mkatagogo
JF-Expert Member
- Nov 21, 2015
- 229
- 43
Nimekuwa nikitafakali kwa muda sasa hivi kuna haja gani kwa mahakama za Tanzania kutoza kiwango kikubwa kwa wanaokata rufaa ya matokeo ya uchaguzi ikiwa lengo nikutafuta haki? Maana gharama hizo zimekuwa kubwa sana,swali lakujiuliza je kwa mtindo huu si ni kama nchi imeamua kutotoa fursa sawa kwa wananchi wake ktk kupata uongozi ktk nchi yao maana wenye fedha wanaweza kutumia nafasi hiyo kuujumu wanyonge ktk chaguzi wakiamin watu hao Ni wanyonge na hawana ubavu wakulipia gharama za uendeshwaji wa kesi binafsi naona sio sahii kuweka gharama kubwa kufungua kesi ya kupinga matokeo maana uko tuendako hatma ya nchi itakuwa mikononi mwa watu wenye fedha na nguvu kiuchumi Ni rai yangu kwa serikali hasa kama inania ya dhati ya kukuza demokrasia hapa nchi maana sasa huduma ya mahakama imekuwa anasa