kwetumasoko
JF-Expert Member
- Aug 24, 2016
- 866
- 518
Wakuu,
Nipo hapa kituo cha Polisi kwa masuala yangu binafsi, ila nimekutana na kesi moja, kuna jamaa kawekwa ndani na mpenzi wake wa kike. Katika uhusiano wao, wamejaliwa kupata mtoto mmoja ambaye ana miaka 2 katika mahusiano yao katika Chuo Kikuu kimoja.
Jamaa kalala Rock-up ana siku mbili, kisa si unajua tena katika uhusiano wa mapenzi kuna kusaidiana. Mmoja anapokuwa na shida, na ikaonekana mwingine anaweza kumsaidia mwenzie, basi inakuwa hivyo kuonyesha mapenzi ya kweli, kupeana fedha pamoja na vitu vingine.
Sasa issue iko hivi, mwanamke anadai katika mahusiano yao alimpa jamaa laptop na shs. 1,000,000/= wakiwa chuo. Inavyoonekana mahusiano yao tayari yameshaharibika, jamaa kamtosa mwanamke kutokana na kutoelewana katika mahusiano yao.
Mwanamke kakomaa, anahitaji laptop yake pamoja na fedha yake. Jamaa kawekwa ndani na amelala siku mbili. Naona jamaa zake ndo wanahangaika ili aweze kupata dhamani.
Sasa wakuu hii inakaaje?