Mahusiano yanapovunjika, wanawake ndio huumia zaidi...!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
Kwa kuangalia idadi ya watu wanaoathirika kufuatia kuvunjika kwa uhusiano kati ya mwanamke na mwanaume mtu atagundua kwamba wanawake ndiyo ambao hupatwa na athari kubwa zaidi. Kwa mfano ukichukua watu ishirini, wanawake kumi ambao wameachwa na wapenzi wao na wanaume kumi ambao nao wameachwa pia na wapenzi wao, utagundua kwamba, wakati ni wanaume watatu tu kati ya hao kumi ndio watakaosumbuliwa sana na na hali hiyo, kwa wanawake idadi itakuwa ni saba kati ya hao kumi.

Watu wengi wanaweza kukimbilia kwenye kusema hali hiyo inatokana na utegemezi wa wanawake kwa wanaume. Hii ikiwa na maana kwamba, wanaathirika zaidi kwa sababu, kwa kuachwa ina maana pia kwamba hawataweza tena kupata mahitaji ambayo walikuwa wanapewa na wanaume hao. Dhana kama hii inaweza kuwa na ukweli fulani, lakini hali halisi inakataa. Kuna wanawake ambao wana uwezo mkubwa nap pengine ndiyo wanaowalisha na kuwavisha wanaume, lakini wanapoachwa na wanaume hao huathirika sana.

Wanawake wa aina hii inadaiwa kwamba huathirika zaidi kuliko wale walio tegemezi. Kuathirika huku kwa ziada huhusishwa kwa kiasi kikubwa na ukweli kwamba wanaume ni watu wa kutoa ili kupalilia penzi, lakini hapa badala ya kutoa wanapewa na bado wanaondoka. Hili huwatanza wanawake wa aina hii. Lakini sababu ambayo huenda wengi wetu tulikuwa hatuijui kuhusiana na suala hili la wanawake kuathirika zaidi baada ya kuvunjika kwa penzi au kuachwa ni ndoto. Kimaumbile wanawake huota zaidi ndoto za mchana au hufikiria zaidi kuhusu maisha yao ya kimapenzi yatakavyokuwa ukilinganisha na wanaume. Siyo kufikiria tu, bali hufikiria kwa njia inayoonyesha kuwa maisha hayo yatakuwa kama peponi.

Wanawake, wakiwa bado wasichana (baada ya kuvunja ungo) huanza kufikiria na kupiga picha jinsi busu lao la kwanza litakavyokuwa, mtu ambaye watabusiana awali. Hufikiria pia kuhusu wapenzi wao wa awali watakavyokuwana jinsi itakavyokuwa watakaposhiriki nao tendo kwa mara ya kwanza na huwa wanapiga picha ya jinsi siku yao ya harusi itakavyokuwa na watu watakaowaona. Katika kupiga picha huko huwa wanafikiria namna ambavyo mambo hayo yote yatakavyoenda vizuri bila doa, huwa wanajiona wakiwa wamefanikiwa katika hatua zote na hatimaye kuishi kwa raha mustarehe milele na watakaokuwa wapenzi wao. Kwa upande wa wanaume hakuna ndoto za aina hii na hata kama zipo ni kwa wachache sana, wakati kwa wanawake ni kama sehemu ya makuzi kwao.

Kwa hali hiyo, ukiacha mazingira wanamokulia wanawake, kwa sehemu kubwa hukua wakiwa na hizo ndoto zao, ambazo kwao siyo ndoto bali ukweli. Wanapokuja kwenye ukweli wa uhusiano hugundua kwamba busu la awali siyo kama walivyotegemea liwe, mpenzi wa awali siyo kama walivyomtegemea awe na wala maisha ya ndoa siyo matamu kama walivyokuwa wameota. Kwa kuwa hawakujiandaa wala kutegemea mazingira magumu ya uhusiano, hawakuwa wakiota kuhusu ugumu wa uhusiano bali wororo, wanapokutana na masuala ya kuvunja moyo kama kuachwa hubabaika sana. Kwa kuwa akilini mwao walikuwa na picha ya mafanikio katka uhusiano, kushindwa kwa uhusiano, huwafanya wajione kwamba, wao ndiyo wakosaji, wameshindwa kulinda uhusiano ambao katika ndoto zao waliamini kwamba ni mzuri na usio na doa

Ukiangalia kwa makini katika uhusiano, wanawake ndio wanaojitahidi sana kulinda uhusiano usivunjike, wao ndiyo wavumilivu zaidi, ndiyo ambao hujitahidi kuyarudisha mambo yaende sawa pale yanapokwenda kombo hata kama kufanya hivyo kunawagharimu. Yote hii ni juhudi yao ya kutaka kuishi kwa kadiri ndoto zao za kabla zilivyowaonyesha, kwamba uhusiano kati ya mwanamke na mwanaume ni mtamu, mororo na usio na chembe ya doa

Kesho nakuja na mada, kwa nini wanaume wengi hawapendi kuoa siku hizi!
 
Mkuu umenena vema sana. Kuhusu day dreaming ni kweli kisaikolojia mwanamke huwa na daydreaming nyingi sana zinozohusu mahusianao ya kimapenzi na mara zote mapenzi yanapoenda kombo kwao huwa ni hatari sanatofauti na wanaume ndio maana kuna msemo "MAPENZI YA MWANAMKE YAKO MOYONI ILA YA WANAUME YAKO KICHWANI"...

Nachojua siri kubwa ya kusolve ishu ya kuachwa ni kuendelea na day dreaming wakati uhusiano ni mbovu. Hii kwa wataalamu wa metaphysics & law of attraction huwa na effect kubwa sana kuchange hali ya mambo
 
Nausubiri mjadala wako wa kesho...

Ila kwa uzoefu wangu mie sikuumia kihivyo....labda kwa vile nilikua mtu wa kuacha na si kuachwa..... ingawa kipindi cha mpito huwa kinaumiza kidogo.

Acha waje wlioumizwa watupe experience, kwa nini binadamu mlokutana wote na meno 32 akuumize moyo?
 
nausubiri mjadala wako wa kesho...

ila kwa uzoefu wangu mie sikuumia kihivyo....labda kwa vile nilikua mtu wa kuacha na si kuachwa..... ingawa kipindi cha mpito huwa kinaumiza kidogo.............

acha waje wlioumizwa watupe experience, kwa nini binadamu mlokutana wote na meno 32 akuumize moyo?

BT, mmi nakumbuka niliacha ilihali bado napenda but sikuwa na jinsi. oh no by that time i thout it was end of my life. aah baadae nikazoea tu. sasa nimekua mwalimu na ambassador. looh maisha haya ni shule
 
unaona eeeh,
ukishasoma alama za nyakati, au kama mtu hasomeki, kila siku unaambulia maumivu, heri uumie muda mfupi kumuacha kuliko kuumia muda mrefu kwa kuuguza donda sugu.....

naamini mapenzi ni kutake risk, na kwenye mapenzi maumivu hayakosekani... loh



BT, mmi nakumbuka niliacha ilihali bado napenda but sikuwa na jinsi. oh no by that time i thout it was end of my life. aah baadae nikazoea tu. sasa nimekua mwalimu na ambassador. looh maisha haya ni shule
 
Pamoja na ukweli kwamba wanawake wanapenda kwa moyo wakati wanaume wanapenda kwa akili kama alivyosema asigwa na jeneneke, pia kuumia zaidi kwa mwanamke kunatokana na ukweli kwamba wao kupata replacement (mwenza mwingine) ni ishu zaidi kuliko kwa mwanaume
 
Nitakuwa na mengi kesho....

Kwa hili la leo kwaa uzoefu nimeshuhudia wote tunaumia tu, inategemea na mahusiano yenyewe na mtu uliyapa uzito gani na jinsi ulivyopagawa na mwenzio na jinsi mnavyoachana....

Kila sheria ina "exceptions" zake!
 
maumivu ya utegemezi wa 'material needs' ni afadhali kuliko maumivu ya utegemezi wa kihisia.

Mie sikubaliani na hii hoja moja kwa moja.
Kwani Whitney Houstoni alikuwa anamtegemea Bobby Brown kwa lipi?
Nadhani alikuwa tegemezi kihisia kuliko ki-material.
 
Nitakuwa na mengi kesho....

Kwa hili la leo kwaa uzoefu nimeshuhudia wote tunaumia tu, inategemea na mahusiano yenyewe na mtu uliyapa uzito gani na jinsi ulivyopagawa na mwenzio na jinsi mnavyoachana....

Kila sheria ina "exceptions" zake!
Kwa kuangalia idadi ya watu wanaoathirika kufuatia kuvunjika kwa uhusiano kati ya mwanamke na mwanaume mtu atagundua kwamba wanawake ndiyo ambao hupatwa na athari kubwa zaidi. Kwa mfano ukichukua watu ishirini, wanawake kumi ambao wameachwa na wapenzi wao na wanaume kumi ambao nao wameachwa pia na wapenzi wao, utagundua kwamba, wakati ni wanaume watatu tu kati ya hao kumi ndio watakaosumbuliwa sana na na hali hiyo, kwa wanawake idadi itakuwa ni saba kati ya hao kumi.
Mkuu naamini kipengele hicho hapo juu kinahusika sana kujibu kauli yako...........................
 
Hili ndo jibu nilitaka kutoa.
"MAPENZI YA MWANAMKE YAKO MOYONI ILA YA WANAUME YAKO KICHWANI"...

Halafu Mtambuzi hao maharusi hapo juu nawafahamu huyo kaka ni mmalawi anafanya mahali fulani naenda kumwambia umetoa picha yake bila idhini yake akudai fidia..

Unajuaje kama katoa bila idhini yao?huenda yeye pia anawafaham
 
"Women treat friendship like glass and it break, men treat friendship like football but do not get crack"
 
I totally disagree mzazi.
Wanawake wanaweza ku-move on haraka sana kwa sababu ni wepesi ku-seek support kutoka kwa wanawake na wanaume pia (emotionally)
Wanawake wanaotegemea wenzi wao ndo wanaishia nahisi. Ngoja nimalizie sikukuu, keshooo tutajadiliana hili. Navuna ufuta
 
I totally disagree mzazi.
Wanawake wanaweza ku-move on haraka sana kwa sababu ni wepesi ku-seek support kutoka kwa wanawake na wanaume pia (emotionally)
Wanawake wanaotegemea wenzi wao ndo wanaishia nahisi. Ngoja nimalizie sikukuu, keshooo tutajadiliana hili. Navuna ufuta

Tatizo mtoa mada kawalundika "Wanawake" wote kama akili yao moja vile.

Ndio maana nikauliza wanawake wanaozungumzwa hapa ni wanawake wepi?

Sijapata jibu.
 
Halafu Mtambuzi hao maharusi hapo juu nawafahamu huyo kaka ni mmalawi anafanya mahali fulani naenda kumwambia umetoa picha yake bila idhini yake akudai fidia..
Hizi picha naziweka kwa makubaliano na wahusika na wengine wapo humu humu JF
 
Back
Top Bottom