Mahusiano ni gharama ya kujitoa sadaka

Mahusiano ni gharama ya kujitoa sadaka

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
37,156
Reaction score
55,653
Mahusiano yana gharama sana, kama hauko tayari kubeba hizo gharama ni bora usiingie kwenye mahusiano. Na hizi gharama zinajitokeza pale mmeshakuwa wawili ama mmeshazoeana vya kutosha. Na hizi gharama ni kama hizi:-
  • Kumchoka mwenzako na kutaka kumuacha...kama hujakomaa ni rahisi kumuacha,
  • Gharama za magonjwa utatakiwa uzibebe wewe...kama hujakomaa utamuacha,
  • Gharama za uchakavu wa mwili utatakiwa uzibebe wewe...kama hujakomaa utamuacha,
  • Gharama za kifo kama atafariki utatakiwa uzibebe wewe...kama hujakomaa utamuacha,
  • Gharama za kujifungua mlemavu utatakiwa uzibebe wewe...kama hujakomaa utamuacha,
  • Gharama za changamoto za kimaisha utatakiwa uzibebe wewe....kama hujakomaa utamuacha,
  • Gharama za kuridhishana kwenye penzi utatakiwa uzibebe wewe....kama hujakomaa utamuacha
  • Gharama za kuzeeka utatakiwa uzibebe wewe...kama hujakomaa utamuacha n.k
Kama hauko tayari kubeba hizo gharama, bora usiingie kwenye mahusiano.
 
Leo umeandika kakitu.

Ndio maana mnakula kiapo cha kwenye shida na raha.
 
Back
Top Bottom