Mahusiano: Kuna mwenza bora kuliko mwenzie?

BOB LUSE

JF-Expert Member
Jan 25, 2014
3,738
3,198
Wadau salam,

Kuna tabia zipo katika baadhi ya mahusiano ambazo nimekuwa sipati majibu ya kuridhisha, utakuta upo na msichana/msichana yupo na mvulana wamepanga kuoana (uchumba wa kawaida) sasa kama kawaida ya ubinadamu mmoja akifanya kosa dogo (sio kuchepuka) mmoja wapo anaweza toa vitisho kuwa ukiendelea na tabia kama hiyo nitakuacha.

Mfano msichana amenenepa/anazidi kuwa mnene mwanaume anatishia atamuacha, hii nihaki?

Swali langu, mtu ukiamua kuoa mnakuwa mmeridhiana au mmoja anamfanyia favour mwingine aibuke aibu ya kutoolewa/kuoa?

Pili ndoa ya namna hii inaweza kudumu ambayo mmoja anajiona bora kuliko mwenzie? Changia kama umewahi pewa angalizo la kuachwa kwasababu zisizo na mashiko.

Karibuni.
 
Kuna watu hawaridhiki

Ukinenepa unaambiwa umenenepa sana, ukikonda unaambiwa unashida gani umekonda mpk unatisha

Ukivaa suruali unaambiwa imekuchora umbo, ukivaa skirt unaambiwa uvalie matshirt makubwa
Saa zingine ukivaa nguo unaambiwa kila siku unavaa hiyo hiyo mpk wamekukremu

Acha mkuu
 
Love is supposed to be a give and take kind of a relationship for equal partners.sasa inapotokea mmoja anajiona bora! i hate that,kweendra zako kafie mbele kule.
 
Mahusiano lazima yawe na kuchukuliana mizigo as kila mtu ana mapungufu yake. Ila me naona kama mtu anaona nina upungufu fulani afu hawezi kuvumilia, basi aniache tu no matter how namvumilia ya kwake. Asijilazimishe kuwa kwenye mahusiano yasiyompa furaha.
1. Kuna weakness ambazo zinaweza zikabadilika/kuisha kabisa
2. Kuna weakness ambazo zitapungua kidogo (Eg mtu alikuwa mlevi ila now anakunywa responsibly
3. Kuna weakness ambazo haziwezi kubadilika kamwe. So it's either uubebe huo mzigo kwa kuwa mvumilivu au usepe tu mapema.
Tatizo linakuja hapa, Kila mtu anaona weakness ya mwenzake ndo mbaya zaidi kuliko ya kwake. Me hata mtu awe ananivumilia kwa mapungufu yangu 100, afu yeye akawa na weakness moja tu "maneno makali", khaaa ntamuacha tu aende kwa kweli nisije kufa kwa presha. Nipo sensitive na maneno mnooooo, maneno makali yananiumizaga Mmh. Ndoa ni kuridhiana na kuweza kubebeana mizigo yenu (sio mizigo yoyote inabebeka lakini).
 
Basi ningekuwa mwanaume wewe ningekukosa hivihivi
 
Hahahah nashukuru hujawa mwanaume. Ilikuwa ukinijibu vibaya basi ntakujibu jibu moja zuri sana na utalikumbuka mwaka mzima. Tatizo sasa nikishakaa baadaye, roho inaanza kuniuma "kwa nini fulani nilimjibu vile, nimemuumiza", yani inaniumiza mimi mwenyewe tena zaidi. So nikajikuta najifunza tu kukaa kimya, ukinikwaza/ kunijibu vibaya nakuangalia tu usoni bila kukujibu naondoka. Ntarudi baadaye hasira zikishaisha afu najikuta uzito wa ile issue umeshapungua so napotezea tu kama vipi. Tatizo ipo siku utanipa maneno yako makali afu ukute na mimi nimeamka vizuri, Aaah ntakufurahisha afu lazima pozi na mimi litapungua tu ndo ntakuwa nishaharibu teh
 
Imenitokea asubuhi tu hapa wakati naongea naye kwenye simu(huyu mwanamke jana usiku saa 4 nilimpigia nikakuta simu ipo bize kama nusu saa nzima so nikamaind flani,nikamtumia usiku mwema then nikalala) so hii asubuh anasema eti nikiendelea na hii tabia yangu ya kumaind ataniacha! Nikajiuliza hivi huyu ananifanyia favour kunipenda ama vipi? Sikumjibu vibaya nimemuweka kiporo kwanza
 
Hahahaa yani mi mtu akiniboa huwa nashindwa kuremba aisee..... Kama sitampa kubwa basi ntapotezea tu namsamehe ila haiwezi kutokea mtu amenitibua af nimwambie kwa kumbembeleza
 
Mmh me najitahidigi kupotezea, ila siku yakinishinda hata hutoamini kama ni mimi. Afu kuongea kwa mdomo siwezagi so nakuandikia hilo gazeti utasoma mwaka mpya hadi mwaka mpya mwingine. Afu kuna wale wanafanyaga makusudically kukukwaza, hawa nawavutiaga kasi then nawapa moja tu afu akinuna akicheka ni juu yake na hapa roho hainiumi kabisa,
 
Imenitokea asubuhi tu hapa wakati naongea naye kwenye simu(huyu mwanamke jana usiku saa 4 nilimpigia nikakuta simu ipo bize kama nusu saa nzima so nikamaind flani,nikamtumia usiku mwema then nikalala) so hii asubuh anasema eti nikiendelea na hii tabia yangu ya kumaind ataniacha! Nikajiuliza hivi huyu ananifanyia favour kunipenda ama vipi? Sikumjibu vibaya nimemuweka kiporo kwanza
wapo wengi mkuu! wanajifanya wana run the show! siwapendi! lazima nimwache kwenye mataa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom