Mahojiano ya T Mhando(AZAM TV) na Kamishna wa Tume ya Kuzuia Madawa ya Kulevya, Rogers Sianga

Azim Sokoine

JF-Expert Member
Aug 20, 2014
1,432
2,629
Kamishna wa kupambana na madawa ya kulevya Rogers Sianga, katika kipindi kinachorushwa na azam TV chini ya ndugu Tiddo Mhando amesema suala la madawa ya kulevya halipo kwa viongozi wa serikalini.

Binafsi kauli hii ya Kamishna huyu imenistua sana kwani haiwezekani kusema kiujumla tu kwamba eti viongozi wa serikali hawajihusishi na madawa ya kulevya.

Nini kimejificha nyuma ya pazia juu ya kauli hii? Kwa hiyo kumbe wanaohusika na madawa ya kulevya ni wanasiasa wa upinzani, wasanii na wafanyabiashara tu! Kwa staili hii vita ya kupambana na madawa ya kulevya haitokuja kufanikiwa.

Kamishna Rodgers anasema hakuna connection yoyote ya viongozi wa serikali kujihusisha na madawa ya kulevya. Hebu tujiulize kama tu ndo ameteuliwa hajafanya kazi hata wiki tatu then anakuja anasema hajaona connection ya viongozi wa serikali kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya. Hii inaleta picha gani?

Kamishna wa kupambana na madawa ya kulevya Rogers Sianga,katika kipind kinachorushwa na azam tv chini ya ndug Tiddo Mhando..amesema suala la madawa ya kulevya halipo kwa viongoz wa serikalini,binafsi kauli hii ya kamishna huyu imenistua sana kwani haiwezekani kusema kiujumla tu kwamba eti viongoz wa serikal hawajihusishi na madawa ya kulevya..nini kimejificha nyuma ya pazia juu ya kauli hii,kwa hiyo kumbe wanaohusika na madawa ya kulevya ni wanasiasa wa upinzani,wasanii na wafanyabiashara tu,kwa stail hii vita ya kupambana na madawa ya kulevya haitokujakufanikiw
Kama kweli katoa matamshi haya it's ridiculous.Anajuaje?Kawapima?No research no right to speak. Frankly hatufai if it is true,na ana ajenda ya siri.Je vita ya madawa itafanikiwa under his leadership?The answer is most probably a flat no.
 
Nilisoma pahali kuwa wakina Masogenge walikuwa na diplomatic passport na zile bag 3 za 50kg each pale airport zilipita kama diplomatic bags!

Aljazeerah now wakaja kuripoti kuwa msafara wa raisi wa china ulisaidiana na watawala husika kubeba vipusa vya 'kona bara' kwenye diplomatic bags na kusepa navyo china bila kikwazo!

Halafu wanafiki wakasema kuwa Chief Mangungo wa Wadanganyika alipaa hadi kwa kina Bruce Lee kumkomboa prince wake baada ya kukutwa na sembe !!

Kama haitoshi awamu zilizopita mkulu aliiomba serikali ya kina Don Yen isiwanyonge wabongo wanaoshikwa na unga huko Macau na Hu Ha City huku pia Waziri mwenye Luku yenye VI alitumwa south kwenda kufuatilia hali ya Masogange aliponyakwa anarangua unga huko bondeni ili atendewe vzuri!!

Me naipongeza serikali kwa kuja na matokeo ya mkemia mkuu kuwa wakina fulani hawahusiki kabisa!!
 
Matendo na kauli za viongozi wetu wengi wa serikali yanaonesha wazi kwamba wanayo matatizo makubwa ambayo ni vigumu kuyatofautisha na matatizo yanayowapata waathirika wa madawa ya kulevya. Kiongozi mwenye akili timamu na ambaye hajaathirika kwa namna yoyote hawezi kukurupuka tu na kuanza kuropoka maneno ya ajabu ajabu kama tunavyoshuhudia kila kukicha.

Hapana Sianga, hapa umekosea...labda utuambie chanzo cha matatizo yanayowakumba viongozi wetu hadi wakose kabisa hekima na busara katika maamuzi ni kipi. Usikivu, uvumilivu na takafuri katika uongozi ni sifa ambazo muathirika hategemewi kuwa nazo kwani hubaki kutazama kila tukio kwa macho yaliyotanda ukungu. Kiongozi kama huyo kujipa uwezo wa kimungu ni kitu kisichoshtua.

Tatizo tulilo nalo kama Watanzania ni kuanza kuyakubali bila kuyashtukia hayo matendo au hizo kauli na hii ni dalili mbaya sana kwa ustawi wa jamii yenye kujali utawala wa sheria. Ukisoma michango ya mashabiki wa viongozi wa aina hiyo humu JF, utabaki unashangaa kama taifa hili bado lina watu wenye hulka ya kibinadamu. Taswira ya jumla unayopata ni Tanzania kuwa ni dampo la walevi; hasa viongozi...
 
Kamishna wa kupambana na madawa ya kulevya Rogers Sianga,katika kipind kinachorushwa na azam tv chini ya ndug Tiddo Mhando..amesema suala la madawa ya kulevya halipo kwa viongoz wa serikalini,binafsi kauli hii ya kamishna huyu imenistua sana kwani haiwezekani kusema kiujumla tu kwamba eti viongoz wa serikal hawajihusishi na madawa ya kulevya..nini kimejificha nyuma ya pazia juu ya kauli hii,kwa hiyo kumbe wanaohusika na madawa ya kulevya ni wanasiasa wa upinzani,wasanii na wafanyabiashara tu,kwa stail hii vita ya kupambana na madawa ya kulevya haitokujakufanikiw
Hahaha habari hiyo kweli?
 
Aliposema.hayo maana yake ni pamoja na wabunge.
 
Kama Sianga kasema hayo, tena kwa mdomo wake, basi ameshindwa kabla hajaanza na vita dhidi ya madawa ya kulevya ndo imekoma.

Awezaje kuyasema hayo wakati hata mwezi kazini hajamaliza? Yaani tayari ameshawachunguza wote na kuthibitisha kuwa hakuna hata mmoja anayetumia au kushiriki kwa namna fulani kwenye biashara hiyo haramu?

Mmm, mimi siamini kama kasema hivo. Weka kaclip tafadhali!
 
mkuu ni kweli kasema hajalishwa maneno
 
Jamani mambo mengine tusiwe tunapotosha.

Wengi tumemsikia Rogers Sianga akihojiwa na Tido Mhando ktk kipindi cha Funguka,amejieleza vizuri sana,akajibu maswali kwa uzuri sana.

Moja ya swali aliloulizwa,ni je kweli viongozi wa siasa wanajihusisha na madawa ya kulevya?
Akajibu akasema,hawezi kusema ndio wala hapana,kwa sababu ndio kwanza anaingia ofisini.Wampe mda kwanza ili afanye kazi na majibu yatapatikana kama wapo au la!

Akasisitiza kuwa,operation inayoongolea watakamata watu,ukiona mtu amekamatwa anakwambia mimi nilitumwa na fulani(ambaye ni mwanasiasa) au ndugu yangu ni fulani,au unakamata mtu halafu unaanza kupigiwa simu na kiongozi kuwa huyo "kijana wangu" naomba umuachie,hapo ndio utakuwa na nafasi ya kusema,viongozi na wanasiasa wamo ktk mtandao huu.

Kamishna Sianga akasisitiza kuwa,madam ndio wamepewa ofisi,basi wapewe mda.Akasema lakini watu wajue,zile "cartles" unazozisikia Brazil na Mexico,basi na hapa zipo.

Hayo maneno wewe mkuu Azim Sokoine umeyatoa wapi? Kwanini usisikilize vizuri na kuleta ukweli wa mambo?Kwa hili....Umemsingizia Rogers Sianga!!Sio vizuri
 
Kama Sianga kasema hayo, tena kwa mdomo wake, basi ameshindwa kabla hajaanza na vita dhidi ya madawa ya kulevya ndo imekoma.

Awezaje kuyasema hayo wakati hata mwezi kazini hajamaliza? Yaani tayari ameshawachunguza wote na kuthibitisha kuwa hakuna hata mmoja anayetumia au kushiriki kwa namna fulani kwenye biashara hiyo haramu?

Mmm, mimi siamini kama kasema hivo. Weka kaclip tafadhali!
Mkuu nisome hapo juu
 
Back
Top Bottom