Hii hali hata mimi nimeiona na ni aibu sana, baadhi ya wabunge wamekuwa watoro. Hivi huwa hakuna daftari maalumu la kusaini mahudhurio na litumike kwa kuhalalisha payments?
Pia tatizo lingine ni kwamba huu utaratibu wa wabunge wakati kikao kinaendelea unasikia spika anasema wajumbe fulani mnatakiwa mkakutane ukimbi wa Pius Msekwa, na mtoke taratibu! Sasa najiuliza kwa nini hiyo isifanyike baada ya kikao kikuu cha bunge? Je kwa namna hii si wanawafanya wabunge wengine wakose mijadala muhimu?