Mahusiano ya Kimapenzi sasa hivi ni 'full Comedy'

Bartazar

JF-Expert Member
Oct 4, 2011
1,043
565
Hii kitu imenitokea live, demu wng anayesoma UDSM mwaka wa mwisho, na tukiwa tumepanga mikakati mingi ya maisha ghafla akawa hapokei simu. Mwanzo nilidhani simu yake kaiacha mbali hasa ukizingatia mazingira ya kupanga nje ya hostels za vyuo husika, nikahisi kuwa huenda kaiacha simu room. Hivyo nikasitisha kwanza zoezi la kupiga simu, kwa lengo la kumpigia usiku, nikiamini kuwa muda huo pilika pilika zitakuwa zimeisha. Na kama atakuwa aliitelekeza simu yake, muda huo lazima atakuwa nayo, pamoja na imani yangu kuwa kuziona tu missed calls angepiga tu. Ajabu ni kwamba hakupiga, na nilipompigia bado hakupokea. Nikamtumia ujumbe bado haukujibiwa. Siku ya tatu alinitumia meseji, baada ya mimi kupiga sana na kumtumia ujumbe kuwa 'yupo bize' na maandalizi ya mitihani! Toka hapo mawasiliano yamekatika, hakuna simu wala meseji. Hivi naona ni viroja. Hivi waungwana ninyi mmesoma vyuoni wengi wenu! Katika hali ya kawaida mchumba wako au mpenzi wako akikupigia simu unaweza kubehave namna hiyo hata kama upo bize? Je, ni komedy gani hiyo ninayochezewa wanajukwaa?
 
Siku hizi mapenzi yamekuwa maigizo ukijifanya unampenda demu atakuumiza tu sex ndio imepewa kipaumbele. Mabinti wa chuo sio kabisa wengi wao ni vicheche wanawezana wao kwa wao. Huyo raia achana nae atakupotezea time mzazi
 
Ukiona manyoya ujue mnyama .......
Tupa kule, anza kwingine upya huku ukitanguliza mguu mmoja kwanza. Pole sana mkuu.
 
wajanja wameshajimegea, cha msingi tafuta kifaa kingine, usipime kina cha maji kwa miguu miwili wewe utazama shauri yako.
 
Mapenzi ya kibongo ni magumu kwa sababu tunasumbuliwa na njaa
 
Hii kitu imenitokea live, demu wng anayesoma UDSM mwaka wa mwisho, na tukiwa tumepanga mikakati mingi ya maisha ghafla akawa hapokei simu. Mwanzo nilidhani simu yake kaiacha mbali hasa ukizingatia mazingira ya kupanga nje ya hostels za vyuo husika, nikahisi kuwa huenda kaiacha simu room. Hivyo nikasitisha kwanza zoezi la kupiga simu, kwa lengo la kumpigia usiku, nikiamini kuwa muda huo pilika pilika zitakuwa zimeisha. Na kama atakuwa aliitelekeza simu yake, muda huo lazima atakuwa nayo, pamoja na imani yangu kuwa kuziona tu missed calls angepiga tu. Ajabu ni kwamba hakupiga, na nilipompigia bado hakupokea. Nikamtumia ujumbe bado haukujibiwa. Siku ya tatu alinitumia meseji, baada ya mimi kupiga sana na kumtumia ujumbe kuwa 'yupo bize' na maandalizi ya mitihani! Toka hapo mawasiliano yamekatika, hakuna simu wala meseji. Hivi naona ni viroja. Hivi waungwana ninyi mmesoma vyuoni wengi wenu! Katika hali ya kawaida mchumba wako au mpenzi wako akikupigia simu unaweza kubehave namna hiyo hata kama upo bize? Je, ni komedy gani hiyo ninayochezewa wanajukwaa?

Bora anayekata mawasiliano kuliko akupigie/au aku sms na kusema: "kuanzia leo tusijuane nimepata mwingine. Usinipigie wala kutuma meseji". Yaani unaweza kutupa simu chooni na kujuta baadaye.
 
Mwanangu tafuta mwingine gashi huyo kaona kama unamtegemea kiuchumi au labda anarudi kwao. Anatakumrudia mshikaji wake wa kitaa be care chalii au labda alikuwa anakuchuna sasa anaona anamaliza hataweza. Tena
 
Pole mkuu! Hao ndio aina ya wanafunzi wa kike tulio nao vyuoni. Katika suala hilo sioni ajabu maana uchumi huwa unabana sana chuoni especially kwa madada zetu na inafika kipindi hata wale wachache wasiokuwa na kale katabia ka kuwavulia wanaume ile nguo ya kwanza kuvaa na ya mwisho kuvua inawabidi wa-adapt hiyo tabia kutokana na vishawishi au ugumu wa maisha. Usijali kaka, hujapoteza kitu hiyo ni ajali ndogo tu sawa na kudondoka. Simama jipanguse na uendelee na safari yako kwa kutafuta mwingine pia mshukuru Mungu kwa kukuonyesha kuwa huyo sio chaguo lako halisi kwaajili ya kuishi nae kama wife.
 
hakuna kitu kinachouma,kama kutendwa na mtu ambae unampenda.utajikaza ila deep down unakuwa na maumivu,unachotakiwa ni kusonga mbele na maisha yako,mambo ya mapenzi uyape break kidogo
 
Si kasha kwambia yupo bize na maandalizi ya mitihani??

MWACHE MWENZIO ASOME
 
karibu kwenye ulimwengu wa mapenzi ya ki.com! usijali huo ni mwanzo wa safari yako ndefu sana katika ladha mpya ya malavidavi ya namna hiyo.... maana dunia ya sasa imejaa warembo na mabrother kama hao!!! usijali ndo unajifunza hivo, utakuwa mtaalamu na wewe tu baada ya muda..
 
shule imembana, na pengine ukimpigia unamuuliza maswali ya kumboa, mood ya kusoma inaharibika

ili asifell ameamua akuchunie kidogo, then baadae atarudi kwenye line

hata mie ilishanitkea hiyo, kila nikiongea na mtu lazima aniboe, kusoma tena inakuwa issue, nikaamua kuuchuna for three month ila mie nilizima sima simu na kuweka kwenye beg
 
Hii kitu imenitokea live, demu wng anayesoma UDSM mwaka wa mwisho, na tukiwa tumepanga mikakati mingi ya maisha ghafla akawa hapokei simu. Mwanzo nilidhani simu yake kaiacha mbali hasa ukizingatia mazingira ya kupanga nje ya hostels za vyuo husika, nikahisi kuwa huenda kaiacha simu room. Hivyo nikasitisha kwanza zoezi la kupiga simu, kwa lengo la kumpigia usiku, nikiamini kuwa muda huo pilika pilika zitakuwa zimeisha. Na kama atakuwa aliitelekeza simu yake, muda huo lazima atakuwa nayo, pamoja na imani yangu kuwa kuziona tu missed calls angepiga tu. Ajabu ni kwamba hakupiga, na nilipompigia bado hakupokea. Nikamtumia ujumbe bado haukujibiwa. Siku ya tatu alinitumia meseji, baada ya mimi kupiga sana na kumtumia ujumbe kuwa 'yupo bize' na maandalizi ya mitihani! Toka hapo mawasiliano yamekatika, hakuna simu wala meseji. Hivi naona ni viroja. Hivi waungwana ninyi mmesoma vyuoni wengi wenu! Katika hali ya kawaida mchumba wako au mpenzi wako akikupigia simu unaweza kubehave namna hiyo hata kama upo bize? Je, ni komedy gani hiyo ninayochezewa wanajukwaa?
Usiwe mzito wa kufikiri,kutokupokea simu nayo ni majibu.
 
Back
Top Bottom