Maige amwita Nape 'Gamba', Nape amjibu...

Mkuu wangu Kimbunga kweli lazima uchanganyikiwe huyu ndege jina jingine anaitwa Ardeotis Kori nyama yake tamu ana kilo 18 upate jike wanachoma na kula na mkate wa kuchoma...kweli Maige tumuonee huruma...kila jumatatu anachinjiwa Nyemera jike.

Duh mkuu ritz nilikuwa nadhani nimekuacha kumbe na huko kwenye maliasili za nchi yetu upo!! Unaambiwa Bush anampenda sana huyu ndege. Niliwahi kujichanganya mahala nikamla huyo ndege! Anapatikana Ngorongoro Crater.
 
Last edited by a moderator:
Jamani, 'Tuwaache CCM wazikane wenyewe sisi tutakuja kutoa pole baada ya mazishi' na sisi tutamteua mtu wa kumrithi mjane atakayekuwa amebakia kutoka familia nyingine iliyo na uwezo wa kuilea familia iliyobaki.
 
Maige kachanganyikiwa baada ya kupigwa chini halafu wewe Nape usijifanye wewe msafi sana wakati hujawahi kufanya chochote kwenye taifa letu zaidi ya maneno mengi.

Maige alikuwa wapi leo atamke Nape avue gamba? Angezungumza akiwa waziri tungemwelewa asubiri apigwe chini atafute wa kufa nae? Mbona hakuzuia twiga kupanda ndege wakati alikuwa na dhamana ya uwaziri, Nape anasaidia kukabidhi Nchi kwa Cdm anafanya makusudi kuibomoa mwishoe atamfuata Millya subirini muone pamebaki padogo.
 
Hahahaha! Safi sana Nape mwambie huyo Maige wale wanyama wetu vipi aturudishie kwanza Twiga wetu!
 
Nikiwa mtanzania halisi nilie zaliwa ktk taifa langu teule Tanzania naunga mkono jitihada za ccm, viongoz wote wa cc kuanzia Mwenyekit mpaka katibu mkuu Nape Mnauye zakukisafisha chama. Nia yangu nikusema mpaka J. K anamaliza muda wake na mafisad weng watakuwa wamekauka.

Kwa mfano kile kinacho fanywa na alie kuwa wazir wa Maliasil mh Maige sio kitu chakukinyamazia, anaichonganisha serikal na wananch wake, chama na makada wake, jambo ambalo nikinyume na sheria za baraza la mawaziri na Ethics za uongozi, Mh maige anataka kuwada umma wa watanzania kwakujikosha yeye ni msafi na kwamba ameonewa.

Mimi nadhani Mh Maige hawezi kuizidi nguvu serikal na usalama wataifa, nilazima akumbuke alipo apishwa kuwa waziri aliapa kutunza siri za baraza la mawaziri hivyo kujifanya analipua siri nzito nikujikaanga yeye mwenyewe ktk mafuta aliyojichemshia.

Watanzania tukumbuke huyu alikuwa waziri mwenye dhaman ya Umma wa watanzania, yapo mambo amekosea, ipo harufu yakunuka ufisadi na asifikiri ataendelea kuongopea uma muda sio mrefu atawajibika kama wengine walivyo wajibishwa ajuwe wapiganaji wapo kwenye mapambano na ni mpaka tone la mwisho la damu na jasho la watanzania litapiganiwa.

Akumbuke cheo ni dhamana na sio kufikiri atakuwa Mungu mtu.
 
Maige aache kumchafua Nape ajipange upya sio kukulupuka ovyo, I think kumwagwa uwaziri kumemkuta unprepared ndo maana kila kukicha analalama pole mwee , ushauri wangu kwa Maige kule kwetu Masanza Bubinza kuna fisi wengi kama vipi tuanzishe mbuga yetu itatulipa in future
 
MaIGE alikuwa wapi siku zote kusema haya? huuyu jamaa kachanganyikiwa huyu si bure
 
Na bado tutayasikia mengi na tutayaona mengi tumezoea kuona wabunge nchi nyingine wakishikana mashati sasa subilini kuona wana ccm wakishikana mashati kwenye majukwaa na kwenye vikao vyao. Tanzania raha sanaaaaaaaaaaa!!!!!!!
 
Unajua Maige anaweza akawa na hoja ya msingi kabisa au kunakitu anakijua lakini kwakua hakusema enzi ni waziri kwa maslah ya kulinda meza sasa hiv watu hawamuelewi,mi nazani akisikilizwa na akachimbuliwa anamengi,mi najua mbali na ubadhilifu kwa kutumi report ya CAG lakin inaonekana kabisa kunakitu anakijua ambacho huwenda alikitaa na anaamini ndicho chanzo cha kumtoa kwenyd uwazi.Mtakuja kuniambia

Mkuu na kama asingetolewa uwaziri angesema lini yote haya???
Akisikilizwa na kuchimbuliwa wapi na nani, kwa faida ya nani???

Kama kuna kitu anakijua ye aweke wazi sisi tutachuja na kupima na kumuweka kila mtu katika kundi lake......tatizo la mabwana wakubwa hudhani wananchi tunawachukulia for granted.......tunaangalia kwa umakini na nadhani tunajua silka za kila mmoja wao na personalities zao as wao ni binadamu kama sisi na wala wasidhani watu wanafuata kila wanalosema eti kwa kuwa yeye ni au alikuwa kiongozi.....no way we go with contents, time, audience, power relations, personal vs institutional relations and the likes.....it is only that wao wana access na media kuliko sisi. Na kwa viongozi walio humu JF wanalijua hili waaaazi kweeeupeee na ndio maana wengi wa walio humu wako kean na maneno yao na wakisema wanajua fika wananchi tutahoji for clarity or validity if need be

Hatutakuja kukuambia wala nini......postmorteum hazina nafasi kwa siasa na maendeleo ya sasa ndo maana wenzetu hadi baadhi ya mission za serikali huanikwa kama story baada ya kuwa hazina effect.....fuatilia RT utaona majasusi wakitoa ushuhuda wa mambo ambayo yalikuwa classified....embuse waziri mstaafishwa bana..!!!!!!!
 
Tatizo kubwa la Nape ni kujifanya mtetezi wa wanyonge wakati pamoja na kelele zake tupu haelekei yeye na wenzie ndani ya NyinyiEM hawachukui hatua madhubuti kudhibiti hawa ambao leo anawaita wezi na wahujumu wa mali za umma!!
Kama Nape kweli ni mtetezi wa wanyonge mbona kila siku husikika akizinanga na kukashifu juhudi za kweli za CDM za kukomboa wanyonge na kulinda raslimali za Taifa??! Nape alifahamu lini kwamba Maige ni mwizi na alichukua hatua gani mbona maige bado ni mwana NyinyiEM?!
Nape hatudanganyiki, mikakati ya kujivua gamba uliyoipigia debe kwa nguvu zote mbona mpaka leo imekwama, wapi utekelezaji wake, umebakia kusubiri watu wajivue magamba ndipo ukimbilie kwenye vyombo vya habari kuwananga eti walikuwa mizigo!!
Hadanganyiki mtu hapa ni kweli Maige has a point; chama kinapukutika wewe unashangilia !!
 
"Waarabu wa Pwani wanajuana kwa vilemba vyao"Nape na Maige wote ni magamba lazima gamba moja limnyooshee kidole gamba lingine.
 
Haya maneno ya maige yangalikua dhahabu kabla na siyo sasa. Golden opportunity never comes twice.
 
namlaumu sana JK sijui alimpata wapi huyu Mwehu EM. Maana anabwabwaja kama mwanamke aliyepewa Talaka kwa kufumaniwa
 
Lakini Jamani Maige amennepa kwenye hiyo picha jamaa amenona mafuta kibao teh teh teh :happy:
 
Ulipo kuwa waziri hukuliona hilo?au baada ya kuvuliwa uwaziri ndiyo umeliona? Na yeye atakuita ww ndiyo gamba baada ya kupigwa chini. siasa wakati mwingine burudani na nimachungu wakati mwingine.
 
Back
Top Bottom