Mahakamani bila ya ushahidi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahakamani bila ya ushahidi

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by wanatamani, Jul 21, 2011.

 1. w

  wanatamani JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 413
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  ninajamaa yangu alimkopesha mtu pesa kiasi cha shilingi 420000tsh. Baada ya wiki kupita mtu aliyemkopesha akamfuata tena na kumuuliza kama kunakiwanja kinauzwa maeneo ya morogoro road. Jamaa yangu akaamua kupiga simu kwa mjumbe wa serikali ya mtaa picha ya ndege kibaha (wanafahamiana) .jibu likapatikana kiwanja kipo ila kina nyumba ndani yake kinauzwa shiliki 26,000,000. Jamaa yangu na yule nayehitaji kiwanja wakaenda kuangalia. Jamaa akakipenda akaahidi baada ya wiki angeenda kulipia.ilipotimia wiki hawakuenda kulipia tajri akampigia simu rafiki yangu mimi mbona kimya au auziwe mtu mwengine.rafiki yangu akamfuata anayehitaji akamjibu mambo bado hayaja kaa sawa.
  Basi habari ya kiwanja hicho ikaaishia hapo. Wiki tatu zilizo pita yule anayehitaji kiwanja akampigia simu rafiki yabgu njoo uchukue pesa uiliyonikopesha nimeshapata, rafiki yangu akamfuata alipofika akamkuta yupo na askari polisi 3.wakamkamata mpaka kituo kidogo cha polisi vijimbweni kigamboni, alipofika akawa analazimishwa kusoma karatasi ,ikabidi asome.
  Kilicho kuwamo kwenye karatasi hiyo ni mauziano ya kiwanja kati ya yule bwana na mtu ambaye rafiki yangu mimi hamfahamu hata kidogo, picha ya yule bwana na muuzaji rafiki yangu pia hamfahamu ikionyesha nauziano hayo yamefanyika kibaha saini muhuri vyote vya serikali ya mtaa kibaha kwa thamani ya shilingi milioni kumi 10,000,000. Jamaa yangu alipo maliza kusoma mlalamikaji akadai anataka alipwe shilingi milioni mbili2,000,000 ndio kesi iishe,.
  Rafiki yangu alishangaa sana mauziano hayo kwani hayajui hakuna jina lake wala saini lakini anadaiwa atoe milioni mbili.
  Akakataa na kupelekwa kitio kikuu kigamboni akawekwa kwa muda wa siku 7 akitakiwa alipe hizo pesa.
  Kwa bahati nikamfuata mke wake akamdhamini ,rafiki yangu yeye akasafiri kwa kumuaga mpelezi akatakiwa siku ya jumano aripoti kituoni ,ajabu siku ya jumanne askari mpelezi akanifuata mimi akitakanimletee rafiki yangu au mdhaminiwake kwani mlalamikaji ameenda kwa ocd kumshitakia kuhusu kumchelewesha yule jamaa . Basi nikamfuata mdhamini akawekwa lockup siku nzima mpaka alipokuja nae kudhaminiwa na ndugu zake.
  Mpaka sasa tumesha kwenda kupata ushauri wa kisheria kulichoelezwa ni kuomba kesi iende mahakamani.
  Tunaomba ushauri zaidi kwa hili mimi nimefikiria hivi kama inawezekana:-
  tuandika barua kulalamika kwa igp nakala kwa ocd na rpc kawa hivyo inawezekana kabla ya suala hili kufika mahakamani
  maana kesi ipo wazi hata hao waliofanya mauziano hawajaitwa mtu apelekwe mahakamani huu ni uonevu.

   
Loading...