Mahakamani kwa kujifanya waziri wa Ulinzi

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,954
22,125
Friday, October 09, 2009

MKAZI mmoja wa Mbagala, Shiza Rajab (25) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala ya ya jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kujifanya Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Tanzania.

Mshitakiwa amesomewa mashitaka hayo leo na Mwendesha Mashitaka Mrakibu wa Polisi Naima Mwanga mbele ya Hakimu Samweli Maweda wa Mahakama hiyo.

Katika shitaka la kwanza imedaiwa kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Juni mwaka huu kwa kujifanya kuwa yeye ni Naibu Waziri wa Ulinzi kwa lengo la kujipatia fedha kutoka kwa Brigedia wa Jeshi katika Kikosi cha Nyumbu, Mabula Mashauri.

Iliendelea kudaiwa kuwa katika shitaka la pili mshitakiwa alijipatia kiasi cha fedha shilingi milioni 2.4 kutoka kwa Mashauri ambazo alizichukua katika Benki ya NBC tawi la Pugu kupitia akaunti namba 033201095824.

Hata hivyo, mshitakiwa amekana mashitaka hayo na kesi yake itatajwa tena Oktoba 20, mwaka huu Mahakamani hapo.

Wakati huo huo, mbele ya hakimu huyo vijana watatu Elius John (24), Said Bakari (26) na Solomoni Othuman (30) wamefikishwa mahakamani hapo kwa tuhuma za wizi wa komputa aina ya Dell iliyokuwea na thamani ya shilingi 500,000.

Imedaiwa kuwa washitakiwa hao walitenda kosa hilo Januari 7, mwaka huu, jijinio Dar es Salaam kutoka kwendye gari aina ya Toyota Hiace..

Washitakiwa wote wamekana shataka lililotajwa dhidi yao na kesi hiyo itarudi tena Oktoba 20, mwaka huu kwa kutajwa.
 
Back
Top Bottom