Bujoro
JF-Expert Member
- Jan 30, 2018
- 3,143
- 2,278
Nimefanya tafiti zangu kwa baadhi ya walioko kwenye mahusiano
ambao wanasema wamechokana bwana kamchoka bibi au bibi kamchoka bwana,, nilichogundua na kujifunza ni kwamba siyo mtu kumchoka mtu,,, maana mwingine anasema niko nae kwaajili ya watoto ila nimemchoka sina la kufanya, nashindwa kumuacha kwaajili ya wanangu tu. Tatizo siyo kuchokana kabisaaa, siyo mtu kumchoka mtu....
Tatizo lililopo ni kuzichoka tabia ngeni zinazojitokeza kwa mwenza wake , watu wanachoka kuumizwa mara kwa mara, wanachoka kudanganywa, wanachoka kudharauliwa,
wanachoka kupuuziwa, wanachoka kuona makosa yaleyale yanajirudia kila siku kisa tu ataomba msamaha yataisha bila kujua anamuumiza vipi mwenziwe, wanachoka kusubiri labda atabadilika labda ataacha tabia hii labda atapunguza, watu huchoka tabia mbaya za mtu na siyo kumchoka mtu , wanadamu tumeumbiwa upendo na upendo uko palepale isipokuwa uchungu na maumivu vikishaingia ndani ya moyo basi vinazaa chuki na chuki ni mbaya huleta hasara,,
Kubali kubadilika, sema na mwenzio usikae na uchungu moyoni, epuka kumkwaza mwenzio na ikitokea rekebisha na ubadilike msiishi kwa mazowea kwasababu changamoto zipo nyingi tu ila dawa yake ni kuzikabili na kuzitatua kwa busara na hekima..
hakuna mtu bingwa wa kusamehe sawa anaweza kukusamehe mara ya 1, 2, 3 hadi ya 10 au 100 lakini siku atakapo choka tabia zako na kuchoka kusamehe na kuumizwa na wewe ndipo utajua atachukua maamzi magumu ambay unaweza yajutia milele na hata utakapo amua badilika utakuwa umechelewa sana maana hana mda wa kukupa last chance tena.. Majuto atakuwa mjukuu wako ,amua sasa kubadilika leo hii, sasa hivi kama ni warembo na wazur wapo wengi htakaa uwamalize utakufa utawaacha kama ukivozaliwa unawakuta, wenye pesa na mahandsome yapo tu na utawaacha pia ni hayo tu leo.