Mahari bei gani

Wana Jamii Forum naomba kuwasilisha hapa mbele ya jukwaa hili
Nina mpenzi wangu kamaliza chuo now nataka nioe kabisa!! Tukiwa katika maongezi ya kawaida tu nikamdokezea
Hivi mahari yako ni kiasi gani mchumba wangu kaniambia millioni nne!!Kiukweli na mpenda sana lkn naona hio pesa nyingi japo uwezo wa kuitoa nianao Je Ndio mahari za siku hizi zilivo? Naomba ushauri wenu wana JF

Hivi ukilia hali kwa bodi ya mikopo vipi haiwezi kusaidia?
 
Ukishalipiwa mahari 4M, unasubiria mume aendelee kukuletea perfumes na gari kama zawadi nyingine? Ndo maana hamuishi kunyanyaswa! Babangu akitaka 4M ya mahari nitamlipa mie mwanae, afu ataniskia bombani!

Wingi wa mahari na kunyanyaswa hauhusiani hata punje, maana si kama ukilipiwa mahari madogo hutanyanyaswa. Hao wanaonyanyaswa wote na kusumbuliwa na waume zao ni kuwa waliwatoza mahari makubwa?
Babangu akitaka 4M ya mahari nitamlipa mie mwanae, afu ataniskia bombani!

Hilo ni lako wewe na baba'ako. Ila haimaanishi kuwa ndio ubora wa amali.

Mahari inapaswa kubakia kama symbol ya heshima ya kumchukua binti wa wenyewe. Na sio biashara! Umuhimu ni kwenye kujuana pande mbili na kujenga upendo.

Sasa naona unataka kuwapangia watu waonyeshe symbol ya heshima kwa mantiki yako wewe. Huwezi kuwapangia watu wengine hesima wao waionyesheje. Kuna wengine kwa familia zote mbili Milioni 4 ni peanuts kwa hiyo ni sawa na elfu kumi yako wewe.

Nitarudia tena mfano wangu wa Binti Mfalme aliyetoa mahari ya mji mzima wa Bombay kwa kuonyesha heshima kwa mume wake mtarajiwa.

Is it too much? Maybe to some.
 
lipa m2 tu mahari huwaga haimalizwi....au unawezalipa nusu then utaendeleakulipa taratibu kadri mnavyoendelea kuishi....usikonde kwa mawazo ya mahari mkuu kikubwa angalia kweli mtaishi kwa upendo huo hadi mwisho???so lipa nusu hata m 1.5 then baadae utapunguza kidogo!!!
 
Mmmh..pole kaka..lipa tu utafanyaje..tena fanya fasta akipata masters ndo atazidi kuwa ekspensiv..
 
hivi hawa ng'ombe wa kizungu kumiliki 300+ kwa wakulima wa kawaida si rahisi.

Mara nyingi ng'ombe 30 ni hawa wa kienyeji. Na unapooa angalia msimu maana unatabiri bei ya ng'ombe.

Mwezi wa nane ni kiangazi, baadhi ya maeneo njaa ishaanza so wanauza ng'ombe so cheap labda laki mbili kwa hiyo bei yang'ombe wa mahari ni cheap zaidi.

Unatakiwa ubargain kwa ng'ombe halafu una-convert kwenye hela kulingana na soko la wakati huo. Ukienda msimu wa mavuno inakula kwako maana ng'ombe wanapanda bei.

Ila vijijini hawachukui pesa, wanataka ng'ombe kabisa.

Mmmmh ni hivyo eee? Maana niliona humu JF ng'ombe wa kisasa wa maziwa kila mmoja anauzwa 950,000 na kuendelea hadi 1,350,000. Sasa hii ya milioni nne kupata ng'ombe 30 imenishtua na kunishangaza sana.

Hebu nieleweshe mnavyo bargain wakati wa mahari inakuwaje? Mnakuwa mna bargain ng'ombe au thamani yake?
 
Kiherehere chako....ulitumwa umuulize yeye? Me ndo ningekwambia million 100 hasa mana haihusu mwanamke kuulizwa mahar yake
 
Mahari 4Mil,
Harusi 15Mil,
Kianza Maisha 3Mil.

Kaka sikushauri hata kidogo,
Waambie una laki 7, wakikataa piga chini demu utafute mwengine.

Mimi kuna demu nlimlipiaga Ada ya miaka mi-3 CBE, baada ya demu kupata ki-degree chake eti kwao wakaniambia mahari 3.5Mil, nkawaambia wakate kwenye Ada nliyomsomeshea mwanao, wakagoma.

Nika-surrender na kutemana nae yule demu.
 
Sa unalalamika nini, kama unataka kuoa wewe toa hizo mil 4, kama huna wako wenye uwezo watamuoa.
 
Sa unalalamika nini, kama unataka kuoa wewe toa hizo mil 4, kama huna wako wenye uwezo watamuoa.



Naomba kuuliza - sasa kwa mfano mimi YATIMA - hizo milioni 4 si inabidi nichukue mwenyewe??? SINA BABA - SINA MAMA - SINA MJOMBA WALA SHANGAZI - SIN BIBI WALA BABU

Sina hata Mama au Baba wa Hiyari - Nimekulia mitaani - nikafanya biashara ndogo ndogo - Mungu akanibariki - ikaukua kidogo - nikajua kununua mitumba - kuvaa - kusuka nywele - na NIMEPENDEZA - jamaa ndio anataka kunioa - MAHARI AMPE NANI?? SI ANIPE MIMI YATIMA AU???????????

Naomba ushauri wenu - Great Thinkers!!!!!:smile-big:
 
Ila vijijini hawachukui pesa, wanataka ng'ombe kabisa.

kwa maana hiyo bei halisi ya ng'ombe sio muhimu, muhimu uwapelekee ng'ombe wao tu.

Au ukienda kununua ng'ombe ukisema ni kwa ajili ya mahari unauziwa kwa bei ya chini?

*nipo katika kutafuta kuelewa kwa nini ng'ombe wa mahari tuambiwe ana thamani ndogo ya ng'ombe mwengine
 
Naomba kuuliza - sasa kwa mfano mimi YATIMA - hizo milioni 4 si inabidi nichukue mwenyewe??? SINA BABA - SINA MAMA - SINA MJOMBA WALA SHANGAZI - SIN BIBI WALA BABU

Sina hata Mama au Baba wa Hiyari - Nimekulia mitaani - nikafanya biashara ndogo ndogo - Mungu akanibariki - ikaukua kidogo - nikajua kununua mitumba - kuvaa - kusuka nywele - na NIMEPENDEZA - jamaa ndio anataka kunioa - MAHARI AMPE NANI?? SI ANIPE MIMI YATIMA AU???????????

Naomba ushauri wenu - Great Thinkers!!!!!:smile-big:

Mahari kimsingi inategemea watu na watu. Hata wasiokuwa yatima, wenye wazazi wote hai hadi babu na bibi, wapo wanaompa mahari yote anaeolewa.

Kimsingi kwao mahari ni ya anaeolewa (na yeye ndie husema iwe kiasi gani wakati mwengine) na akiamua kuwagaia wazazi wake ni kwa mapenzi yake tu.

Wewe usie jamaa bila ya shaka ni yako wewe na wewe ndie utakaepanga atoe ngapi.
 
kaka mkuu hiyo ni kubwa sna tena sana, mahali inatakiwa ikizidi sana laki tano tu, ila laki tatu ndio mahale pake.
 
Bei gani is right. Maana unanunua mtumwa.

Kesho keshokutwa ukimtwika mkeo utumwa atakataa?

Halafu ndo wanawake hawahawa wanaodai usawa? Au hawa wengine?

The entire institution of marriage is disillusioned and in a state of collapse, what remains is utapeli na biashara.
 
usiogope ni pesa ndogo sana wewe kalipe kama ikiwa nyingi watakurudishia chenji yako itajayo baki.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom