Mahusiano yalimfanya rafiki yangu kuwa kichaa

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,270
40,080
Miaka mingi iliyopita kidogo baada ya kuhitimu chuo, nilianza kutafuta ajira za hapa na pale..kutokana na ufinyu wa ajira nilitafuta shule moja nikawa nafundisha kwa hapa Dar es salaam. Baada ya kama miezi kadhaa hivi kuna rafiki yangu mmoja baharia mzoefu, yeye alikuwa akifundisha shule moja wilaya ya Mwanga kilimanjaro; akaniambia, kaka unalipwa kiasi gani huko..hebu njoo huku mkoani ujipange vizuri ndio urudi mjini.

Basi tukaweka mikakati nikaenda mwanga kilimanjaro, baada ya kukaa kama siku mbili tukaenda huko milimani (milima ya pare) kutafuta shule za kufundisha. Mazingira ya kule yalikuwa mazuri sana, hali ya hewa safi ya ubaridi baridi, vyakula bei nafuu, maziwa, mayai n.k moyoni nikasema nabaki huku huku sirudi mjini.

Basi nikapata shule, na baada ya siku tatu nilitakiwa kuripoti...baada ya kuripoti nikapelekwa kwenye nyumba waliopanga wafanyakazi wenzangu ambao walikuwa ni mabachela. Nyumba kubwa kila mmoja na chumba chake ila mnashea sebule. Maisha yalikuwa ni ya furaha sana, tulikuwa tunakula vizuri, tunabadilishana mawazo ya hapa na pale, tunatafuta wahudumu wanatusafishia nyumba, kutufulia n.k

Pamoja na ujana lakini tulikuwa na akili za kutafuta shilingi..mle ndani kila mmoja ilibidi anunue boda boda yake (zile kubwa) huku tukitafuta shule zingine za part time ili kuongeza kipato. Mambo yalienda vizuri kutokana na jitihada tulizojiwekea kipindi hicho.

Nakumbuka ilikuwa mwezi wa kumi na mbili karibia na sikukuu..wengi tuliondoka/safiri kwenda kusherehekea sikukuu na ndugu zetu. Kwenye ile nyumba tulimuacha rafiki yetu mmoja yeye alisema hataondoka. Alikuwa ni mpole, hatumii sigara, pombe wala kilevi chochote kile. Nashangaa baada ya sikukuu kupita na kurejea kituoni kwa kazi, mbaya zaidi tulipofika tulikuta yule rafiki yetu amebadilika kweli; amekuwa muongeaji sana, mlevi, anavuta sigara, anapenda wanawake, wakati mwingine akili zinamruka anakuwa kama kichaa, wakati mwingine anatoka huko milima ya pare anaeda moshi mjini na akifika huko anapatwa na kichaa mpaka anakamatwa na mapolisi na baadaye anaachiwa.

Ilibidi kama kamati ya mabaharia tuchunguze ni kitu gani kimembadilisha huyu jamaa, kuanzia tulipomuacha hadi kuwa na hali hii;...kwa kuulizia ulizia ilisemekana, siku ya mkesha wa sikukuu, alikwenda kwenye mgahawa fulani kula...ndipo alipokutana na jimama aliyetokea Dar na kuja huko upareni kwa ajili ya sikukuu; katika mazungumzo yao wakajikuta wameingia kwenye uhusiano, na wakachukuana na kwenda kulala naye mle ndani...alichompa anajua mwenyewe. Baada ya kufanya naye lile tendo ndipo jamaa akabadilika.

Ofisi ilitoa taarifa kwa wazazi wake ili waje wamchukue ndugu yao kwa ajili ya matibabu na mila. Mpaka leo najiuliza yule jimama alimfanya nini yule rafiki yetu?
 
Wapare washirikina Sana itakuwa alilogwa ashukuru Mungu hawakugandana. Yani uko upareni waiba mke wa mtu chineeke
 
Back
Top Bottom