Mahusiano ya Zamani Vs Mahusiano mapya, Yananipa wakati mgumu wa kufanya maamuzi... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahusiano ya Zamani Vs Mahusiano mapya, Yananipa wakati mgumu wa kufanya maamuzi...

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by tindikalikali, Sep 30, 2012.

 1. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  Habari zenu wana JF, naamini wote ni wazima.

  Husika na kichwa cha habari hapo juu, Mimi ni kijana mwenye miaka takribani 26. Mwaka 2006 nikiwa masomoni katika mkoa mmojawapo hapa Tanzania, nilitokea kumpenda msichana ambaye alikuwa akisoma shule jirani na ile tuliyokuwa.
  Nilifanya kila jitihada za kumzoea na kumwambia yale yaliyokuwa moyoni mwangu. Hapo ndipo safari yenye utata na machungu mengi ilioanzia, huyo binti hakutaka hata kunisikia. Nilikutana na kila aina ya dharau na ukatishaji tamaa. Ni wazi alionesha kutonipenda kwa namna yeyote lakini cha ajabu niliendelea kukomaa huku nikiamini kuna siku mambo yatakaa sawa.
  Hali hiyo iliendelea mpaka nilipomaliza form 6, hapa nataka kusema niliondoka mkoa huo ambao mimi sikuwa mwenyeji pasipo kukubaliwa kwa lolote.

  Niliendelea kuwasiliana naye, na alikuja kunikubalia miezi miezi mitatu mbele. Tuliendelea kuwasiliana kama wapenzi japo kwa mawasiliano ambayo yalikuwa yakinipa shaka.[ningefanyeje na nilishapenda?]

  mwezi october wa 2008 nilifunga safari toka DSM ambako nilikuwa nimeshaanza masomo ya chuo kikuu, na kwenda kumtembelea huyo binti. Nilijiandaa kweli kweli huku nikijua kwamba naenda kulijenga penzi jipya. Niliyoyakuta sitaki hata kuyakumbuka mpaka leo, nilikanwa na yule binti na akadai alifanya makosa kunikubalia, na moyo wake huwa unamsuta akiniita mpenzi. Sikuwa na jinsi, niliondoka nikiwa na majonzi tele, kwa kifupi aliuvunjavuja moyo wangu, nilikaa kimya pasipo kuwasiliana naye hali iliyomfanya naye akae kimya.

  Baada ya hapo mara nyingi amejaribu kurudi, ila kila nilipokuwa nikimuuliza msimamo wake kwangu alikuwa akiruka kimanga
  Maisha hayakusimaa, nilipiga moyo konde na kuamua kusonga mbele.

  TATIZO LINAPOANZIA...
  Hivi karibuni [hata wiki mbili hazijapita], nimefanikiwa kuanzisha mahusiano mapya. Huyu binti niliyenaye kwa sasa bado sijamsoma kiundani, hasa ile nia ya dhati aliyonayo juu yake, bado simuelewi elewi ila sina shaka kwa kuwa nampenda, bado nampa muda.

  TATIZO ZAIDI NI HILI HAPA...
  Yule binti aliyenikana 2008 anarudi tena kwa speed kubwa, anadai anatamani kuishi na mimi katika maisha ya ndoa....hizi ni sms zake za jana na leo...
  "mcmamo wako wa maisha ya upendo ulonao unanivuta kuja kuish nawe je umeplan lini uishi maisha ya ndoa"....sikujibu hii sms yake, na leo asubuhi katuma hii sms...
  "Mapenzi ya kweli huchukua muda kujengeka, na yakijengeka ni vigumu kuisha.)kwel nw napata hamu ya kuishi na mwanaume nahc unanifaa ktk maisha yangu,labda kama nimechelewa kufunguka moyo plz dont tell me dat im late."....

  NASHINDWA KUFANYA MAAMUZI...
  Huyu wa zamani nampenda na yeye analijua hilo, ila hii gia aliyokuja nayo ya kutaka ndoa na kunipenda kwasababu tu nampenda vinanitisha kidogo. Na huyu mpya sina hakika kama kweli kanipenda, maana kwa mahusiano tuliyonayo yananiaminisha hivyo.
   
 2. b

  blackwizard Senior Member

  #2
  Sep 30, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 163
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  akili kichwani asikufunde mtu umpende yupi
   
 3. MKATA KIU

  MKATA KIU JF-Expert Member

  #3
  Sep 30, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,167
  Likes Received: 966
  Trophy Points: 280
  Nyinyi ndo Lala 1 anawaita Mazombi, yaan hata hiyo inakushinda...

  Mtoto wa sekondari anakuzidi ujanja mtu mzima,,,, yaan akitaka anapotea na akitaka anarudi,,,

  wacha nimalizie report ya assigment nikamuingizie patner midolari
   
 4. promiseme

  promiseme JF-Expert Member

  #4
  Sep 30, 2012
  Joined: Mar 15, 2010
  Messages: 2,715
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 135
  Anakufanya kama toy akitaka kukuchezea anakuchukua na akishakuchoka anakutupa store, ebu jiulize je uko tayari kufanywa kama mtoto? sasa anakuja anataka ndoa keshafujwa uko wewe ndio wakuchukua matapu tapu,ebu kaza roho yako na jipe hadhi ya kiume...
   
 5. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #5
  Sep 30, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  wa zamani, keshatendwa na dunia.
  Ameamua achegue zombie mmoja katika kundi la mazombie wake na kura imekuangukia wewe.

  Kwa maelezo zaidi nakuitia lara 1 na The Boss.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Dr. Wansegamila

  Dr. Wansegamila JF-Expert Member

  #6
  Sep 30, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 1,233
  Likes Received: 819
  Trophy Points: 280
  Ni ngumu sana kutoa ushauri katika swala la mapenzi,
  Uamuzi unao wewe, lakini ni vema kwanza kujiuliza kwa nini huyo wa zamani amerudi? Je, ni kwamba she is desperate?Anataka kuolewa, na muda umeenda akaona arudi kwako sababu anajua unampenda? Nini kimembadilisha? you have to know that, umuulize na akujibu uridhike na majibu yake, pia wewe ndo unamjua ni msichana wa aina gani and what she is capable of........ kinachonitisha mimi kwa huyo wa zamani ni hiyo ya yeye kung'ang'ania ndoa, am worried she is desperate.
  All in all, the decision is yours mkuu, all the best!!!!
   
 7. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #7
  Sep 30, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Huyo wa zamani anacheza na feelings zako!!Ameshajiaminisha kwamba bila yeye wewe huwezi songa mbele.Mie ningekushauri uendelee na hilo penzi jipya kwa vile kuna kaupendo kameanza kujengeka!
   
 8. kazikubwa

  kazikubwa JF-Expert Member

  #8
  Sep 30, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Inaonyesha umemaliza Form six ukiwa na miaka 20, kwa wanafunzi wa kidato hicho wewe ulikuwa kijeba sana ndiyo maana hukumvutiwa nawe. Kwa sasa matarajio ya mwenzako yametoweka hivyo anaona arudi kwako kama last resort. Siumi maneno huyo hakufai, "Najuta kwanini nilikueleza kuwa nimekukubalia" kauli hii ya huyo binti inatosha kukupa dira.
   
 9. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #9
  Sep 30, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,347
  Likes Received: 2,683
  Trophy Points: 280
  mbona umenisahau na mimi jamani Kongosho...mzima lakini wewe?
  Ngoja nimpe somo huyu ndugu halafu The Boss na lara 1 nao watakuja kandamizia.
  tindikalikali, ni hivi mapenzi huwa hayaanzi kwa bahati mbaya. Ni mkusanyiko wa fikra za matamanio na shauku ya kutaka kuwa na fulani. Kifupi ni kuwa maamuzi ya kuanza au kuacha kupenda yapo ndani ya fahamu zako. Mapenzi ni ya mioyo miwili, ni jukumu la watu wawili, moyo mmoja unapopenda usipopendwa hapo sidhani kama tutasema kuna mapenzi.
  Ngoja nikupe ukweli,huyo binti hakuwahi kukupenda wakati uliompenda na wala hakutaka kukufahamu zaidi ili walau ajue haja ya moyo wako. Kuna udhaifu mmoja ambao mabinti wengi huwa nao, uwezo mdogo wa kutambua nani hasa anamhitaji maishani, je ni yule kijana mwenye elimu, pesa, au mwenye upendo wa dhati. Amini usiamini wewe unayeonesha kujali unaweza ukatoswa na penzi akapewa Nyangema anayeishi mtaa wa pili kisa tu anajua kuvaa na kupiga pafyumu.
  Ushauri wangu ni kwamba achana na binti wa awali, angalia maisha yako vile unataka yawe, jipe nafasi ya kumjua huyu binti uliyenaye na si ajabu pia huyu uliyenaye asiwe ndiye utakayemuoa. Yote hayo ni sehemu ya maisha, jifunze kutokana na yaliyopita ili wakati ujao usifanye tena kosa.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #10
  Sep 30, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,841
  Trophy Points: 280
  Daaaaah huyo wa zamani hakupendi wala usidanganyike kabisa, ameshatendwa huyo namtu sasa na yeye ameona kwako ndio kwa kupumzikia.

  Hata ukimkubalia lazima atakuja kukukana tu.

  Nakushauri we mchunguze huyo mpya kama ana kufaa!
   
 11. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #11
  Sep 30, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,325
  Likes Received: 2,320
  Trophy Points: 280
  The Boss ni retired zombie?? nimeuliza tu
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #12
  Sep 30, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  una utani naye??
  Am out, sitaki shuhudia damu yako ikimwagika.

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #13
  Sep 30, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,325
  Likes Received: 2,320
  Trophy Points: 280
  Wewe ndiye umeanzisha habari ya zombie......na itabidi uklozi mwenyewe
   
 14. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #14
  Sep 30, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,123
  Trophy Points: 280
  Sema wewe, manake mimi mdomo unaanza kupinda. UMEONA MIDUME INAVYOPENDA YENYEWE UZOMBIIIII!
   
 15. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #15
  Sep 30, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,123
  Trophy Points: 280
  Hahahahahaaaaaaaaaaaaaaaa! MIMI CHICHEMIIII!
   
 16. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #16
  Sep 30, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,123
  Trophy Points: 280
  Kazikubwa wewe ni kazi kwelilkweli, eti KIJEBAAAA! LOL!!!!
   
 17. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #17
  Sep 30, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  mkuu nilikuwa na 22,
   
 18. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #18
  Sep 30, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  hapo kwenye red umesomeka mkuu
   
 19. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #19
  Sep 30, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Kama muoaji kweli hebu angalia humu...kuna vitu nimeviona..nadhani vinaweza kukusaidia..

   
 20. BRO LEE

  BRO LEE JF-Expert Member

  #20
  Sep 30, 2012
  Joined: Dec 25, 2011
  Messages: 580
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Unatakiwa kufahamu kwamba mapenzi ya kweli hutokea ndani bila ya kuwa na ushawishi wa aina yoyote, unaweza kumshawishi m2 kukupenda iwapo kuna sababu ya kufanya hivyo kwa mf iwapo anaonyesha kukupenda lkn ana hofu au hajiamini kuhusu mambo kadhaa.

  Kumshawishi asiyekupenda wala kuonyesha kujali hisia zako ni kupoteza muda tu, na kwa maneno machache unakuwa king'ang'anizi. Sasa unaweza kukubaliwa wakati mwenzio anatega ampate anayempenda jambo ambalo litakuumiza sana hapo baadaye atakapo anza visa ili mtengane.
  Halikadhalika kwa kuwa bibie anatambua unampenda sana basi unaweza kuwa mtumwa wa penzi lenu kwa maana wewe ndo utakuwa umelibeba c unampenda sana bwana na hutaki kumpoteza!

  Kwa mtizamo wangu huna haja ya kumng'ang'ania asiye kupenda imarisha penzi kwa huyo mwingine km anamwelekeo, wahaenga walishanena mpende akupendaye kwani ni adhabu kumpenda asiye kupenda.
   
Loading...