Mahujaji 35 wafariki Makkah

Mahujaji 35 wafariki Makkah

Interest

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2015
Posts
3,434
Reaction score
7,091
Wizara ya Afya ya nchini Misri imeeleza kuwa Mahujjaj 35 wa nchi hiyo wamefariki dunia wakati wa siku ya kwanza ya Hijja iliyomalizika nchini Saudi Arabia kutokana na uchovu na umri mkubwa.

4cf7d6b2589a4948a0189dbc91cef2cd.jpg
0ae061512dc3dfe8577f047855ba5364.jpg

Afisa mmoja wa Wizara hiyo, Ahmed el Ansary, amesema umri wa Mahujjaji waliofariki ni kati ya miaka 60 hadi 85.

Katika Ibada ya Hijja ya mwaka huu zaidi ya Mahujaji milioni mbili walihudhuria wakiwemo milioni 1.8 kutoka nje ya nchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hivi kwa nini kila mwaka lazima watu wafe?
Hakuna mbinu za ziada kuzuia vifo?
ni bora kungekuwa na watu wachache kuliko kuwa na idadi kubwa ambayo inaweka uhakika wa uwezekano wa watu kufa.
Hakuna mbinu ya kuzuia kifo. Mbona sehemu nyingine zisizokuwa Hija watu wanakufa why?

Siku zimefika...! Mungu awalaze mahala pema panapo lazwa wema, ameen.
 
hivi kwa nini kila mwaka lazima watu wafe?
Hakuna mbinu za ziada kuzuia vifo?

ni bora kungekuwa na watu wachache kuliko kuwa na idadi kubwa ambayo inaweka uhakika wa uwezekano wa watu kufa.
like seriously
 
Hakuna mbinu ya kuzuia kifo. Mbona sehemu watu wanakufa why?

Siku zimefika...!
ndio maana watu wanasoma Risk and Disaster Management.
kuwa na system ambayo Lazima kila mwaka mtu afe bila kuja na suluhisho la kudumu ktk dunia hii ya kisasa lazima kuwe na shida mahala.
Hayo ni mambo ya kiimani, lkn ingekuwa burudani kama Soccer tayari wadau wangekwishakuja na suluhisho la Kudumu.
 
Hilo ni jambo la Kheir kwasababu wamefia katika mji mtakatifu wakihiji.

Hakika pepo wataiona hao Waumi'ni na tunuku zile watazipata, Inshaallah

Wabillah Tawfiq,
Imani haibishiwi, lkn ingekuwa jambo la kiserikali au la kijamii tu, au la kitaaluma tungehoji zaidi mkuu.
 
Waongeze muda wa kuhiji, iwe mara nne kwa mwaka.
 
hivi kwa nini kila mwaka lazima watu wafe?
Hakuna mbinu za ziada kuzuia vifo?
ni bora kungekuwa na watu wachache kuliko kuwa na idadi kubwa ambayo inaweka uhakika wa uwezekano wa watu kufa.
Kwani ibada ni kwa ajili ya MUNGU au WATU?kila NAFSI ITAONJA UMATI NA KILA MAUTI YANA SABABU ZAKE....mbona kila siku watu WANAKUFA KWA AJALI ya NDEGE au BUS lakini WATU WANAPANDA? na wengine wanakufa USINGIZINI kwahyo TUOGOPE KULALA?sababu utakufa?huwezi kumkataza MTU kufanya IBADA YA HIJJA kwa UMRI wake au HALI YAKE...kwani HIJJA NI NGUZO MOJA WAPO YA UISLAM...na wala huwezi kupanga ratiba za hijja sababu SIKU HAZIGANDI...ikipita HADI MWAKANI....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hilo ni jambo la Kheir kwasababu wamefia katika mji mtakatifu wakihiji.

Hakika pepo wataiona hao Waumi'ni na tunuku zile watazipata, Inshaallah

Wabillah Tawfiq,

Asalaaaaale!!!!
We Azarel ulikuaga unaponda Uislamu na kusema sio Dini ya haki!!!
Umesilimu nini!!!
 
Kwani ibada ni kwa ajili ya MUNGU au WATU?kila NAFSI ITAONJA UMATI NA KILA MAUTI YANA SABABU ZAKE....mbona kila siku watu WANAKUFA KWA AJALI ya NDEGE au BUS lakini WATU WANAPANDA? na wengine wanakufa USINGIZINI kwahyo TUOGOPE KULALA?sababu utakufa?huwezi kumkataza MTU kufanya IBADA YA HIJJA kwa UMRI wake au HALI YAKE...kwani HIJJA NI NGUZO MOJA WAPO YA UISLAM...na wala huwezi kupanga ratiba za hijja sababu SIKU HAZIGANDI...ikipita HADI MWAKANI....

Sent using Jamii Forums mobile app
sikatai mkuu, ndio maana nasema kama kwa ground za kiimani, hata wakifa wote ni sawa.
Lkn kijamii, kila mwaka kufa watu wengi eneo lile lile, kwa sababu ileile na mazingira yaleyale lzm watu wazame waje na suluhisho.

Hata wasimamizi wenyewe wa huo mkutano ukirefer vifo vya mwaka 1990 na 2015 hawasemi ni thawabu, badala yake wakaja na njia za kuzuia vifo kama.
Crowd Management
Surveillance cameras ziliongezwa
electronic controls za njia na mageti
Watu kuvaa electronic robbon maalum ili kutambuliwa location zao.

Bado watu kufa huko sio sifa, na bado wanaweza kufanya vizuri zaidi ya hapo ili watu wakienda kwenye Mambo ya kiimani au kutimiza nguzo warudi salama majumbani kwao.
 
Kwahyo wewe bado huamini km KIFO ni AHADI?kuna KIFO CHA AJALI na mazingira ya kawaida...hao hawafi kwa ajali bali UMRI WAO unachangia.....idada ya HIJJA sio SWALA TU....kuna mambo mengi yanafanyika...ikiwemo kuzuru MAENEO MATAKATIFU ya MITUME..kuzunguka LKHABA...wazee hufa sababu ya UMRI wao.....labda UKATAZE WAZEE KUHIJI....rejea kwenye thread inasema wanaokufa ni kati ya 65 na 80 umeona kuna mtu wa 35 au 40 katajwa hapo?

wazee wanaweza kupewa kipaumbele. Mbona hata mahospitalini,benk na sehemu za kawaida wazee,wajawazito na walemavu wanapewa fursa.

yote kwa yote kwa sababu ya mambo ya kiimani hayabishiwi, yote unayosema ni sawa tu sikubishii mkubwa
 
ndio maana watu wanasoma Risk and Disaster Management.
kuwa na system ambayo Lazima kila mwaka mtu afe bila kuja na suluhisho la kudumu ktk dunia hii ya kisasa lazima kuwe na shida mahala.
Hayo ni mambo ya kiimani, lkn ingekuwa burudani kama Soccer tayari wadau wangekwishakuja na suluhisho la Kudumu.
Kufia mji mtakatifu wakati wa kuhiji ni thwawabu. Wengine wanaenda kwa ajili ya kujiulia huko
 
Back
Top Bottom