Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 299,611
- 752,036
Kwanza kabisa kwa dhati ya moyo wangu nipende kuchukua nafasi hii kuwapa pole kubwa kwa yule yaliyowapa clouds media....inauma na kuumiza na kusonenesha moyo POLENI SANA.
Katikati ya pole hii na maumivu haya pia msisahau kujitafakari upya, kwakuwa nyie leo ndio mmeonja machungu haya lakini Kiuhalisia kwa kuwa na ukaribu wa kutia mashaka sana na nyumba kubwa tangu enzi za JK mpaka sasa kuna wenzenu kwenye Tasnia ya habari wameumizwa na matendo yenu hayo hasa kubebwa na mamlaka za juu.
Rc mwenye utata wa majina mmesaidia sana kumtengeneza mpaka kufika alipofikia... Mlikiuka kanuni nyingi, mkafunika madhaifu na mabaya yake mengi mkatangaza yake yaliyo mazuri tu, ukaribu wenu huo ukazidi hata urafiki wa kawaida, kituo chenu cha habari kikawa kama sehemu ya kupata taarifa za RC kwenye utendaji wake wa kila siku TBC ikasahulika kabisa.
Mlijisahau kwakweli mkalewa sifa na mkafaidika mno na rc huyu kwa njia anuwai hasa kujitangaza.
Malalamiko juu yenu kwenye mitandao ya kijamii yakageuka eti ni wivu husuda na kijicho.... Post nyingi zimo humu.... Mnabeba asilimia kubwa kwenye kumuumba huyu kiumbe.... Msilalamike.
Falsafa ya panya ni kuuma na kupuliza, Mahojiano ya leo ya Ruge na wafanyakazi wake yaliegemea zaidi kwenye ku compromise kutaka heshima kutaka mipaka nk! Heshima ipi tena wakati mmeshadhalilishwa kwa kiwango cha juu hivyo?
Kuna baadhi ndani ya clouds wanataka sheria ichukue mkondo wake lakini kwa hali ilivyo na uhusiano wa karibu mno kati ya Ruge na Rc ni vigumu mno kusimama mbele na kumshtaki mkosaji... Wamefanya mengi pamoja ya siri na ya wazi... Ngoma ipo kwenye hayo ya siri.
Kesi iko wazi kabisa lakini mpaka sasa Ruge anarudiarudia kusema kuwa alitegemea(na pengine anategemea) Rc aende kuomba radhi yaishe...kuna kitu kinafichwa hapo
Kuomba radhi ni uungwana ni hekima ni ujasiri lakini hakuondoi kosa LA jinsi lililofanywa kwenye taasisi...
Na kwa wadogo zangu kina Sudi Kumbukeni umbea hauna posho angalieni kona mlipo sasa watu wote macho kodo kwenu hamna raha hamna amani...
Tukio hili liwe fundisho kwenu.