Mahojiano JF: Madai ya Uraia ya Anatory Amani na tofauti zake za Kisiasa na Mhe. Kagasheki - #6

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,202
5,013
SWALI: Tofauti zenu za Kisiasa kati yako na Anatory Amani unatokana na nini? Ni kweli tofauti hizi zinachangia kuzorotesha maendeleo?





(Katika maandishi kutokana na video hii)


Unajua hili swala, mimi nafikiri kwa kuwa nimepata nafasi Jamiiforums naomba mnipe nafasi ya niliizungumza vizuri zaidi ,kwasababu utakuwa watu wengi wa Bukoba wanaliuliza ulizai,mimi siwezi nikawa na ugomvi ama na uadui ama na chuki, Anatolia Amani.

Anatoli Amani reteraly alikwisha futika katika siasa za Kagera, alijaribu kugombea ubunge Kyela Kagera mara mbili akashindwa, alijaribu jaribu mambo mengine mle kashindwa na akajibu mambo yake ya shule akashindwa.

Ni mimi na naweza kusema kwamba naregret lakini siregret kwamba nimefanya jambo baya,nia ilikuwa ni njema,niliitizama ile halmashauri yetu ,tulikuwa tumemaliza kipindi cha kwanza 2002 mpaka 2010 nikaona ni jambo jema tutakapoconstistute madiwanai balaza la madiwani tupate Meya ambaye katika mimi mtizamo wangu,atatusaidia,Bukoba inahitaji kusaidiwa,sitaki kwenda katika details za madiwani wakoje,background zao za education, kwasababu ni watu ambao wanachaguliwa na watu,I have no power over that, watu wa kata hii wakisema wanamtaka flani wa kata hii wakisema …..wewe huwezi kuwaambiwa msimtake,ukasema…no way!

Lakini sasa mmekwishachaguliwa mnalo baraza lenu la madiwani ili sasa halmashauri yenu iweze kufanya kazi, of course kiungo kikubwa pale ni Meya wa pale au Mwenyekiti wa ile Halmshauri na mimi kwakweli kwa nia njema kabisa niliona katika wale madiwani,na mimi nilimshawishi ,nikwambia kwanini usigombee udiwani akaniambia sasa mimi kugombea nikiwa ni diwani nikamwambia hapana gombea diwani alafu shabaha iwe ni ili uweze kuwa umeya

Sasa mimi mtu ninayemchukia mtu niliyekuwa na uadui naye siwezi kumshauri hivyo,siwezi kumtaka awe meya,kweli akapita katika udiwani,akapita katika umeya, na mtu aliyekuwa anashindana nae si mtu mdogo, alikuwa anashindana ni Mzee Samweli Lwangisa ambaye ni mzee ,amekuwa mbunge pale miaka 20 amekuwa meya muda mrefu sanapale,

Lakini kwasababu imani wa watu wa Bukoba walikuwa wanayo kwangu mimi,wakaona mbunge anania njema fine,tukampa dokta Amani,ambaye mnamwita dokta lakini is not even doctor any way.

Akaingia pale kwa nia njema kabisa,na mimi nikamwambia kwamba look,mimi ni mbunge lakini shughuli zangu,lakini sio mbunge tu lakii mim ni waziri shughuli zangu nyingi zitakuwa za kitaifa, shughuli za kuendesha hii halmshauri ni shughuli yenu madiwani kikubwa tuwe in consultation ,mniambie nini kinafanyika nini kinafanyika.

Tukakubaliana vizuri na kweli tukaanza vizuri,tatizo na unaweza kusema ugomvi wapi upo,kama unaweza kuuita ugomvi n kuiita wala sio personal sina sababu sijachukua pesa zake,sijachukua mke wake,sijachukua anything chake wala na yeye hajafanya vile kwangu mimi.

Tatizo limekuja katika mapesa ya halmashauri,na kwanini nasema tatizo, kwa mfano waliingia katika mikataba wa kutengeneza soko,mkataba wa pili mradi wa viwanja, mradi wa viwanja na mkataba wa tatu kujenga sehemu ya kuoshea magari pale car wash na mashine na nini pale Bukoba Mjini,na vitu vyote hivi vitatu ambavyo ni vikubwa vinainvolve pesa nyingi ,mimi ni mbunge pale nikaomba , naomba mnionyeshe mikataba ya vitu hivi.

Na nikasema mimi ni mbunge,maswala ya mikataba tunahangaika sana maswala wabunge wanahangaika sana na serikali sio kwa nia mbaya wanataka kuona , hii mikataba iko sawa sawa,hii mikataba inawasaidia watanzania,hii mikataba iko pale kusaidia watu binafsi.

Tatizo la kwanza nimekuwa nalo na mpaka leo nimezungumza, sikuona hii mikataba na these are big big project,kwa mfano baada ya kuvurugana kutaka kujua mikataba na mimi nikasema as long as sitaona mikataba,as log as sitaona kitu gani kimekuwa negotiated katika mikataba hii as long sitaona hizi pesa atalipa nani terms na terms zipi nikasema hakuna mradi utakaotekelezwa hapa as long as mi ni mbunge hapa,

Kumbe mimi I thought mimi napambana na Amani,it was not nilikuwa napambana na mkoa wa mkoa wa wakati ule nilikuwa napambana na mwenyekiti wa chama,nilikuwa napambana na katibu wa chama wa mkoa nilikuwa napambana na forces nyingi , kumbe unapozungumzia ufujaji wa mapesa ndani ya halmashauri,huu uilikuwa si ufujaji bali bomba la wizi ndio mimi nikaomba kabla hatujaenda mbali tupate odditing ya kujua mradi wa soko umekaaje,mradi wa viwanja 5000 umeakaje,mradi wa car wash station ambayo inajenga umekaaaje nk.

Kwanza ikakataliwa, Mkuu wa mkoa by then,mkuu wa mkoa akaweka mashinery yake ya pale mkoani, wakacome out wakasema the manispaa is clean, hauna kitu chochote kilchofanyika ,mbunge anapiga kelele tu na kwakuwa nilikuwa na baadhi ya madiwani ambao walisema tunakwenda na mbunge hata vikao havitafanyika mpaka tujue hatma ya hii miradi imekaaje.

Wale madiwani wakasema kwakuwa meya wao anamatatizo tumtoe,kwa sababu tunayo provision ya kufanya hivyo,na tunazo sababu za kufaya hivyo wala si za kuumuonea, mkuu wa mkoa akaingia kati,akasema hili haliwezi kufanyika,sasa tukasema how nyie mnaingiliaje kitu cha namna hii, tukawa na mzozo ndio hilo swali limekwenda kwenye chama mpaka limefika….mpaka kuja kufika…

Wewe tizama,ndugu zangu jamani tizameni,chama tangu lini ,hawa wamekwishakuwa madiwani wanautaratibu wao wa kiserikali,ambao unagovern biashara yao ndani ya….yaani wafanyaje kazi zao kwa utaratibu na miongozo yao.

Chama mnakaa level ya mkoa,wewe tizama mnafukuza madiwani wa CCM wa8,wala hata kufikiri tukiwa na uchaguzi hapa ambao lazima uwe by election CCM itashinda.?,mmekwisha wafukuza hao madiwani wa8,unauhakika ………nan i mimi nikwaambia mmefawafukuza madiwani 8 CCM hamtashinda na it's a fact sasa nikasema na hizi ni politics za wapi, tunafight siku zote kama wanasiasa ,kama vyama kupata dola,leo dola mnayo… kwasababu mnamprotect mtu mmoja ambaye amekwenda kinyume na utaratibu zote,mnaona bora hata uchaguzi uwepo jimbo liharibike,lakini mimi sishangai kwa sababu nilikuja kusikia ni hata tungempoteza mbunge,hii kuonyesha rushwa ya nchi hii ilipofika imefikia pahala pabaya, maana watu sasa ,sasa kitu nilichotaka kukuambia.. kuspend nafasi…..CGA na ninamshukuru Rais Kikwete on this one,na CAG isingekuwepoa kama asingekuwa yeye

Utasikia watu wanakwambia waziri mkuu sijui, Waziri mkuu TAMISEMI,ningesema maneno mabovu zaid hapa kwahiyo…. seriously na mimi nasema am gratefull and thankfull kwamba raisi aliweza kuona na hata uamuzi ya kwamba pelekeni CAG ulikuwa ni uamuzi wake,CAG amekwenda ameyatizama maeneo ripoti ile inatisha kungekuwa na good will ya kuwa na uchungu wa rasilimali za nchi hii TAMISEMI wangeshachukua action katika jambo hili ni vitu ambavyo viko so oviously na viko wazi, TAMISEMI mkapa leo hii ninavyozungumza na almost serikali imebakiza miezi mitatu nafikiri, by the end of june serikali inakuwa imekwisha, hakuna kitu ambacho kimefanyika.

Ukitizama hii,kwa mfano hii kampuni ya bia,kampuni ya kutengeneza car wash CAG amegundua kabisa mikataba haikufata utaratibu ,kwanza hakuna mikataba,kumbe ndio maana mi wakati naomba mikataba sikupewa,kwasababu mikataba haikuwepo ,not only that pesa zimetolewa wamekuja kutazama utaratibu mzima,your talking about milioni 297 ya kujenga car wash haina mikataba,haina kikao maalum cha balaza la madiwani kupitisha lakini ni kitu ambacho kimepitishwa…..alafu kampuni iliyopewa kufanya kazi hii hailipi,TRA haijulikani,BRELA haujulikani, sasa hizi ni kampuni za watu tu binafsi wamepeana,hilo tunaliacha.

Unakuja katika Swala la viwanja umekwenda umechukua ardhi ya watu 5000 square mita moja unamlipa mtu sh 300, wewe unauza sh 4500 kweli, mbunge siseme na akisema anawivu akisema anaogopa Amani atamnyanganya ubunge,kweli aaht his isn't possible na wako watu unaona kabisa wanalishabikia hilo wakasema kwamba…sasa ofcourse viwanja hivyo wame….kitu ambacho mimi nasema,wewe listern to this nikupe statistic kidogo na ndio maana nikasema nije hilo.

Halmashauri ilipopima hivi viwanja wakaingia ubia na UTT wapate pesa, halmashauri tarehe 21/06/2011 si ndio tumeingia pale ndio mwanzo 2010, jumla nzima ya pesa ya kufanya shughuli hiyo survey siji nini mpaka wauze viwanja ilikuwa ni shilingi Bilioni 1,318 milioni nah ii ni estimate waliitoa halmshauri, aliitoa huyu huyu meya,tarehe 20/6 four month later ilivyofika tarehe 10/10 estimate yake ikatoka 1bilioni point 3,ikaenda 2.2 bilioni kukawa na ongezeko la milioni908 shilingi ambao ni sawa sawa na 69% ilivyofika tarehe 6/11 waongeza jingine 767 milioni jumla sasa ikafika bilioni 2,994.

Sasa jamani CAG anasema kwamba hili lilikuwa ni kinyume na agizo 51 (2b)y a memorandamu ya fedha za serikali ya mtaa ya 2009 ambazo linazuia manispaa kujiengage katika vitu hivi bila kupata vibali vya waziri husika

Nikisema hili tatizo langu litakuwa wapi, na hiyo nitaisimamia kwahiyo vikao vilikuwa havifanyiki na kwaamaana hiyo ofcourse…..sio kwamba mimi niko proud,kuna mambo yangefanyika ingekuwa record yangu ingekuwa ni record ya chama katika utekelezaji wa irani.

Ya mwisho ambayo mimi nasema its important,ni soko la Bukoba, juu ya soko juu ya soko ,listen to this tena hii yoyote atayesikiliza kwa nia njema,nafikiria atasema wizi sasa imefikia pala ,hata sijui ndio maana me nasema TAMISEMI inanivuruga akili yangu,meya huyu mradi ule wa kujenga soko before hata ule mradi haujaingia makubaliano na kampuni ambayo,wanamwita sijui mkandarasi mwelekezi, huyo mkandarasi mwelekezi,ambalo kwa jina la kampuni yake anaitwa OGM whatever the company means, this OGM ndani yake sasa ilikua na kampuni nyingine nne,ambazo nyingine zinawahusu hao wengine ninaokutajia lakini ndugu yangu huyu ni mkandarasi mwelekezi, sio ya kujenga soko, charge yake charge yake yeye as a consultant ni shilingi 789 milioni, ndugu yangu wewe, honestry kwa akili yangu ya kawaida mimi ningependa niwe consultant nipewe pesa kama hizi, ningependa sana.

Sasa nikizuia na ni kweli nimekizuia na as long as mimi ni mbunge wa pale it will never happen,kwa sababu there is no way,sasa kama gharama ya consultant ni milioni 789,nigharama ya consultant, gharama ya kujenga soko itakuwa ni ngapi, kweli unataka kuniambia 789 milioni sio … na tunazungumza….hata ukichukua exchange rate na sio ya leo ya dola hii 2011 hivi kweli utakuwa haujenga kitu kikubwa ambacho inaweza kikaservice watu na hizi pesa kwamba zinajenga hizi zinaingia katika mfuko na sio kwamba anajenga anatoa muelekezi,sasa muelekezi wa soko anaelekeza kitu gani?


Na ana watu hapa kampuni nyingine ambazo ofcourse mimi hapa siwezi kuzitaja,CAG amezitaja sasa hili limenichukuli na muda, nan i mengi lakini nimeona nilieleze na haya ya msingi na ndio maana nasema hata ningekuwa nachaguliwa tena siwezi, project za namna hii siwezi huzikubali huu ni wizi,sasa mtu akisema eti umezuia maendeleo sijazuia maendeleo,hizi pesa mabilion haya yinakwenda katika mifuko ya watu na kama ndivyo watu walivyozoea na ndivyo biashara zinavyoenda mimi nasema that is not the way, atalipa nani hii kutoka wapi, halmshauri waliponegotiate na UTT walikubaliana kwamba faida itakayopatikana watagawana 50%, kwa 50% bila maelezo,bila kupitia katika baraza la madiwani,wakabadilisha,UTT watapa 60 na council wapata 40,juzi juzi hapa tumepiga kelele hapa wakasema sasa imebadilika itarudi 50 kwa 50 mimi nasema huu ni mchezo gani kama hii si rushwa kama hii si wizi.

SWALI: Vipi madai kuwa ulumpa Dr. Amani uraia wakati ukiwa Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya ndani?



(Katika maandishi kutokana na video hii)


Mimi sikumpa uraia na nisingeweza kumpa uraia wakati ule nilikuwa ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, portfolio ya Waziri yoyote Yule lakini more specific Wizara ya Mambo ya Ndani, yako mambo ambayo Naibu Waziri anafanya na yako mambo Naibu Waziri hawezi kama Waziri hayupo, swala moja ambalo Naibu Waziri hawezi hata akiwa anakaimu pale ni kutoa Uraia, hii ipo katika exclusive domain ya Waziri mwenyewe.

Amani alitolewa uraia, kunyang'anywa uraia tena kihaki wala sio nini na Rais Mkapa, sio mimi na wakati Rais Mkapa alikuwa rais, mimi sijawa Mbunge hapa. Baadae ameomba akapewa uraia, kwa hiyo uraia wa Amani sio uraia kama wa mimi na wewe ,wewe ni raia wa kuzaliwa yeye ni raia wa kupewa kwa Kiswahili wanasema raia tajinisi ama kwa kingereza wanasema naturalized.

Maana yake wewe na mimi sisi tumezaliwa hapa na hata mtu hawezi kuniambia wewe uende, nitamwambia niende wapi, yeye amepata uraia wa kuomba, confunsion mimi sijawahi kumpa uraia na wala hiyo isesemwe na mtu anayesema kitu hicho ni mzushi tu.Wapi nilimsaidia Amani? Ni hapa ambapo nitapataja…

Binti zake wawili,waliomba passport Wizarani, Wizara ikawakatalia, Amani akaniomba mimi, Kwamba binti zangu wameomba passport, Wizara imewakatalia, me nikasema but why…

Nilichofanya nikamwita ofisa husika nikamwambia niletee faili la Amani, Liko pale, ukienda Wizarani pale lipo, mimi langu lipo, lako lipo ,wakalileta faili la Amani, nikalitizama nikaona kwamba alikuwa approved, akapata uraia.

Nikawaamba tatizo ni lipi mbona msimpe mwanae, binti yake, wakaniambia kwamba tunalo tatizo la interpretation ya sheria, nikamwambia which one, wakasema ni kweli yeye ni raia lakini ni raia wa kuomba , nikasema fine lakini yeye ni raia, ni raia wa kuomba lakini n raia, wakasema kwa hiyo watoto wake itabidi waombe, nikasema waombe kitu gani sasa, wakasema itabidi waombe, nikawaambia lakini si ni raia, watoto wake by the virtual of the fact kwamba baba yao ni raia.

Lakini sio hivyo tu nikawakumbusha pale, nikawaambia sheria imebadilika, mama yao ni raia wa Tanzania, baba yao ndio ameomba lakini their mother ni raia wa Tanzania. Kwa hiyo kama hawawezi kupata rights kwa baba yao watapata rights kwa mama yao, nikasema zamani sheria tuliyokuwa nayo uraia ulikuwa unatolewa upande wa baba tu, lakini sasa hivi either ways.

Kwa hiyo kwangu mimi ilikuwa swala dogo, it was in that bases wala sio bases nyingine, isipokuwa nataka nikwambie kitu for the records, Amani alikuja anataka nimsaidie tuiondoe ile ya kwamba he is a natural citizen, lakini ni citizen wa kuzaliwa.

Nikawambia hilo sitoweza, lakini kwa kuwa sikutaka alisikie kwamba ni langu mimi peke yangu, nikampeleka kwa Waziri wa Mambo ya Ndani at that time Lorance Masha, nikamwambia Muheshimiwa Masha, mimi ni Naibu wako, huyu ni mwanajimbo mwenzagu alinyanganywa uraia anataka tumsaidie, ndio ombi lake, kuona kama uraia wake badala ya kuwa ni naturalized citizen wa Tanzania ionekane kama ni raia wa kuzaliwa, nakumbuka Masha alicheka, you can even asked him Masha laughed, tena Masha akamtizama machoni Amani, akamwambia aah we unataka kugombea uraisi.

This was Masha's question, wakati ule sasa yaani nayaweka haya wazi kuonyesha kwamba hii yote hii ya kusema sijui nilitaka kufanyaje kufanyaje, no me am not that kind bwana wala sio type hiyo, kwa hiyo hiyo ya uraia imekaa namna hiyo na Yule ni raia tajinisi wala sio raiawa, yeye na kesho na kesho kutwa mpaka dunia nyingine inakuja, raia tajinisi.

*Zingatia hii ni swali la kwanza katika orodha ya maswali yaliyojibiwa. Kwa taarifa zaidi tembelea - https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...rview-ya-jamiiforums-na-khamis-kagasheki.html



 
Last edited by a moderator:
Kadhalika sina upande, lakini kwa Kiswahili na Kısw-Kinge anachojaribu kutumia mleta mada, ni dhahiri kuwa naye ni mhamiaji tena toka Rwanda, anaweza asiwe haramu.Kwanza hakuna jimbo linaitwa Kyela mkoani Kagera na neno reteraly ni lafudhi ya Kinyarwanda kwa neno la Kiingereza Literaly.Kiufupi, mkuu umeandika vbaya sana, haueleweki, unabandika tu Kizungu kisichoeleweka.w
 
Kadhalika sina upande, lakini kwa Kiswahili na Kısw-Kinge anachojaribu kutumia mleta mada, ni dhahiri kuwa naye ni mhamiaji tena toka Rwanda, anaweza asiwe haramu.Kwanza hakuna jimbo linaitwa Kyela mkoani Kagera na neno reteraly ni lafudhi ya Kinyarwanda kwa neno la Kiingereza Literaly.Kiufupi, mkuu umeandika vbaya sana, haueleweki, unabandika tu Kizungu kisichoeleweka.w
Mkuu,
Wanyarwanda wanakutibua akili?
 
Hawa wanyarwanda wanaopewa uraia na hapohapo kuwa viongozi wataipeleka pabaya hii nchi.

Hawa watu ni virusi hatari
 
Huyu naye aachane tu na siasa, atulie anyolewe badala ya kushinda Jf anajisafisha wakati ukweli kaharibu mwenyewe. Hauwezi ukaliacha jimbo rehani kwa miaka 5 yote alafu ukategemea urudi ugombee, anasingizia ufisadi Wa viwanja na soko wakati hata vitu vidogo kama taa za barabarani zimemshinda, stand imemshinda, hata round about ameshindwa kuzidizaini bado tu amekomaa na meya. Ulitakiwa ujikumbushe kwamba wakati tuliopo ni results oriented, as a manager you need to balance the game kitu ambacho yeyr kashindwa badala yake anaanza siasa za kulialia.
 
Back
Top Bottom