Mahusiano ni jambo pana sana katika dunia hii
watu wengi wamejikuta wanaendele mbele kwenye mahusiano feki wakaishia kuumizwa na wengine hadi wamedhubutu kujiua kwasababu ya gmahusiano .
Leo nataka tuangalie kwa ufupi chimbuko sahihi la mahusiano mpaka watu waingie kwenye ndoa .Vijana wengi wamejikuta wanaumia au kuumizwa katika mahusiano kwasababu ya kukurupuka kwa kufuata tamaa za mwili kulikpo kuangalia kanuni za kiroho zitakazowaongoza kupata watu sahihi kwenye maisha yao.
Ili ndoa yako iwe imara na iweze kudumu lazima ivuke hatua mbili za awali ambazo zitakufanya umjue mwenzako madhaifu yake na kuweza kukabiliana nayo kabla hujafanya maamuzi ya kukubali kumuoa au kuolewa naye.
Vijana wengi wanajikuta wanakosea sana kwa kukimbilia tamaa za mwili kuliko kuangalia nini alichokibeba anayetaka kuanzisha naye safari ya maisha ya ndoa.
Kijana hakikisha huivuki hatua ya urafiki ili ndoa yako ije kuwa bora zaidi , katika urafiki utatafuta kumfaham tabia zake kabla hujasema huyu anakufaa kuwa mchumba .
usikimbilie uchumba kabla hujamjua tabia zake na mwenendo wake utaacha wengi sana ukiwa unakimbilia uchumba.
Nawatakia wasaa mwema wana JF wote.
Amani ya bwana iwe nanyi.
Ni mimi mtumishi wa mungu
Avatar mok