Kwanza nianze kwa kuwatakia Mwaka mpya 2011 uwe wa fanaka na mafanikio. Kwangu Mwaka uliyopita ulikuwa na changamoto nyingi sana ila nashukuru Mungu kwa yote.
Leo nitapenda zungumzia silaha zitumikazo kwenye kuangamiza mahusiano katika ndoa. Urafiki wa kimapenzi hudumu zaidi na kuwa na faraja pale tendo zima takatifu la ndoa linapofanyika kwa maridhiano ya wote. Huleta matatizo iwapo mwanamke anatumia sex kama silaha, siku akichukia basi mnapeana migongo ama mzungu wa nne. Mara nyingi wadada wanaotumia njia hii husababisha wenzi wao kutafuta wagombea wenza. Tendo la ndoa ni muhimu katika kuboresha mahusiano tafiti nyingi zimeonyesha hilo, sitaki kurudia umuhimu wa sex kwenye maisha ya kila siku. Wanawake wanaotumia Ngono kama silaha mara nyingi hawadumu kwenye ndoa zao maana hujifananisha wao na kama chombo cha burudani ambayo anaweza mpatia mteja mwingine.
Ulevi kupindukia, pamoja na kuwa na madhara kiafya pombe husababisha kuyumba kwenye suala zima la ndoa. Wanaume walevi wengi wao wamekuwa hawana uwezo wa kukidhi haja za kingono kwa wenzi wao. Wanawake waliolewa na wanaume walevi wanaongoza kwenye suala zima la cheating, tafiti zinaonyesha hivyo.
Kudumisha ndoa cha muhimu ni kusikilizana na kupeana kile roho na matamanio ya mwili yanachohitaji. Sababu za kichwa kinauma, leo sijisikii ama baba anarudi amelewa kila siku na kuishia lala sebuleni ni hatari sana kwenye ndoa.
The Most Rev Masanilo ni mtafiti aliyebobea katika masuala ya Mahusiano, mapenzi na urafiki
"Nina mwezi wa 3 sasa sijamruhusu kunigusa"...!
Ni jana tulikuwa na mkasa wa aina hii ukiwa umeletwa na mdada ambaye ni family friend wetu, kisa amepata habari kuwa bwanake ambaye anafanya kazi na kontrakta wa barabara ya Arusha-Namanga, ana mahusiano na mwanadada mwingine...
Kwa ufupi ni wazi silaha hiyo ya kunyimana tendo takatifu la ndoa ni ya hatari sana...maana party inayolalamika lazima itatafuta namna fulani ya kumkomoa mwenzie kwa kuwa na mahusiano ya tofauti nje ya ndoa, halafu meli yote inakuwa inazama taratibu...
Maongezi ni ufunguo...familia zipate wakati muafaka wa KUSEMEZANA...kwa mazuri na mabaya, hapo mndipo miarobaini ya shida zote itatolewa.
Zote ni silaha....kukomoana!Silaha ninazozungumzia hapa ni kumnyima mwenzio tunda kama kumkomoa hivi!
Swali, kama mwanaume ameoana na mwanamke Rasmi yaani kwa Ndoa au harusi. Kwa bahati wakazaa watoto angalau 2. je Wakija kuachana tatizo linakuwa ni kukosa uvumilivu, au shetani ameingilia ndoa.
Mkuu inategemea na sababu! Kama ni uzinzi basi ndoa hiyo is beyond repairable hakuna kusingizia shetani
Heri ya Mwaka mpya Rev Masa,
Hili suala ni gumu sana mkuu. Ingawa sex inatakiwa kuwa immotional deal, mara nyingi watu wamelifanya kuwa physical zaidi na kupoteza maana yake ya msingi.
Kuna dada mmoja nilisikia habari zake kuwa yeye anaamini sex ni sawa na kumgusa mtu mkono na alikuwa tayari kutoa kwa mtu yeyote... A very complex business ingawa hatuwezi kukwepa kununua shea katika hizo kampuni!
kutumia sex kama silaha ni makosa sana,,hata kama kuna makwazo ni muhimu kuongea na kutatua tatizo,,,lkn mchungaji kuna wanandoa wametengana chumba kabisa kutokana na chronic cheating,,hii unaizungumziaje?
Duuuh hii iko complicated sana! Sasa huyo dada akikutana na vijana wa sasa mikono si itaota sugu kwa kusalimiana mara kwa mara? Kazi kweli kweli
Kutengana vyumba nadhani si suluhisho! Ningependa wakae chini wamalize tatizo. Kuna Dr mmoja mkoa wa Shinyanga alikufa akiwa chumbani kwake bila mkewe kujua kwa siku mbili, sababu za kutengana.