Heshima yenu wakuu! mwenzenu hilo swali hapo juu linasumbua akili yangu hivyo nataka kufahamu. Binti anapochumbiwa na kutolewa MAHARI(pesa) huwa inaenda WAPI? Je,anapewa yeye mwenyewe yote kwa mambo yake binafsi, au wazazi/walezi baba na mama wanagawana peke yao, au familia nzima huwa inagawana wakiwemo mashangazi cjui wajomba madada na makaka, au binti mwenyewe na wazazi wake pekee, au huwa inawekwa kwa ajili ya maandalizi ya vitu kama kitchenparty na sendoff?,ama inakuwaje? Au matumizi na mgawanyo huo hutofautiana kabila na kabila? Nijuzeni mwenzenu mana sikuhizi mahari imekuwa kama mtaji mtu anaoa hadi kwa millioni 2 utadhani ananunua kiwanja magwepande daah! That y vijana bado wapowapo wakifikiria hapa, siwalaumuu! Haya karibuni kwa discussion..... Nitarudi bdaye! Cc Heaven on earth christine ibrahim Lady doctor @Lara1 Nivea Smile miss strong DEMBA Kongosho Mamndenyi Mtambuzi watu8 Himidini HorsePower Mr Rocky Kaizer and OTHERS...

.Kwa mujibu wa taratibu na mafundisho ya kiislam, Mahari huwa ni stahiki ya binti.
Mengineyo ni tamaduni na mapenzi binafsi juu ya mgao.
Mahari kama walivyotangulia kuchangia inategemea na mila za kabila lako. Kabila letu mahari ikitolewa kama ni ng'ombe wanauza ng'ombe unanunuliwa zawadi kadhaa, zinazobaki kama mna kijana wa kiume na yeye anatafutia mke na kwa kuwa zimepungua tayari baada ya kuuzwa hapo inabidi kijana asubiri either miaka miwili zizaliane ili zitoshe na yeye atoe mahari. Au mjomba anachukua jukumu la kununua hizo zawadi afu anapewa ng'ombe wawili.
Uchoyo huo mkuu.Ya binti zangu ntakula peke yangu lol
hakuna cha mjomba wala shangazi
haahaa! Hata mkeo humgawii?
Uchoyo huo mkuu.
sio uchoyo ni haki
siku hizi wanaume hawaoi binti asiye na kazi nzuri
na kazi nzuri mpaka binti asomeshwe shule nzuri na wazazi wake
mzazi unajinyima binti yako asome
halafu mtu akiona ana kazi nzuri analeta posa
sasa hapo unajilipa pensheni..lol
...duh kweli nyie noma......mi naona kwetu hata hizo mila hakuna maana ni full mchanaganyiko, so ambacho nilikiona kwa ndugu yangu ni hiyo mahali kupewa wajomba na wazazi wakagawana..vinhine hata cjuiSie kwetu mahari hadi walioko vijijini hata kama ni watoto lazima wapewe chao haijalishi ni 200,300 lazima wapewe.