Mahanga achangayikiwa!?

Kutokana na kesi inayomkabili Mbunge wa Segerea Mhe. Mahanga jana wakati akihitimisha mjadala wa muswada wa sheria kuhusu Mamlaka ya udhibiti wa mashirika ya hifadhi za jamii alijikuta akijitabulisha kama anazungumza kwa niaba ya waziri wa fedha badala ya waziri wa kazi na ajira.

Nashauri ni muda muafaka washauri nasaha wamsaidie ili asichanganyikiwe zaidi!
Tuambie hukumu ni lini ?hayo mengine hayasaidii kitu
 
Tuome Mungu, Haki Itendeke; Nadhani ni wakati mwafaka wa Kujipima Dar es salaam; baada ya kujipima kwenye chaguzi ndogo za udiwani (Mwanza, Songea, Kiwira, Tanga, Dodoma) na ubunge Mkoani Arusha (Arumeru). Ni vizuri tukijitadhini hapo Segerea.
 
Unajaribu kuunganisha kesi na majukumu ya MAHANGA BUNGENI. Hujatutendea haki tusiojua mwenendo wa kesi yenyewe. Tafadhali njoo na up-dates za kesi angalau kwa manufaa ya sisi Bush-stars
Kwa manufaa ya nyie Bush-stars, baada ya kuwasiliana na waliokuwa wanahudhuria kesi hiyo mahakamani (siyo wanaosoma magazeti tu), ni kwamba Mahanga hana hata shitaka moja kwenye kesi hiyo iliyo mbele ya jaji, kwa maana ya iliyo kwenye petition ya mpendazoe - maana yake ni kwamba mpendazoe hajamlalamikia mahanga kama mahanga, hata ya kushikwa na masanduku halikulalamikiwa na mpendazoe (ni mashahidi tu waliokuwa wakiropoka mahakamani, na wote hakuna aliyemwona, ila, "nilisikia, nilisikia". Mpendazoe asingelalamikia uvumi huo wa masanduku kwa sababu wakati wakivumisha mahanga kashikwa kituo cha polisi buguruni, mpendazoe na mahanga walikuwa segerea wakihangaikia kura za udiwani kata ya segerea, hivyo mpendazoe anajua huo ulikuwa uvumi tu. KUMBUKENI SUALA LILILOIBULIWA TU GHAFLA MAHAKAMANI NA HALIKUWA KWENYE PETITION, SIKU YA MWISHO WALA MAHAKAMA HAILIJADILI HATA KIDOGO! Pili, Mpendazoe hakulalamikia kampeni chafu, hakulalamikia uvunjaji wa sheria kwenye upigaji wa kura, hakulalamikia uvunjaji wa sheria kwenye kuhesabu kura kwenye vituo. Analalamikia ujumulishaji wa kura kwenye kituo cha kujumilishia kura, BASI! Sheria inasema kama malalamiko yako kwenye ujumulishaji wa kura (TALLYING), lazima uombe kitu kinaitwa SCRUTINY(sijui kama kuna wanasheria kwenye jamvi hili). Maana yake lazima uombe kupitia upya tallying ya kura kwenye maeneo unayodai majumuisho hayakufanywa vizuri. MPENDAZOE HAKUOMBA HIYO SCRUTINY!!! Mwisho, mashahidi wote 14 wa mpendazoe, pamoja na yeye, hakuna hata mmoja alitoa evidence yoyote iliyopokelewa na mahakama. HATA MOJA! Ukiacha gazeti la mwananchi la mabox hewa!

Sasa mtajaza, kama kuna haja kweli ya kumhonga jaji ili kesi hii itupiliwe mbali, na gharama zilipwe na mlalamikaji. Lo! Masikini Mpendazoe, alivyochacha, na nyumba yake ya Segerea iko mnadani, atatoa wapi hela za kulipa gharama za kesi hii? Wana CDM mwanze kumchangia.
 
Mkuu unatafuta kura yake tu,Makongoro amechanganyikiwa hivi mtu uliyenormal unaweza kweli ukasahau position yako? Lini makongoro kawa Naibu waziri wa fedha?
Mimi sikumsikiliza Mahanga alipozungumza Bungeni, lakini kama alisema hivyo, mbona ni kuteleza ulimi tu, wangapi tunateleza ulimi na wala hatuna kesi mahakamani? Kuteleza ulimi kunahusishwa vipi na kesi mahakamani? Acheni chuki za kij"&"&|*...!
 
Na umwambie kiwanja che2 pale bima alipojenga bar yake(nyantare)akirudishe,yule ni mwzi tena sio mwiz wa kujifunza bali wa kurithi.
Hili la NYANTARE, nasikia watu wanaomchukia Mahanga kule Segerea wamekwenda hadi kwa wenye kiwanja (Kariakoo Market), wakaenda na wizara ya ardhi .... majibu waliopata huko na vielelezo, walijiona wajinga, sasa wako kimyaaaa. Wala huyo Bw. Sungura mwenye baa ya Nyantare (aliyekodi kiwanja hicho kutoka Kariakoo Market) ambaye anatoka Kigoma, wala hawajuani na Mahanga (anayetoka Musoma). Mara mvumishe amebeba masanduku ya kura, mara mvumishe ana baa ya nyantare, mara mvumishe amejenga night clubs, mara mvumishe hajafanya chochote segerea. Uliza buguruni hadi vingunguti barabara za lami.. uliza vingunguti barabara za lami na daraja la uhakika,... uliza kiwalani barabara ya kijiwe samli, barabara ya jet corner vituka, uliza tabata barabara ya kuelekea mawenzi na kimanga... uliza segerea barabara ya tabata, segerea, kinyerezi, uliza segerea mwisho (eti kuna mtu humu anasema anaishi segerea mwisho) stendi ya kimataifa ya daladala segerea mwisho bila yeye isingekuwepo pale, uliza kinyerezi barabara za lami, uliza stakishari, barabara ya kutoka kinyerezi, uliza kipawa barabara ya banana kwenda kipunguni na kitunda. Ameshinikiza tanroad wapanue barabara kutoka airport hadi banana, kero kubwa ya foleni pale kwisha kabisa. MNYONGE MNYONGENI, HAKI YAKE MPENI. At mbunge wa NEC! NEC ndiyo waliokuja kumpigia kura Ukonga mwaka 2000 akapata kura 85,000 akawa wa kwanza TZ nzima? NEC ndiyo ilikuja kumpigia kura mwaka 2005 akapata kura 130,000 akawa wa kwanza TZ nzima? Na kama jimbo lisingegawanywa mwaka 2010 angepata tena kura nyingi kuliko wabunge wote Tanzania. Wote hawa anawahonga kweli? Mahanga ni jembe! Mimi binafsi namkubali saaaana.
 
Jinamizi la kuwa raia linamwandama kwa sababu hajazoea kupita mitaani bila kusalimiwa.
 
Huyo aanze mazoezi ya kushika jembe hana lake tena segerea.jeuri ya fedha ni umauti.
 
Kwa manufaa ya nyie Bush-stars, baada ya kuwasiliana na waliokuwa wanahudhuria kesi hiyo mahakamani (siyo wanaosoma magazeti tu), ni kwamba Mahanga hana hata shitaka moja kwenye kesi hiyo iliyo mbele ya jaji, kwa maana ya iliyo kwenye petition ya mpendazoe - maana yake ni kwamba mpendazoe hajamlalamikia mahanga kama mahanga, hata ya kushikwa na masanduku halikulalamikiwa na mpendazoe (ni mashahidi tu waliokuwa wakiropoka mahakamani, na wote hakuna aliyemwona, ila, "nilisikia, nilisikia". Mpendazoe asingelalamikia uvumi huo wa masanduku kwa sababu wakati wakivumisha mahanga kashikwa kituo cha polisi buguruni, mpendazoe na mahanga walikuwa segerea wakihangaikia kura za udiwani kata ya segerea, hivyo mpendazoe anajua huo ulikuwa uvumi tu. KUMBUKENI SUALA LILILOIBULIWA TU GHAFLA MAHAKAMANI NA HALIKUWA KWENYE PETITION, SIKU YA MWISHO WALA MAHAKAMA HAILIJADILI HATA KIDOGO! Pili, Mpendazoe hakulalamikia kampeni chafu, hakulalamikia uvunjaji wa sheria kwenye upigaji wa kura, hakulalamikia uvunjaji wa sheria kwenye kuhesabu kura kwenye vituo. Analalamikia ujumulishaji wa kura kwenye kituo cha kujumilishia kura, BASI! Sheria inasema kama malalamiko yako kwenye ujumulishaji wa kura (TALLYING), lazima uombe kitu kinaitwa SCRUTINY(sijui kama kuna wanasheria kwenye jamvi hili). Maana yake lazima uombe kupitia upya tallying ya kura kwenye maeneo unayodai majumuisho hayakufanywa vizuri. MPENDAZOE HAKUOMBA HIYO SCRUTINY!!! Mwisho, mashahidi wote 14 wa mpendazoe, pamoja na yeye, hakuna hata mmoja alitoa evidence yoyote iliyopokelewa na mahakama. HATA MOJA! Ukiacha gazeti la mwananchi la mabox hewa!

Sasa mtajaza, kama kuna haja kweli ya kumhonga jaji ili kesi hii itupiliwe mbali, na gharama zilipwe na mlalamikaji. Lo! Masikini Mpendazoe, alivyochacha, na nyumba yake ya Segerea iko mnadani, atatoa wapi hela za kulipa gharama za kesi hii? Wana CDM mwanze kumchangia.

Kama wewe ni mwanasharia unatakiwa kujua kuwa umevunja sharia kwa kuzungumzia kesi ambayo ipo mahakamani na bado hukumu kutolewa.

Kuwa na subra ili usije ingilia maamuzi halali na huru ya mahakama.

Inaweza ikawa aibu sana mahakama kumpa ushind mahanga maana amebanwa kila kona kama wakicheza hatuto amini tena mahakama kwamba ni chombo cha kuonyesha haki itabid tuamini nguvu zagiza nasio mawalili wala mjaj
 
Kama wewe ni mwanasharia unatakiwa kujua kuwa umevunja sharia kwa kuzungumzia kesi ambayo ipo mahakamani na bado hukumu kutolewa.

Kuwa na subra ili usije ingilia maamuzi halali na huru ya mahakama.

Wana CHADEMA (walioanzisha thread hii, na nyingine nyingi za nyuma) wakijadili mwenendo wa kesi hii na kuendeleza sana mjadala, siyo kuingilia uhuru wa mahakama, lakini wengine wakijadili mwenendo huo huo, wanaingilia mahakama! Mkuki kwa nguruwe..., siyo?
 
Naomba ujue kuwa baya alilipwi kwa baya.

Ndio maana nikakuuliza kama kweli wewe ni mwanasharia kitaaluma basi nafikiri ujumbe utaupata kwani hili ni moja ya maadili na ethics za wanasharia hususan kwa nchi yenu yenye kufuata Rules of Law (Utawala wa sharia).

Nawapa pole sana.
 
Andika utawala wa sheria, hiki ndiyo kiswahili sanifu! Ukiandika utawala wa sharia wengine tunakuwa na wasi wasi!
 
Andika utawala wa sheria, hiki ndiyo kiswahili sanifu! Ukiandika utawala wa sharia wengine tunakuwa na wasi wasi!

Akhasantum.

Kumbuka Kiswahili ni lugha yangu ya Pili. Lugha yangu ya awali ni Kiarabu.

Tuvumiliane kwa hilo.

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom