Mahojiano ya jana baina ya EATV na mtalaam wa TRA

koryo

JF-Expert Member
Jun 21, 2010
639
278
Jana kuanzia saa moja na nusu usiku kulikuwa na mahojiano baina ya EATV na Mtalaam wa kodi kutoka TRA. Mada kuu ilikuwa kuhusu ongezeko la VAT kuwa iwahusu wateja au Mabenki. Niseme ukweli maelezo yaliyokuwa yanatolewa na mtalaamwa kodi HAYAKUKIDHI KABISA matakwa ya wasikilizaji.

Maelezo yake hayakueleweka kabisa na sauti yake ilikuwa haisikiki. Kwa ujumla hakuwa amejitayarisha na uelewa wake juu ya mada ulikuwa chini ya kiwango kabisa.

Namshauri Kamishna Mkuu wa TRA kuwa unapompeleka mtumishi kukuwakilisha kwenye vipindi kama cha jana basi uhakikishe unampeleka mtu ambaye ana uelewa mpana na masuala ya kodi na siyo kama yule wa jana.
 
Watalaam wa Bongo, wapo wa aina nne.
1: Watendaji kazi na ni waongeaji sana/ kujieleza.

2: Watendaji kazi na sio waongeaji.

3: Wasiotenda kazi lakin waongeaji wazuri.

4:Wasiotenda kazi na wasiojua kuongea/ kujieleza.

Kwahiyo yule wa jana atakuwa kundi la pili, kwahiyo alitakiwa aambatane na mtu muongeji kutoka ofisini kwake ..!!
 
Hapo sijakuelewa mleta maada
Tuwekee angalau hata sie ambao hatukumsikia tujue wapi alivurunda
 
Siwezi kuchangia Umbea labda utuweke clear kwanza. Au tupia video tuone
 
Back
Top Bottom