jMali
JF-Expert Member
- Nov 9, 2010
- 8,412
- 5,013
KATIKA siku za karibuni, jina la Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) kutoka Tanzania, Shy-Rose Bhanji, limetawala vyombo vya habari kwa sababu tofauti.
Raia Mwema limezungumza naye wiki hii jijini Dar es Salaam na ameeleza ya moyoni kuhusu maisha yake, siasa za EALA na tuhuma lukuki dhidi yake zilizotawala katika vyombo vya habari.
WAKATI tulipoanza mahojiano haya, Shy-Rose Sadrudin Bhanji, hakuwa na furaha. Kama umemfahamu kwa muda mrefu, ilikuwa wazi kwamba hakuwa katika hali yake ya kawaida.
Siku mbili kabla ya mahojiano yetu, nilizungumza naye kwa njia ya simu na alikuwa akilia. Taarifa mbalimbali zinazoenezwa kuhusu matukio yake zilikuwa sasa zimeanza kumuumiza.
Kwa maelezo yake mwenyewe, kiwango chake cha uvumilivu sasa kilikuwa kinaelekea kwenye ukomo. Ananieleza kwamba yeyé ni mwanadamu na anapokuwa anaelezwa kwa ubaya wake tu, tena kwa tuhuma za kupikwa, roho yake inaumia.
Siku hizi nikienda kwenye mikutano ya EALA, kama hakuna shughuli ya kufanya najifungia tu chumbani kwangu. Maana kila ninapoonekana linazushwa jambo ambalo halipo.
Nashukuru tu kwamba ndugu, jamaa na marafiki ambao wananifahamu wamekuwa wakinipa moyo sana. Hivi ninavyozungumza nawe nimefunga kwa siku ya tano leo nikiomba Mungu aniepushe na kipindi hiki, anasema Bhanji.
Hii ni mara yake ya kwanza kuwa mbunge. Na nyingi za taarifa zinazotoka kumhusu zinakuwa mbaya. Matokeo yake, amekuwa maarufu, si kwa mazuri, kuliko wabunge wote wa EALA kutoka Tanzania, ukiondoa Makongoro Nyerere.
Kabla ya yote, namuuliza anieleze kuna nini hasa kilitokea wakati wa safari ile ya hivi karibuni ya wabunge wa EALA kwenda jijini Brussels, Ubelgiji, ambako inadaiwa alifanya fujo akiwa ndani ya ndege.
Ni kweli mzozo ulitokea kwenye basi ambalo tulikuwa tunalitumia lakini hayo yalikuwa ni malumbano ya kawaida kabisa miongoni mwetu. Na malumbano kama hayo ni mwendelezo wa mizozo ambayo imekuwapo tangu baadhi ya wabunge waliposhindwa kumuondoa Spika wa EALA madarakani. Hakikuwa kitu kipya.
Mpaka tunamaliza ziara yetu hapakuwa na mbunge yeyote aliyetoa malalamiko au kinyongo chake kuhusu tuhuma zozote dhidi yangu juu ya tukio lolote.
Wabunge wamesubiri wiki mbili baadaye ndipo walipoibuka na kupeleka jambo hilo kwenye kikao cha Bunge, Kigali, Rwanda kilichomalizika mwishoni mwa Oktoba mwaka huu.
Siku mbili kabla ya kikao cha Bunge, tuhuma hizo zilisambazwa na mtu asiyejulikana kupitia njia ya WhatsApp kwenye simu za mikononi.
Hatua hii iliwapa nguvu na mwanya wa kutaka Bunge linijadili juu ya tuhuma dhidi yangu na kutaka nichukuliwe hatua za kuondolewa kwenye Kamati ya Uongozi ya Bunge na vilevile nisimamishwe na hatimaye nifukuzwe ubunge.
Tuhuma hizi ni njama za baadhi ya wabunge. Tuhuma hizi ni njama za kuniharibia sifa yangu ya utendaji kazi na vilevile kunipunguzia nguvu ya kutetea maslahi ya Tanzania.
Hawajawahi kupendezwa jinsi ninavyoonyesha mapenzi makubwa kwa nchi yangu na pale inapobidi nimesimama kidete kuisemea nchi yangu.
Isitoshe wabunge ambao wamekuwa mstari wa mbele kuendeleza kampeni ya kumtoa madarakani Spika nimekuwa nikiwasema waziwazi kwa vile walikuwa wana agenda ya mchezo mchafu na mara zote wamekuwa hawapendezewi na ukweli wangu.
Tujiulize, je, sakata hili lilistahili kusimamisha shughuli halali za Bunge zilizopangwa kwa kipindi cha wiki mbili? Kwa nini wabunge wenye malalamiko dhidi yangu hawajaandika barua za kulalamika kwa uongozi wa Bunge ili na mimi nipate nafasi ya kujibu malalamiko hayo na kujitetea, alihoji Shy-Rose.
Wakati akizungumzia suala hili ambalo lilizua mijadala mikali katika mitandao ya kijamii, mbunge huyu alikuwa mtulivu. Kama alikuwa na uchungu wowote na mahasimu wake, aliuficha ndani ya moyo wake.
Wakati akinywa glasi yake ya maji, namuuliza pia kuhusu tuhuma za kupigana na mbunge mwenzake wa EALA kutoka Tanzania, Nderakindo Kessy (NCCR-Mageuzi).
Sijampiga na wala sijawahi kupanga kumpiga Mbunge mwenzangu Mheshimiwa Kessy kama alivyodai au inavyodaiwa.
Ukweli ni kuwa tuligongana kwa bahati mbaya wakati tukipishana ndani ya ukumbi wa Bunge mara baada ya kikao cha Bunge kuahirishwa siku ya Jumanne, Novemba 18 jijini Nairobi, Kenya.
Isitoshe, sijapelekwa Polisi wala kuitwa na kituo chochote cha Polisi kule Nairobi kwa kuhojiwa au kushikiliwa na Polisi kutokana na tuhuma hizo zilizoripotiwa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari hapa nchini.
Inashangaza na kusikitisha baadhi ya vyombo vya habari kuripoti kwamba nilikuwa nimekamatwa na Polisi na kwamba nilikuwa chini ya Polisi kwa madai ya kumpiga Mbunge mwenzangu.
Kessy alikwenda kushitaki Polisi akisindikizwa na wabunge wa Rwanda, Uganda na Kenya kwamba nilimpiga.
Sasa tazama, huyu mbunge ni Mtanzania mwenzangu. Katika hali ya kawaida kimbilio la kwanza lingekuwa kwa Ofisi ya Spika, Naibu Waziri wa Afrika Mashariki, Dk. Abdallah Sadallah au Mwenyekiti wa Wabunge wa Tanzania (EALA), Adam Kimbisa ambao wote walikuwa bungeni. Hakufanya hivyo.
Badala yake, Kessy aliamua kwenda na mahasimu wangu ili waendelee kuwa na uhalali na agenda ya tuhuma dhidi yangu ambazo walizisambaza kwenye mitandao na vyombo vya habari. Kinachoniuma ni kwamba huyu ni Mtanzania mwenzangu. Kwa nini anafanya hivi? Anafaidi nini kwa jina la Tanzania kuchafuliwa?
Nilitaraji Nderakindo angejikita katika kusimamia maslahi ya Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla lakini badala yake bungeni hajawahi kutoa mchango wowote na mara zote hukaa kimya.
Ajenda kubwa na ya kwanza kutoka kwake imekuwa ni tuhuma dhidi yangu. Najua nilimkera nilipotoa taarifa Wizara ya Afrika Mashariki kwamba katika kikao cha Bunge kilichofanyika jijini Dar es Salaam na kususiwa na Wabunge wa Rwanda na Burundi na yeye aliungana nao kususia Bunge na takribani shughuli zote za kikazi zilizokuwa zimepangwa kwa ajili ya wabunge wa EALA.
Wanawake tunahitaji kupendana na kusaidiana na si kupigana vita kwani ni kwa kusaidiana tu ndipo tutaweza kupiga vita mfumo dume na wanawake wengi wataweza kuingia katika nafasi za uongozi, anasema.
Ni katika wakati huu ndipo anapokumbusha tena kuhusu tuhuma za yeye kulewa na kutukana Marais wa nchi za Kenya, Rwanda na Burundi. Mbunge huyo alisema hajawahi kumtukana kiongozi yeyote na ndiyo maana wale wanaoeneza taarifa mbaya kumhusu hawajawahi kuwa na ushahidi.
Haiingii akilini kwamba matukio mabaya kama haya (tena yanayofanana na ya kigaidi) yangefumbiwa macho na Shirika la Ndege la Kimataifa la KLM ambalo tulisafiria. Vile vile vyombo vingine vya usalama na vyombo vya sheria visingesita kuchukua hatua dhidi yangu iwapo ningehusika kwa namna yoyote ile ya kuhatarisha usalama wa safari yetu.
Na iwapo tukio lolote baya lingetokea basi lisingesubiri wiki mbili baadaye ndipo wabaya wangu walitangaze. Huu ni uwongo wa aina yake, anasema.
Kwa wafuatiliaji wa masuala ya EALA, mojawapo ya mambo yanayoibuka mara kwa mara ni suala la Spika wa Bunge hilo, Dk. Margaret Nantongo Zziwa, ambaye inadaiwa hatakiwi na wabunge kutoka katika nchi za Rwanda, Burundi, Kenya na baadhi wa Uganda.
Bhanji ni mmoja wa wabunge saba wa Tanzania ndani ya EALA ambao walipinga hoja ya kutaka kumwondoa Zziwa kwenye Uspika. Kimsingi, katika wabunge tisa wa Tanzania walio ndani ya Bunge hilo; ni wawili tu Abdallah Mwinyi na Kessy pekee, ndio ambao waliunga mkono hoja hiyo.
Namuuliza Bhanji kwamba imekuwaje wabunge wa Tanzania wanamtetea Mganda ambaye wenzake anaotoka nao katika nchi moja hawamtaki?
Kwanza kabisa siyo kweli kwamba Waganda wote hawamtaki. Ukweli ni kwamba wapo pia Waganda wanaomkubali. Sehemu kubwa ya wabunge wa EALA kutoka Tanzania tunamuunga mkono huyu Spika kwa sababu tuligundua kuna ajenda ya siri dhidi yake ndiyo maana tulipinga hatua hiyo.
Msimamo wetu ni sahihi kwa sababu ajenda ya kumng`oa Zziwa haina maslahi mapana ya mtangamano wa Afrika Mashariki na wala haina maslahi kwa Tanzania. Isitoshe huyu ni Spika wa Bunge la Afrika Mashariki si Spika wa nchi moja na kwa maana hiyo ni Spika anayewakilisha Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Vita ya kumng`oa ni ajenda ya siri ambayo ina harufu ya mchezo mchafu. Wanaotaka kumng`oa wana lengo la kuweka Spika mbadala atakayeafikiana na matashi na matakwa ya wanaotaka kumuweka madarakani.
Kwa lugha rahisi Spika atayewekwa madarakani atakuwa anatimiza matakwa ya waliomuweka. Lengo la kumuondoa Spika huyu ni kundi la wachache ili wapate mwanya wa kumuweka Spika atakayehujumu maslahi ya Tanzania.
Hakuna sababu zozote za msingi ambazo zinahalalisha kutaka kumuondoa huyu Spika kwenye nafasi yake. Alichaguliwa atumikie nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka mitano na tutahakikisha kwamba anamaliza kipindi chake ifikapo 2017, anasema.
Wakati tukizungumza kuhusu suala hili la Zziwa, nabaini Shy-Rose ameanza kurejea katika hali yake ya kawaida. Ameanza kutabasamu wakati akizungumza. Sura ninayoiona sasa ni ile ya mtangazaji wa Kituo cha Televisheni ya Taifa (TvT) niliyekuwa nikimtazama miaka ya nyuma. Namuuliza kwa nini aliacha kazi nzuri na iliyomjengea jina kama uandishi na kuingia katika siasa ambazo sasa zinamnyima raha.
Wakati nikiwa Daily News na TvT taaluma yangu ya uandishi wa habari ilinipa fursa na nafasi ya kuzunguka na viongozi mbalimbali na nilijionea jinsi wanavyofanya kazi yao kwa ufanisi na hiyo ilinipa hamasa ya kutaka siku moja nivae viatu vyao.
Vile vile niliingiwa na hamasa pale nilipokuwa nikiripoti habari za Bunge huko Dodoma nikatamani kwamba siku moja na mimi niwepo ndani ya Bunge ili niweze kutoa mchango wangu kwa namna moja au nyingine.
Nilishafikia kilele cha utendaji wangu wa kazi. Pale NMB niliitwa mahususi ili kuitangaza benki ijulikane na wananchi na kazi hiyo niliifanya kwa mapenzi na hamasa kubwa. Katika kipindi cha miaka sita ya kuwa pale niliifanikisha kwa asilimia 99 kazi niliyopewa. Hivyo nilitamani kuondoka kwenye Corporate World na kuingia kwenye siasa ili kuwa na uwanja mpana wa kuihudumia jamii, anasema.
Hadithi ya maisha ya Shy-Rose si hadithi rahisi. Huyu ni mwanamke ambaye alipoteza wazazi wake angali mdogo na ameishi sehemu kubwa ya maisha yake kama mtoto yatima.
Katika mazungumzo yake na Raia Mwema, Bhanji anaeleza namna ya kujituma, kutokata tamaa, weledi na uhusiano mwema na watu ulivyomfikisha, hatimaye, katika nafasi aliyonayo sasa.
Natamani sana stori ya maisha yangu iwe kichocheo kwa watoto wengine walio katika maisha magumu kutokata tamaa na kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu. Watu wengi wakiniona wanaona kama nimefika hapa kwa kubebwa tu, lakini hawajui. Ndiyo maana naumia sana watu wanaponisingizia habari ambazo lengo lake ni kuniangusha, anasema.
Kwenye suala la kutokata tamaa, Shy-Rose ni mmoja wa wanasiasa wa mfano kwa hapa nchini. Kabla ya kupata ubunge huu wa EALA, Bhanji aliwania nafasi mbalimbali za kisiasa bila mafanikio.
Alikuwa mgombea aliyekuwa akifahamika kwa kushindwa, kiasi kwamba kuna wakati Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, alipata kumtia moyo kwamba ipo siku kura zake zitatosha.
Niligombea ubunge mara nne. Mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 2005 kupitia Viti Maalumu kwa Mkoa wa Dar es Salaam lakini kura hazikutosha. Mara ya pili niligombea katika uchaguzi mdogo wa EALA-TZ mwaka 2006 ili kuziba nafasi ya Dk. Harrisson Mwakyembe na Beatrice Shellukindo ambao walikuwa wabunge wa EALA lakini walirudi nyumbani kugombea ubunge wa jimbo na kushinda na hivyo nafasi zao zilibaki wazi.
Sikushinda. Mara ya tatu ilikuwa 2010 niliamua kujitosa katika kura za maoni ndani ya chama changu (CCM) ili kuweza kupeperusha bendera ya chama kwenye Jimbo la Kindononi. Tulikuwa wagombea kumi na mimi nilikuwa mwanamke pekee katika kura za maoni. Hata hivyo Iddi Azzan ndiye aliyeshinda katika nafasi hiyo. Mara ya nne niligombea Ubunge EALA mwaka 2012 ndipo niliposhinda.
Maishani mwangu sijawahi kukata tamaa kwani naamini kwamba kukata tamaa ni dhambi kubwa sana. Kwenye maisha tunaambiwa kwamba iwapo hujapata kitu ambacho ungependa kuwa nacho basi labda Mungu anakuepusha na jambo, labda si wakati wako au sicho Mungu alichokupangia.
Sikukata tamaa ndiyo maana nimefika nilipofika. Kuna wagombea wengine ambao tuligombea nao ubunge mwaka 2005 walishakata tamaa mara baada ya kushindwa na waliposikia kuwa nimeshinda mwaka 2012 walinipigia simu wakijutia kwa nini walikata tamaa, anasema mbunge huyu huku sasa akitabasamu.
Kutokana na namna alivyotiwa moyo na Kikwete, Shy-Rose anamtaja mwanasiasa huyo kama mmoja wa waliomfanya atamani kuwa mwanasiasa na anayetamani siku moja afikie mafanikio makubwa.
Role models wangu kwa akina baba ni Marais wawili ambao ni Kikwete na Rais Paul Kagame wa Rwanda kwa namna ya kipekee wanavyohangaika kutatua changamoto za maendeleo katika nchi zao.
Nasema haya kwa vile nimeshafika Rwanda na kujionea maendeleo makubwa yaliyofikiwa miaka 20 baada ya mauaji makubwa ya kimbari nchini humo. Kwa kweli amefanya kazi kubwa sana katika kuleta umoja na mshikamano nchini Rwanda na vile vile kuleta maendeleo nchini humo.
Rais Kikwete amejitahidi sana katika utendaji wake. Changamoto ndani ya nchi yetu ni kubwa sana lakini amehakikisha kwamba mtandao wa barabara unakuwa ni kiwango cha lami na umerahisisha sana safari kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Pia amejitahidi sana kuhakikisha wanawake na vijana wanapata nafasi katika ngazi mbalimbali za uongozi, anasema.
Katika orodha yake hiyo ya watu anaowaona kuwa mfano katika jamii, Bhanji pia alimtaja Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dk. Regional Mengi kwa namna ya pekee alivyo karibu na jamii na jinsi anavyojitolewa muda na rasilimali katika kuwasaidia.
Kwa upande wa akinamama, Shy-Rose anatamani mafanikio ya Dk. Asha-Rose Migiro (Waziri wa Sheria na Katiba) na Profesa Anna Tibaijuka (Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi).
Hawa wawili ninawahusudu kwa uwezo na upeo wa kufika walipofika hadi ngazi ya Umoja wa Mataifa (UN) na katika ngazi ya Baraza la Mawaziri. Hii ni heshima kubwa sana kwa Tanzania na ni kielelezo kikubwa kwa akina mama kwa ujumla, anasema.
Sifa mojawapo ya mwandishi huyu wa habari aliyegeuka mwanasiasa ni kuzungumza jambo pasipo unafiki. Hii ni sifa adimu kwa wanasiasa na anasema kinachomponza mara nyingi ni tabia yake hiyo ya kuwa mkweli na kutokubali kuyumbishwa.
Namuuliza anadhani tabia yake hiyo ameirithi wapi.
Baada ya kufiwa na wazazi wangu katika umri mdogo sikuwa na mtu wa kumkimbilia katika matatizo na changamoto bali ilinilazimu kukabiliana nazo na ndipo nilipopata ujasiri. Nimepitia changamoto nyingi sana katika maisha yangu binafsi, kikazi na hata katika nafasi yangu kama mbunge kwa vile tu ninaongea ukweli. Mimi ni muwazi, mkweli na si mnafiki. Mara nyingi ukiwa na sifa kama hizi utakuwa na maadui wengi.
Ila kwenye siasa kuna uwongo na unafiki mwingi sana na ndiyo maana wanasema siasa ni mchezo mchafu changamoto haziishi na ndizo ambazo nakumbana nazo. Niko tayari kuzikabili kwani ndiyo njia niliyochagua.
Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuvuka chamgamoto mbalimbali hadi leo. Pia nichukue nafasi hii kuwashukuru wote walionisaidia kufika hapa nilipofika. Ninawaomba Watanzania waendelee kuwa na imani na mimi, anasema.
Sasa umefika muda wa Shy-Rose kuwahi Uwanja wa Ndege tayari kwa safari ya kwenda Nairobi kuhudhuria Mkutano wa Bunge la EALA unaofanyika huko. Ananiambia pamoja na changamoto zote alizokutana nazo, amefurahia muda wake wa ubunge.
Ni changamoto mpya katika maisha yake. Katika kipindi kifupi kijacho, amepanga kushawishi wabunge wenzake wapiganie mijadala ya EALA nayo ionyeshwe kupitia katika televisheni za nchi wanachama. Hii itasaidia sana wananchi kufahamu kinachoendelea na pia kurahisisha mtangamano wa kisiasa.
Ni changamoto nyingine ambayo ameamua kukabiliana nayo.
SOURCE: Raia Mwema - Shy-Rose Bhanji: Naponzwa na misimamo yangu
Addition:
"Zziwa said she is also being accused of having made comments that there was no genocide in Rwanda and refusing members of the regional committee to meet M23 DRC rebels."
source:https://www.jamiiforums.com/interna...ensured%92-for-wearing-high-heeled-shoes.html