Mahitaji ya mnyonge katika uchaguzi mkuu 2020

kALEnga kidamali

JF-Expert Member
Nov 19, 2015
542
733
Jamani sisi wanyonge tusio na sauti tupaze sauti zetu angalau na sisi tusikilizwe mahitaji yetu na hawa wagombea...

Kwa wagombea,
Mimi namtaka kiongozi mwenye msimamo usioyumba kwenye kutetea maslahi yangu kama mnyonge katika nyanja mbalimbali kama vile za kijamii,kiuchumi,kisiasa,n.k.

Kiongozi mwenye Sera zenye kuijenga nchi na kuwaunganisha wananchi wala sio kutugawa

Kiongozi mwenye sera za Kusimamia na kuzitumia rasilimali za nchi kwa manufaa ya nchi na wananchi wake.

Kiongozi atakae ilinda amani yetu.

Mahitaji muhimu kwa ufupi,
Lakini pamoja na hayo yote mimi mnyonge nipate yafuatayo:-
Maji safi,barabara,umeme,soko zuri la mazao yangu na unafuu wa kodi kwenye biashara zangu.

Hitimisho,
Hatimaye nimeyataja yangu, sasa nitoe fursa kwako na wewe utaje yako ila kigezo kwa mchangiaji utatakiwa uwe kundi la wanyonge sio bwanyenye kwani hutakuwa na uwakilishi mzuri wa hoja zetu sisi wanyonge,

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom