Mahari ya harusi ikatwe kodi ya TRA

Mahari ya harusi ikatwe kodi ya TRA

Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2012
Posts
3,401
Reaction score
1,618
Moja ya sheria muhimu ya nchi ni PAYE (Pay As You Earn).

Naona nchi yetu inapoteza pesa ambazo zingetumika kununua madawati na kulipa mishahara kwa walimu.

Kuingiza pesa bila kulipa kodi huko ni kuhujum uchumi wa nchi, nadhani mnafaham adhabu ya kuhujum uchumi ipoje nchini kwetu.

Mimi kama MCHUNGUZI HURU napendekeza TRA ianzishe utaratibu ambapo kila familia itakayopokea mahari kwaajili ya binti anayeolewa wakatwe asilimia 18 ya pesa hizo.

ASANTENI
MCHUNGUZI HURU
 
Last edited by a moderator:
Mi nashauri wakate hadi VAT ya pumzi....
 
Kule Simiyu, SHinyanga, Mwanza, Mara na mikoa ya jirani itabidi wajenge mazizi ya ng'ombe wafungue na mabucha ya kutunzia nyama.

Mahari ngombe 100, TRA wanapewa ng'ombe 18. Kama mahari ng'ombe mmoja, wanapewa mat.ako ya ng'ombe, raha kweli.
 
Kwani ndoa ni biashara? Mwisho utaomba na sadaka zilipiwe VAT

TRA ni Mamlaka ya mapato tanzania,hakuna neno biashara hapo

Mahari ni pato na linaangukia kwenye kundi ambalo TRA inatakiwa kudai malipo

Upo hapo?
 
Mimi nashauri
Kuanzia kuwe na kulipia kodi ya kiatu unachovaa kiatu cha bei mbaya ulipie tax kubwa kanadambili shilingi 100 peku peku mwisho barabara ya Msimbazi

kama kumbukumbu ziko sahihi tulikuwa na kodi ya kichwa sijuwi imeishia wapi ile
 
Kweli kabisa umeishia hapo?

Kama ni ng'ome 18 haziwezi kuuzwa?

Kama ni ng'ombe mmoja wahusika hawawezi kulipa fedha?
 
Kwani ndoa ni biashara? Mwisho utaomba na sadaka zilipiwe VAT

BUSINESS: An organization or economic system where
goods and services are exchanged for one
another or for money .
SOURCE: m.businessdictionary.com/definition/business.html An organization or economic system where goods and services are exchanged for one another or for money .

Dr. MCHUNGUZI HURU (PhD)
 
Last edited by a moderator:
Kule Simiyu, SHinyanga, Mwanza, Mara na mikoa ya jirani itabidi wajenge mazizi ya ng'ombe wafungue na mabucha ya kutunzia nyama.

Mahari ngombe 100, TRA wanapewa ng'ombe 18. Kama mahari ng'ombe mmoja, wanapewa mat.ako yNa ng'ombe, raha kweli.
Nimependa mahari ya ng'ombe mmoja
 
lazima umelala na chuki/wivu/tamaa rohoni, kanywe dawa ulale tena.
 
Mimi nashauri
Kuanzia kuwe na kulipia kodi ya kiatu unachovaa kiatu cha bei mbaya ulipie tax kubwa kanadambili shilingi 100 peku peku mwisho barabara ya Msimbazi

kama kumbukumbu ziko sahihi tulikuwa na kodi ya kichwa sijuwi imeishia wapi ile

Aisee .....

Huyu nae hajui kama kiatu alichokivaa amekilipia kodi
Hajui kama barabara nazo zinalipiwa kodi

Nchi hii sijui ina watu wa aina gani tu!
 
TRA ni Mamlaka ya mapato tanzania,hakuna neno biashara hapo

Mahari ni pato na linaangukia kwenye kundi ambalo TRA inatakiwa kudai malipo

Upo hapo?

Tobaa! mbona kipato kile ninachopata kwa kutoka kwa baba chanja hakijadaiwa kodi? tena yeye ni mtumishi wa TRA? fafanua zaidi, labda si mapato yote... mimi nilidhani yale ya biashara tu.
 
Back
Top Bottom