Mahudhurio bunge la jamhuri yanakatisha tamaa

Jacobus

JF-Expert Member
Mar 29, 2011
4,007
2,000
Si ubishi kuwa viti katika ukumbi wa bunge la jamhuri vimeongezwa takriban nusu ya idadi ya wabunge wa halisi wa jamhuri. Kilichonifanya nihuzunike zaidi ni leo katika kikao cha alasiri, kamera za StarTV zimeuzunguka ukumbi na kwa kweli viti vingi mno hakuna waheshimiwa hawa. Sasa aidha wanatumia wingi wa viti kukwepa kuhudhuria vikao vya bunge kuhalalisha utoro kitu ambacho si sahihi.
 
Manjagata

JF-Expert Member
Mar 7, 2012
6,342
2,000
Ni kweli hasa..je wanapokuwa hawamo mjengoni.je posho inahesabika?

Posho inalika kama kawa Mkuu! Nilisikia wengine huwa wanakuja kusaini asubuhi na kukimbilia kwenye semina zingine na hivyo kuvuta posho 2 kwa wakati!
 
commonmwananchi

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
3,115
2,000
Si ubishi kuwa viti katika ukumbi wa bunge la jamhuri vimeongezwa takriban nusu ya idadi ya wabunge wa halisi wa jamhuri. Kilichonifanya nihuzunike zaidi ni leo katika kikao cha alasiri, kamera za StarTV zimeuzunguka ukumbi na kwa kweli viti vingi mno hakuna waheshimiwa hawa. Sasa aidha wanatumia wingi wa viti kukwepa kuhudhuria vikao vya bunge kuhalalisha utoro kitu ambacho si sahihi.

ukweli ni kwamba wengi wa watoro ni ccm,wao wanatumia muda mwingi kufanya vikao vya dharura ili kujihami na hoja kali zinazotolewa na wana UKAWA ndani ya bunge.
na si wabunge tu,bali jiulize hata maspika woote wawili huwa wanakuwa na udhuru gani kila jioni?:flypig:
 
IROKOS

JF-Expert Member
Aug 13, 2011
8,684
2,000
Hii hali hata mimi nimeiona na ni aibu sana, baadhi ya wabunge wamekuwa watoro. Hivi huwa hakuna daftari maalumu la kusaini mahudhurio na litumike kwa kuhalalisha payments?

Pia tatizo lingine ni kwamba huu utaratibu wa wabunge wakati kikao kinaendelea unasikia spika anasema wajumbe fulani mnatakiwa mkakutane ukimbi wa Pius Msekwa, na mtoke taratibu! Sasa najiuliza kwa nini hiyo isifanyike baada ya kikao kikuu cha bunge? Je kwa namna hii si wanawafanya wabunge wengine wakose mijadala muhimu?
 
Tungekuwa makini basi pangewekwa utaratibu wa kuhakiki mara mbili (mchana na jioni) mbunge aliyehudhuria session zote mbili ndio mwenye haki ya kupata posho. Lakini nani wa kumshika paka kengere? Nakumbuka spika Anne aliwakanya wabunge kutozungumza na waziri mkuu ndani ya ukumbi wa bunge wakati kikao kikiendelea ili waziri mkuu awe akifuatilia mijadala kwa umakini lakini hilo limeshindikana na spika hakumbushii!!!!!!!!!!!!!!!
 
Jacobus

JF-Expert Member
Mar 29, 2011
4,007
2,000
utoro sugu wa wabunge unaleta hata uvivu kuangalia bunge!
Haya mkuu, kambi ya upinzani wametoka ukumbini wakilaumu kuburuzwa katika hoja ya wizara ya nishati. Sijui Ole Sendeka kabaki? Maana aliapa kutoiunga mkono hoja HATA kwa RISASI.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom