Mahindi yaanza kushuka bei sokoni

Mahindi yaanza kushuka bei sokoni

Billal Saadat

Senior Member
Joined
Nov 30, 2022
Posts
169
Reaction score
358
Hali bei ya mahindi katika masoko makubwa ya Nafaka katika sehemu mbalimbali mikoani imeonekana kuwa na ahueni mkubwa kutoka Tzs 25,000 kwa Debe hadi shilingi 16000-15000 Bei ya hivi leo. Katika maeneo ya;

Mwanza
Geita
Bukoba
Bunda
Manyara
Kibaigwa - Dodoma.

Mchele umeendelea kubaki katika bei yake ya juu sababu mavuno ni mpaka mwezi wa 3 mwanzoni au katikati kutokana hali ya upandaji.

Kwa Upande wa Kanda ya Ziwa hususani
Mwanza, Geita, Bukoba na Kigoma hupanda kwa misimu miwili Desemba na huu mwezi wa Pili unaoanza hivi sasa.

Kwa wale Waliopanda mwezi Novemba na Desemba ndiyo wanavuna sasa
Mahindi huchukua siku 70 tu kuvunwa.
Na Maharage huchukua siku 60 kuvunwa kutoka siku ya kupandwa.
Mpunga wenyewe huchukua miezi minne hadi kuvunwa.

Bei ya Mahindi itaendelea kushuka kuanzia sasa hadi Wiki ijayo Mahindi debe itakuwa shilingi 10,000. Bei ya kawaida.

Madukani bei ya unga imepungua sasa. Ni ahueni kabisa kwa Wananchi. Hali hii imetokana na uwepo wa Mavuni katika baadhi ya kanda, usambazaji wa mahindi kutoka ghala la chakula na kupunguzwa import duty kwa bidhaa za Nafaka kama walivyokubaliana katika kikao cha Jumuiya ya Afrika mashariki hivi karibuni.

Kwa Upande wa manyara tumeshuhudia Gunia la Mahindi kuuzwa 85000 hadi 90000/= kutoka bei ya awali ya shilingi 120,000/=
 
Nipo mwanza vijijin,mahindi yalishuka pale shule zilipofunguliwa yalifika mpaka 12,000 ila yalikaa wiki moja tu baadae yakapaa haraka sana mpaka sahv ni 18,000 sasa wewe sijui uko wapi
 
Hii ya sabini 70 umewahi kuisikia? Hata Kanyanya Ni 90 days.
Vyawa wa Lumumba na Mama hao,wapo kazini,baada ya Lissu kurudi na kuanza kuongea, tutarajie vyawa wengi sana kuongezeka na nyuzi za kila sarakasi.

Wana kazi ya kumsafisha aliekufa,wana kazi ya kumchafua Lissu aliehai na wana kazi ya kujibu ama kupotosha hoja za Lissu,bila kisahau kazi ya kumpaka marashi Mama!!
 
Yapo ya siku 75 lakini fuatilia stuka 1
Hiyo mbegu inaitwa stuka 1? Au umenipa alert?
Kwahiyo utajubaliana na Mimi hakuna ya siku 70 na hopeful itakua kwenye majaribio na hizo siku Ni kukomaa sio kunyauka kwa ajili ya kuvunwa na kusaga kwa ajili ya kupata unga. Nashindwa kukubali au kukataa kwa sababu Sina uthibitisho
 
Nafuu kwa walaji japo kurakua na walakini kwa mbegu za muda mfupi
 
Back
Top Bottom