Mahari bei gani

Ndio, kwani akiwa anaolewa mara ya pili au ya tatu ndio hafai kupewa zawadi?

Hata aolewe mara saba wa sabiini, ana hiari ya kuamua adai mahari au la

Duh, kumbe kuolewa mara nyingi dili.

Nikiolewa mara nyingine mahari yangu itakuwa shamba at least acre 1 lenye minazi na minanas
 
Unataka kutungiwa shairi ndiyo ukubali kufunga ndoa? Kama yeye si stadi wa utunzi je?

Ndio nikasema, na ninarudia tena kusema, ni makubaliano baina ya wanaotaka kufunga ndoa.

Binti ndie anaedai mahari, so atamuangalia anaetaka kumuoa ndio amwambie anataka nini. Wakifikia makubaliano, ndio linapelekwa kwa wazazi.

Shairi akisema hawezi kutunga, ataambiwa akatunge insha :lol:
 
Ujuavyo wewe si sahihi. Jamii za nchi za Asia kama Indonesia, Malaysia, Brunei na Kiarabu mahari anapanga binti na anakabidhiwa yeye akishayapokea.

Namjua dada mmoja Mu-Indonesia, alidai mahari mwanamme ajifundishe Quran yote kwa moyo kisha ndio ende akamuoe (hili halikuwa na faida kwa mwanamke moja kwa moja, alidhani akiweza hilo maisha yake yatakwenda kwa taratibu za dini anayoiamini tu)

Kwa hiyo wasiodai mali wapo tele duniani.

Hmmmm....hapa sasa itabidi watu tuzame kwenye nyenzo zetu tulichambue vizuri hilo neno 'mahari'.

Manake huo mfano wa huyo Muindonesia kwangu mimi ni kama sharti na si mahari. Sharti ni kwamba, ujifunze kwanza quran tukufu ndiyo unioe (tuoane).

Na kwa mantiki hiyo binti anaweza kusema kapimwe kwanza magonjwa ya zinaa na kama vipimo vikirudi na kuonyesha huna ndiyo unioe (tuoane)...? Na hii iitwe mahari?
 
Sina shida na mahari, shida yangu ni wanatumia vigezo gani kufika hapo kwenye Million 4 au Elfu 40
Gaijin naomba vigezo tafadhali
 
Kimsingi kwa sheria za Kiislam aliyotumia huyo Mu-Indonesia, mahari ni sharti tu [ambalo pia linaweza kutimizwa kidogo kidogo].

Kwa maana hiyo mtu anaweza kusema mahari yangu ni kwako wewe kufunga siku tatu, kutoa sadaka kwa masikini, kumsomesha mdogo wangu kusoma na kuandika, kunifundisha lugha ya kigeni unayoijua ambayo mimi siijui, nakadhalika nakadhalika
 
Duh, kumbe kuolewa mara nyingi dili.

Nikiolewa mara nyingine mahari yangu itakuwa shamba at least acre 1 lenye minazi na minanas

hahaha, ujue inategemea sheria gani zinafuatwa. Kama hapo kuna sheria za Kiislam zinahusika, ukijiachisha bila ya sababu ya msingi unatakiwa urudishe mahari ya watu.

Sasa dili linaweza kukutumbukia nyongo :lol:
 
Hahaha kwa hiyo wadai mahari wote ni "chuna buzi"!!!

Nyinyi ndo mnaiharibu dhana nzima ya mahari, mie nataka kudai kutungiwa shairi, hapo chuna buzi imehusikaje?

Nasindikiza kwa muziki
"Si hasara asilani, nyuki kufa asalini
Tuchekeni, furahani haha haha haha haha

Mahari uzaramoni unaweza kuambiwa 25,000/=

Basi sikilizia vikolokolo vingine hivyo, sijui bakora ya babu, mkoja, sijui usinga vitu kibao.

Ambavyo hata 100,000/= havifiki.

Hapo sasa ukimwambia mtu hii ni zawadi tu ya kuonyesha upendo anaelewa.

Sio mahari milioni nne? Kwani ndio mmesikia mahari ndio mwisho wa kushukuru kwa familia?

Matokeo yake, ukichanganya huu upuuzi wa mahari za kukomoana na harusi za kifahari, mtakuta watu wanaamua kuishi pamoja tu.

Utambulisho wa kwanza kwa wazazi mamaa kabeba ujauzito tayari.
 
hahaha, ujue inategemea sheria gani zinafuatwa. Kama hapo kuna sheria za Kiislam zinahusika, ukijiachisha bila ya sababu ya msingi unatakiwa urudishe mahari ya watu.

Sasa dili linaweza kukutumbukia nyongo :lol:

Alaa, sasa kama 'simuelewi' (nitakuwa naikalifisha nafsi yangu) kwa nini asiniache/nisimuache niolewe na yule 'ninayemuelewa'.
 
Sina shida na mahari, shida yangu ni wanatumia vigezo gani kufika hapo kwenye Million 4 au Elfu 40
Gaijin naomba vigezo tafadhali

Kimey hili suala gumu kujibu, kwa sababu kila mmoja ana vigezo vyake

Wengine wanaangalia mwanamme ana uwezo kiasi gani, wengine wanajithaminisha wao wafaa kupewa zawadi gani.

Wengine wanaangalia kwa misingi ya manufaa ya kiimani na wengine wanaangalia kwa manufaa ya ki-romantic zaidi

Nadhani inategemea hao wanaooana wakoje.
 
Mahari uzaramoni unaweza kuambiwa 25,000/=

Basi sikilizia vikolokolo vingine hivyo, sijui bakora ya babu, mkoja, sijui usinga vitu kibao.

Ambavyo hata 100,000/= havifiki.

Hapo sasa ukimwambia mtu hii ni zawadi tu ya kuonyesha upendo anaelewa.

Sio mahari milioni nne? Kwani ndio mmesikia mahari ndio mwisho wa kushukuru kwa familia?

Matokeo yake, ukichanganya huu upuuzi wa mahari za kukomoana na harusi za kifahari, mtakuta watu wanaamua kuishi pamoja tu.

Utambulisho wa kwanza kwa wazazi mamaa kabeba ujauzito tayari.

Sasa nyinyi mnataka kuharibu kwa kuharamisha dhana nzima ya mahari kwa ukosefu wa hikma wa watu wachache.

Mahari si lazima pesa na nawajua watu waliosema leteni chochote, wakaletewa mahari pesa nyingi wakazirudisha, wakasema haifai.

Harusi za kifahari mnataka wenyewe, kwani lazima? Mwanamke kama ana hamu ya kufanya harusi ya kifakhari si afanye kwa pesa zake? Wewe mwanamme imekuhusu na nini? Mengine mnajitakia wenyewe kisha mnalalama. Ati mwanamme amnunulie mwanamke shela sijui na mambo mengine.....why???
 
Huyo mbaba kayavulia, inabidi ayaoge.

Mwanamama kaona kaulizwa "bei"? Mungu ampe nini tena, gunia la chawa?

Hamad kibindoni.

Milioni nne.

Kama mie namwambia mama milioni nne si tatizo, ila sharti tupime mstari kwenye mshono kama Field Marshall Tantawi!!!

Hapo sasa.

Ukitaka mahari kubwa shurti ujue maadili.

Sio kila gumegume linaleta udumedume, kibiashara zaidi kama maskhara zaidi.
 
Alaa, sasa kama 'simuelewi' (nitakuwa naikalifisha nafsi yangu) kwa nini asiniache/nisimuache niolewe na yule 'ninayemuelewa'.

Kama humuelewi unamuacha/anakuacha lakini ndo mahari jamaa akiyadai inabidi uyakabidhishe kwake pamoja na inflation. Hakuna kukalifisha nafsi, ila pia hakuna dili

Kiranga

Kwani uliambiwa maadili hana? Na unapozungumzia maadili, ni yepi, hebu tupe vigezo tuone kwanza
 
Kama humuelewi unamuacha/anakuacha lakini ndo mahari jamaa akiyadai inabidi uyakabidhishe kwake pamoja na inflation. Hakuna kukalifisha nafsi, ila pia hakuna dili

Kujitoa kumo na mahari inarudishwa pale ambapo hakuna jimai. Kama alishagusa mahari/zawadi haiwezi rudi; si keshafaidi bana.

Kuna mila nyingine mahari ni ya 'bi harusi', familia haina hati miliki kabisa na chochote kila. Hebu fikiria wewe umetaka 'zawadi' ya shairi au insha, familia hapo inapata nini?
 
As far as I know, ni zawadi. Kuonyesha upendo kwa mwanamke anaeolewa na familia yake.

Na kwa zile jamii zenye tamaduni za wanawake kutoa mahari je? Na kwenyewe mahari ni ishara ya upendo kwa mwanaume?
 
Hivi mantiki ya kutoa mahari ni nini?

Originally ilikuwa a token of appreciation (chauvinist some may say) but several factors zimeibadilisha kabisa.

Kwanza zamani ilikuwa si nadra kukuta hata mahari kubwa inapotajwa, huwa haimalizwi. Mtu anatoa kiasi kidogo tu kinaitwa "kishikia mke" halafu anabaki forever indebted kwa familia ya mke wake. Na wengine hata walipokuwa na uwezo wa kuimaliza hawakuimaliza kama ishara kwamba shukurani ya kulelewa mke haiwezi kumalizwa.

Kuna baadhi ya jamii, kama Wasukuma kwa mfano. Mwanamme ukioa bila mahari huhesabiki kama umeoa, na mwanamke mzuri zaidi (some say mweupe zaidi) ndiye ana haki ya kudai mahari kubwa zaidi.

Kwa hiyo ungeweza kukuta baba anadaiwa mahari ambayo kashailipa kama mara mia kwa misaada mingine kwa upande wa wazazi wa mke.

Sasa siku hizi hizi habari za "mahari milioni nne" halafu tunapewa picha kwamba milioni nne isipokamilika hakuna ndoa, inaonekana imekaa kibiashara zaidi.

Wanawake inabidi wakubali moja.

A.Kuendelea kutolewa mahari na kuwa subservient kwa wanaume (wao wanaolewa, wanatolewa mahari, hawawezi kuwa sawa na wanaume, essentially utumwa fulani hivi).

B.Kukataa mahari na kudai usawa na wanaume.

Hawawezi kutaka vyote viwili kwa pamoja, la sivyo mahari itolewe na pande zote, kuwe na exchange of gifts tu.

Na wasituambie habari zaunyumba ni exchange kwa mahari kwa sababu that will just be prostituting the entire institution of marriage.

Sometimes I wonder if there is much of a difference anyway.
 
Kujitoa kumo na mahari inarudishwa pale ambapo hakuna jimai. Kama alishagusa mahari/zawadi haiwezi rudi; si keshafaidi bana.

Kuna mila nyingine mahari ni ya 'bi harusi', familia haina hati miliki kabisa na chochote kila. Hebu fikiria wewe umetaka 'zawadi' ya shairi au insha, familia hapo inapata nini?

Jimai peke yake haitoshi. Yeye alikuwa na dhana ya kuwa atafaidi milele, wewe umemfaidisha siku mbili kisha umwambie keshafaidi mahari usirudishe?!

Sema kama ndio shairi au insha inakuwa imekula kwake. Maana hairudishiki

Familia inafaidi kwa kuona mtoto wao anakwenda kwa mwanamme anaempenda na kuweza kumpa mahari aliyoyataka
 
Back
Top Bottom