Mahusiano ya kimapenzi

ISHERUHINDA

New Member
May 5, 2011
3
0
Wapenzi wasomaji habari za kazi? Mimi kuna jambo linanitatiza juu ya suala zima la kimapenzi. Jambo hili ni juu ya watu wenye tabia ya kubadili wanaume (Kwa wasichana na wanawake) na wanawake (Kwa vijana na wazee). Hivi inakuwaje mtu anamiliki mpenzi zaidi ya mmoja na wakati mwingine zaidi ya wanne?? Hivi ni kweli kwamba anapoonja asali kwa kila MZINGA ndipo hamu ya ASALI inapoisha?? AU Ni kipaji cha kufisadi maana UFISADI ni kujilimbikizia MALI na yule anayelimbikiza wanawake au wanaume si FISADI????................. Watu wengi usemekana uenda nje ya ndoa baada ya migogoro ya kifamilia na je, wale ambao hawajaoa na wanafanya kazi ya kuwabadili madada wa watu??????...............
 
Ni tamaa na roho ya uchu wa kimapenzi kwa kujiendekeza na kuendekeza uzinifu tu.
Hapa nawatoa wale waliyo na mke zaidi ya mmoja kisheria tu.
 
Ni imani potofu tumejijengea sisi vijana unapobadili sana basi unaonekana wewe ni ndio wewe (sijapata neno la kulezea hii tabia) ila Umalaya sikuhizi vijana tunaona ni sifa. walio ndani ya ndo na wasio ndani ya ndoa..... na tukiendelea hivi ukimwi hautokwisha.
 
Baadhi husema mechi za nyumbani zimewachosha wanahitaji mechi za ugenini
 
Ni tamaa tu za mwili na kutokuwa bize unaishi kupenda kila demu anaipita, mwisho wa siku unaweza achana na mtu akupendae toka moyoni ukawa kiruka njia hii ndo maana yule kijana kaimba eti unatema bigG kwa karanga za kuonjeshwa..... Ile sentensi ina maana kubwa sana na mchango mkubwa kila uingiapo kwenye mawazo ya uchakachuaji
 
Ni tamaa na roho ya uchu wa kimapenzi kwa kujiendekeza na kuendekeza uzinifu tu.
Hapa nawatoa wale waliyo na mke zaidi ya mmoja kisheria tu.

penye red na kataa wote sawa tu niwazinifu tu na udhallishaji wa kina mama
 
hiyo ni moja ya zile tabia zilizoongelewa sana katika kitabu kitakatifu cha Mungu, kila aziniye hana akili kabisa, maana wanachafua hekalu la Mungu.
 
ukiwa na magari mengi ni utajiri sio?nyumba nyingi the same?
na wanawake wengi ni ujinga sio?
i didnt know that....lol
 
Wazinzi tu hao, hawana kipya wanachopata. Zaidi sana watajikuta na magonjwa yasiyo tibika.
 
maisha yana vijimambo na ndio hivo tena kila mtu anaishi kivyake, raha anayopata anaijua mtendaji na huwezi ijua mpaka ufanye hayo
 
maisha yana vijimambo na ndio hivo tena kila mtu anaishi kivyake, raha anayopata anaijua mtendaji na huwezi ijua mpaka ufanye hayo

halafu wanao jifanya wasafi ndo wanafiki mno.....
bora tulio wazi.....
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom