Mahusiano ya Ajabu ya Mkwe na Baba mkwe: Iringa's TRUE STORY

Gagurito

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
5,600
803
Ukistaajabu ya Mussa...ya firauni! Ni uhusiano mbovu ulioleta jambo la ajabu kutokea bt ndio ukweli wenyewe huo na imetokea Iringa, mpaka niandikapo thread hii nipo iringa na hili ndio gumzo la mtaani.. Mume, mwalimu wa shule ya msingi moja ya hapa iringa mjini amezuiwa kuzika, mwili/maiti ya mkewe ikafukuliwa na ndugu za mkewe wakiongezwa baba mkwe wake na kusababisha marehemu kuzikwa usiku kwa kutumia taa za chemli, karabai, tochi na mishumaa kisa mwalimu (mume wa marehemu) hakumalizia kulipa mahali. Hali hii ikasababisha wananchi waombolezaji kuchangia pesa kumlipa baba mkwe ili mwili wa marehemu uzikwe, baba mkwe kapokea na akaonekana akinywa pombe kwa furaha na rafiki zake. Kwa maoni ya mume (mwalimu) anasema mahali alilipa yote toka miaka ya 90 na ameishi ya marehemu kwa takriban miaka 20 pasipo matatizo yoyote ukweni! WanaJF hii stori niyakweli na imetokea hv karibuni hapa iringa.. Sijui unalichukuliaje swala hili? TUNAOTAKA OA TUJIANDAE, KWA MWENDO HUU TEMBO CARD MASTER CARD MUHIMU. Hebutujadili..
 
aaaaaaaaaaaaaahhhh

hiyo hadithi ya walevi wa vijijini huko iringa......

tukianza kujadili kila vituko vya walevi hapa its a waste of time

hai relate na lifestyle yangu kwa kweli
 
aaaaaaaaaaaaaahhhhhiyo hadithi ya walevi wa vijijini huko iringa......tukianza kujadili kila vituko vya walevi hapa its a waste of timehai relate na lifestyle yangu kwa kweli
Mkuu hii story ni real. Nipo hapa iringa kikazi takribani siku ya 3 sasa, nimeyasikia, yametokea hapa mjini. NIMEIRUDIA KUIPOST HII THREAD ILI SISI VIJANA TUTEGEMEAO KUOA KARIBUNI TUJIFUNZE. Kuna mambo mengi hutokea tusiyoweza yajua, tuchukue tahadhari!
 
Wazee wengine sio wastaarabu kabisaaaaaa,kama alishachukuwa mahali long time ago mbona anamletea ukauzu mwalimu tena!
 
Wazee wengine sio wastaarabu kabisaaaaaa,kama alishachukuwa mahali long time ago mbona anamletea ukauzu mwalimu tena!
Ni jambo la kusikitisha pale pesa inapozidi ubinadamu! Tufunguke, Maisha ni Zaid ya Maisha, Mapambano dhidi ya maisha ni silaha dhalimu!
 
aaaaaaaaaaaaaahhhh

hiyo hadithi ya walevi wa vijijini huko iringa......

tukianza kujadili kila vituko vya walevi hapa its a waste of time

hai relate na lifestyle yangu kwa kweli

Mkuu madongo hayo...IRINGA KWETU....
 
kwa mlioko kwenye ndoa, je mmemaliza kulipa mahali ukweni? Uhusiano wako na baba mkwe na wanandugu wa mkeo ukoje?
 
Ukistaajabu ya Mussa...ya firauni! Ni uhusiano mbovu ulioleta jambo la ajabu kutokea bt ndio ukweli wenyewe huo na imetokea Iringa, mpaka niandikapo thread hii nipo iringa na hili ndio gumzo la mtaani.. Mume, mwalimu wa shule ya msingi moja ya hapa iringa mjini amezuiwa kuzika, mwili/maiti ya mkewe ikafukuliwa na ndugu za mkewe wakiongezwa baba mkwe wake na kusababisha marehemu kuzikwa usiku kwa kutumia taa za chemli, karabai, tochi na mishumaa kisa mwalimu (mume wa marehemu) hakumalizia kulipa mahali. Hali hii ikasababisha wananchi waombolezaji kuchangia pesa kumlipa baba mkwe ili mwili wa marehemu uzikwe, baba mkwe kapokea na akaonekana akinywa pombe kwa furaha na rafiki zake. Kwa maoni ya mume (mwalimu) anasema mahali alilipa yote toka miaka ya 90 na ameishi ya marehemu kwa takriban miaka 20 pasipo matatizo yoyote ukweni! WanaJF hii stori niyakweli na imetokea hv karibuni hapa iringa.. Sijui unalichukuliaje swala hili? TUNAOTAKA OA TUJIANDAE, KWA MWENDO HUU TEMBO CARD MASTER CARD MUHIMU. Hebutujadili..

Unajua siku hizi ulanzi umepanda bei nao alikuwa anataka pesa ya ulanzi huyo
 
Katika mambo ya mila hii inawezekana, mi nimewahi kuishuhudia Kigoma zaidi ya mara moja; kama mama amefariki na baba hajamalizia mahali hakuna kuzika hapo mpaka mahali yote iishe (ni kama adhabu vile), lakini vile vile hii inachangiwa/inasukumwa na wahusika kutoenda shule na kutanguliza umaskini wao.

Kuhusu kumaliza/kutomaliza deni chochote kinawezekana kwa sababu ikishatokea umeoa bila kumaliza mahali kwa baadhi ya mila hili linabaki kuwa deni, bahati mbaya unaweza usidaiwe na ukaishi na huyo mtu kwa miaka mingi kama hiyo jamaa anayosema ni 20, mpaka hayo matatizo yanapotokea ndio unakumbushwa.

Mpe pole jamaa, lakini mambo haya ya mila yako tight sana maeneo ambayo wakazi wengi au wahusika wana level ndogo ya elimu na ni maskini kiasi cha kushindwa kuthamanisha utu na pesa.
 
Katika mambo ya mila hii inawezekana, mi nimewahi kuishuhudia Kigoma zaidi ya mara moja; kama mama amefariki na baba hajamalizia mahali hakuna kuzika hapo mpaka mahali yote iishe (ni kama adhabu vile), lakini vile vile hii inachangiwa/inasukumwa na wahusika kutoenda shule na kutanguliza umaskini wao.Kuhusu kumaliza/kutomaliza deni chochote kinawezekana kwa sababu ikishatokea umeoa bila kumaliza mahali kwa baadhi ya mila hili linabaki kuwa deni, bahati mbaya unaweza usidaiwe na ukaishi na huyo mtu kwa miaka mingi kama hiyo jamaa anayosema ni 20, mpaka hayo matatizo yanapotokea ndio unakumbushwa.Mpe pole jamaa, lakini mambo haya ya mila yako tight sana maeneo ambayo wakazi wengi au wahusika wana level ndogo ya elimu na ni maskini kiasi cha kushindwa kuthamanisha utu na pesa.
Mkuu kama hujawahi kumbana nayo unaweza ukadhani ni stori eeh? Kuna haja ya kurekebisha mila zetu ziendane na wkt tuliopo. Mambo mengine ni kudhalilishana. Sijui wabena wanatabia/mila gani!
 
Back
Top Bottom