Mahindi yaanza kushuka bei sokoni

Mahindi yaanza kushuka bei sokoni

Upo kwenye ukanda upi chifu wewe, leo ukienda Rukwa na Mikoa jirani bei zina afadhali, walanguzi ni wengi kabla ya kununua fanya tathimini.

Bei ya Maharage na mchele ipo constant ila kwa Mahindi mzigo umeshuka bei.

Tusubiri na mzigo wa NFRA walanguzi tafuteni pa kujificha.
Nipo kwa mzee wetu Pinda huku komred wangu, mahindi yalishaisha Kwa sasa tunategemea mahindi kutoka Zambia. Na hiyo ndo bei iliyopo sokoni na mahindi yanatoka mjini kwenda kuuzwa vijijini .
 
Vyawa wa Lumumba na Mama hao,wapo kazini,baada ya Lissu kurudi na kuanza kuongea, tutarajie vyawa wengi sana kuongezeka na nyuzi za kila sarakasi.

Wana kazi ya kumsafisha aliekufa,wana kazi ya kumchafua Lissu aliehai na wana kazi ya kujibu ama kupotosha hoja za Lissu,bila kisahau kazi ya kumpaka marashi Mama!!
Kisoda cha bia ww
 
Hiyo mbegu inaitwa stuka 1? Au umenipa alert?
Kwahiyo utajubaliana na Mimi hakuna ya siku 70 na hopeful itakua kwenye majaribio na hizo siku Ni kukomaa sio kunyauka kwa ajili ya kuvunwa na kusaga kwa ajili ya kupata unga. Nashindwa kukubali au kukataa kwa sababu Sina uthibitisho
Ni SITUKA M 1
 
Ni jambo jema

Hayo Mahindi ya Siku 70 ndio yepi Katumani au GMO?
Katumaini, umenikumbusha mbali sana.

Katumaini mbegu fupi ina mahindi ya kuchoma matamu balaa.

Those Days naenda shambani na kidumu cha lita 5 cha maji ama dumu la lita 20 la maji na kiberiti tu. Nikienda sa 4 ama tatu narudi 12 jioni, nimechoma mahindi balaa. Usiku kujamba ni balaa tupu.

Miaka hiyo tunaenda kulinda mpunga, jirani kuna shamba la mahindi, pembeni mpunga, katikati ya shamba la mpunga kuna kibanda cha kupumzikia halafu kwenye kila angle ya shamba la mpunga umefunga tape za kanda za muziki zilizoharibika na kuvisha miti nguo ili kuwatisha ndege lakini ndege wabishi hawatishiki na wala hawababaiki, ukiwatisha hapa wanahamia angle nyingine, ukikimbia kufika kule wamehamia kule ulikotoka. Kama shamba ni kubwa na uko peke yako utakoma

Kazi ni kukimbizana na dege, kupiga kelele na miluzi siku nzima, huku una manati kubwa na mawemadogo madogo ya manati na ya mkono karibu kilo 10 ya kurushia ndege.

Ukikimbiza ndege, ukirudi unakula hindi la kuchoma, maji ya kutosha kupata nguvu tena za kukimbia.

Nakumbuka sana hayo maisha, of course ni maisha matamu sana. I really miss that life, miss a lot.
 
Vita ua Ukraine imeiaha au tutaambiwa kuna Tetemeko Uturuki

Tunapoelekea ni Pazuri tutakuwa na kiwanda kikubwa cha kuzalisha mbolea zaidi ya tani milioni moja mahitaji yetu ya ndani ni tani Laki Sita, hili limetuathiri sana kutoka na sisi kuwa waagizaji wakubwa wa mbolea kutoka nje ya nchi, Na Ukraine ni moja ya wazalishaji wakubwa mno wa mbolea pamoja na Russia so if you know you know.
 
Katumaini, umenikumbusha mbali sana.

Katumaini mbegu fupi ina mahindi ya kuchoma matamu balaa.

Those Days naenda shambani na kidumu cha lita 5 cha maji ama dumu la lita 20 la maji na kiberiti tu. Nikienda sa 4 ama tatu narudi 12 jioni, nimechoma mahindi balaa. Usiku kujamba ni balaa tupu.

Miaka hiyo tunaenda kulinda mpunga, jirani kuna shamba la mahindi, pembeni mpunga, katikati ya shamba la mpunga kuna kibanda cha kupumzikia halafu kwenye kila angle ya shamba la mpunga umefunga tape za kanda za muziki zilizoharibika na kuvisha miti nguo ili kuwatisha ndege lakini ndege wabishi hawatishiki na wala hawababaiki, ukiwatisha hapa wanahamia angle nyingine, ukikimbia kufika kule wamehamia kule ulikotoka. Kama shamba ni kubwa na uko peke yako utakoma

Kazi ni kukimbizana na dege, kupiga kelele na miluzi siku nzima, huku una manati kubwa na mawemadogo madogo ya manati na ya mkono karibu kilo 10 ya kurushia ndege.

Ukikimbiza ndege, ukirudi unakula hindi la kuchoma, maji ya kutosha kupata nguvu tena za kukimbia.

Nakumbuka sana hayo maisha, of course ni maisha matamu sana. I really miss that life, miss a lot.

Katumani bingwa wa maeneo yenye kupokea mvua chache fupi na komavu kwa haraka.
 
Hali bei ya mahindi katika masoko makubwa ya Nafaka katika sehemu mbalimbali mikoani imeonekana kuwa na ahueni mkubwa kutoka Tzs 25,000 kwa Debe hadi shilingi 16000-15000 Bei ya hivi leo. Katika maeneo ya;

Mwanza
Geita
Bukoba
Bunda
Manyara
Kibaigwa - Dodoma.

Mchele umeendelea kubaki katika bei yake ya juu sababu mavuno ni mpaka mwezi wa 3 mwanzoni au katikati kutokana hali ya upandaji.

Kwa Upande wa Kanda ya Ziwa hususani
Mwanza, Geita, Bukoba na Kigoma hupanda kwa misimu miwili Desemba na huu mwezi wa Pili unaoanza hivi sasa.

Kwa wale Waliopanda mwezi Novemba na Desemba ndiyo wanavuna sasa
Mahindi huchukua siku 70 tu kuvunwa.
Na Maharage huchukua siku 60 kuvunwa kutoka siku ya kupandwa.
Mpunga wenyewe huchukua miezi minne hadi kuvunwa.

Bei ya Mahindi itaendelea kushuka kuanzia sasa hadi Wiki ijayo Mahindi debe itakuwa shilingi 10,000. Bei ya kawaida.

Madukani bei ya unga imepungua sasa. Ni ahueni kabisa kwa Wananchi. Hali hii imetokana na uwepo wa Mavuni katika baadhi ya kanda, usambazaji wa mahindi kutoka ghala la chakula na kupunguzwa import duty kwa bidhaa za Nafaka kama walivyokubaliana katika kikao cha Jumuiya ya Afrika mashariki hivi karibuni.

Kwa Upande wa manyara tumeshuhudia Gunia la Mahindi kuuzwa 85000 hadi 90000/= kutoka bei ya awali ya shilingi 120,000/=
Hongera kwa Uchambuzi mzuri.
 
Jamani hapa mjini Babati mjini na Mitaa pamoja na vijiji vyake.Mahindi yote yaliyooteshwa kabla ya 2023 yamekauka.wengine wafanya chakula cha mifugo wengiine wamelima up ya
Yote kwa yote ni kilio
 
Back
Top Bottom