleza lengo lake la kumng'oa kwenye uwaziri," akisema kabla ya kupata wadhifa huo walikuwa marafiki na walitembea pamoja kwenye majimbo yote ya Kahama na Msalala kwenye mikutano yao.

  Lembeli: Maige apangue tuhuma

  Lembeli akizungumzia madai hayo ya Maige, alisema anachopaswa kufanya waziri huyo wa zamani ni kujibu tuhuma zilitolewa na kamati kuliko kuendeleza chuki binafsi zisizokuwa na msingi.

  Lembeli alisema kwamba haingii akilini kuona kwamba yeye mtu mmoja anaweza kutoa ripoti ya kamati ya watu 30 na kuweka mawazo yake binafsi.

  "Anachokifanya kunituhumu mimi ni chuki binafsi za kukosa uwaziri. Anachotakiwa ni kujibu hoja za kamati. Nilichokisoma pale ni ripoti ya kamati yote ya watu 30. Anachokifanya ni makosa," alisema Lembeli.

  Katika ripoti yake, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) alisema Wizara ya Maliasili na Utalii ilikuwa ikiongozwa na Maige, ilituhumiwa kuhusika na upotevu wa Sh800 milioni za mazao ya misitu huku Kamati ya Maliasili na Utalii ikimtuhumu waziri huyo kwa kujimilikisha vitalu.
   
 2. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #2
  May 29, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Simuelewi Maige kwa kweli, kama kweli ameona ameonewa anasuri nini kujiengua kutoka chama kichafu akaingia chama kisafi, huo uadilifu wake uko wapi sasa. Kama kweli yeye ni mwadilifu na siasa za majungu zimemshinda na anatabiri jimbo lake litaenda na CDM 2015, anasubiri nini kujivua gamba? au ni kuendekeza siasa za umaskini kuwa akiondoka sasa atakosa posho na marupurupu?

  Kulalamika bila kuchukua hatua nikuwahadaa wananchi wa jimbo lake na watanzania kwa ujumla.Maige chukua hatua tuone umekerwa na mfumo uliopo.
   
 3. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #3
  May 29, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Waziri wa Twiga na vitalu mstaafu anachemsha sasa
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  May 29, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  CCM yote majizi..huyu si ndo alisema alichukuwa mkopo benki akawa anafanya mishemishe za kuzungusha kila mwezi alikuwa anaingiza $20,000???? au nakosea...Maige bwana hesabu zako rahisi sana bana kwa mtu kukubali na kuelewa unongea nini
   
 5. kivyako

  kivyako JF-Expert Member

  #5
  May 29, 2012
  Joined: Feb 2, 2012
  Messages: 8,828
  Likes Received: 4,198
  Trophy Points: 280
  Baada ya chenge, ngereja, maige nae apokelewa kishujaa!!
   
 6. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #6
  May 29, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Mbona hazungumzii kabisa namna Twiga walivyopakia Ndege na kupelekwa uarabuni!?
   
 7. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #7
  May 29, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,827
  Trophy Points: 280
  Maige, acha usanii, utoto,kukosa ukomavu- mbona hukusema hayo toka mwanzo wakati una keki ya wanyama, miti, etc kwenye sahani? Kardinali Pengo alisema nyie mnao kemea ufisadi, yanawatoka rohoni au kwa vile hamjapata nafasi ya kufanya ufisadi. Sasa wewe umenyanganywa nafasi ya kuiba/kufanya ufisadi unaiona CCM mbaya!! Kabla ya hapo ilikuwa chama makini!!! Shenzi !!!!
   
 8. p

  peter tumaini JF-Expert Member

  #8
  May 29, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 575
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  sioni jipya kwake hana lolote la maana atakalokumbukwa pale wizarani zaidi ya kusafirisha twiga nje ya nchi.
  To hell comrade Maige huna uzalendo zaidi ya majungu.
   
 9. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #9
  May 29, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Huyu jamaa bado anauota uwaziri tu! May be he was born to be a minister, such that missing it is committing a sin.
   
 10. t

  thatha JF-Expert Member

  #10
  May 29, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Nashangazwa na kauli zinazoendelea kutolewa na Mh. Ezekiel Maige tangu alipotolewa katika nafasi ya uwaziri. Lililo dhahiri ni kuwa Maige kaumizwa sana na kung'olewa uwaziri pamoja na madudu yote aliyoyafanya akiwa waziri. Maige ametajirika sana katika kipindi kifupi tu cha uwaziri wake, la kujiuliza ubunifu wa ujasiriamali wa kutengeneza millions of shillings kaupata baada ya kuukwaa uwaziri. Mh Mwakyembe alipata kusema "watanzania si mabwege tena hivi sasa wameshaamka" Utajiri wa Maige una uhusiano moja kwa moja na nafasi yake ya uwaziri wa maliasili na utalii na si vinginevyo. Nawashangaa hata hao wapiga kura wake wanaolalamika, Maige aliomba kazi ya ubunge ambayo walimpatia uwaziri ni matokeo tu hivyo ukikuponyoka huna sababu ya kuchanganyikiwa.

  Maige leo ndiyo anagundua kuwa CCM kuna majungu na matatizo lukuki huu ni unafiki uliopitiliza, mkiwa madarakani mnaona mambo yako sawasawa mkitoka ndiyo ghafla mnageuka kuwa wanaintelijensia na kugundua kuwa kuna matatizo ndani ya ccm. Hata Philip Mangula pamoja na kupata malalamiko kutoka kwa wanaccm wasafi juu ya kukithiri kwa rushwa kwenye chaguzi ndani ya chama aliziba masikio, baada ya kupoteza ukatibu mkuu na kukumbana na rushwa wakati akigombea uenyekiti wa ccm mkoa wa Iringa akagundua kuwa kuna rushwa kwenye chaguzi za ccm. Ni vema viongozi wetu mjihangaishe kutatua kero zinazoikabili jamii mkiwa madarakani msisubiri mpoteze nafasi za uongozi ndipo mgundua kuwa kuna rushwa, it's reinventing the wheel.

  Aliyenishangaza zaidi ni hamisi mgeja mwenyekiti wa ccm mkoa wa shinyanga eti naye anasikitika maige kuondolewa uwaziri na kudai kuwa wanakahama wamepoteza mpambanaji. Hivi huyu mzee yuko sawasawa kweli? maige hajafa, anaendelea na ubunge wake sasa ni vipi wapiga kura wa msalala wamepoteza mpiganaji? Maige jipange upya acha kulialia.
   
 11. M

  MpendaCHADEMA Member

  #11
  May 29, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu jamaa inaonekana ni mlafi...anatakiwa kujua kupata na kukosa yote sawa! alipendelewa na jk akaona ni haki yake kuwa waziri. Atofautishe kati ya privillege na right...
  aache kulialia....kama vp avue gamba tutampa cheo cha "mwanchama wa chadema".
   
 12. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #12
  May 29, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,461
  Likes Received: 5,846
  Trophy Points: 280
  KWA HIYO ANAMAANISHA jk ANASIKILIZA MAJUNGU YA KIPUMBAVU? HATA AKAMUONDOA HUO UWAZIRI?
   
 13. Mziba

  Mziba JF-Expert Member

  #13
  May 29, 2012
  Joined: Feb 7, 2010
  Messages: 226
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Lini kesi yake itaanza sikilizwa?
   
 14. Vinci

  Vinci JF-Expert Member

  #14
  May 29, 2012
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 2,642
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Filipo ni kwamba huyu jamaa alikana kwamba huu uhalifu sio awamu yake, Yeye aliingia tayari hilo limeshatendeka. Ila huyu jamaa anatumia nguvu nyingi kujisafisha mwishoni atajikuta amejichafua. angetulia kimya
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. S

  Sgaga Member

  #15
  May 29, 2012
  Joined: Sep 28, 2011
  Messages: 76
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hili pumbavu kweli yaani hadi leo bado linauma tuu,badala ya kufikiria mbele,yaani kwa akili yake mbovu alijua pale ndyo kafika yaani poyoyo kweli na midomo yake iliyobinuka
   
Loading...