Mahakama yasitisha mgomo wa madaktari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahakama yasitisha mgomo wa madaktari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ALEX PETER, Jun 23, 2012.

 1. ALEX PETER

  ALEX PETER Senior Member

  #1
  Jun 23, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  [h=2]TAARIFA KWA UMMA

  Yah: Mahakama Kuu ya Tanzania imetoa amri ya kusitisha mgomo wa Madaktari [/h] Kufuatia Tangazo la Chama cha Madaktari nchini (MAT) la kuanza mgomo siku ya Jumamosi tarehe 23 Juni, 2012, Mahakama Kuu ya Tanzania, Kitengo cha kazi, Dar es Salaam imetoa amri ya kusitisha mgomo huo mpaka hapo pande zote mbili yaani Serikali na Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) yatakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.


  • Amri hiyo ya Mahakama imetolewa kufuatia maombi namba 73 ya 2012 yaliyowasilishwa chini ya hati ya dharura na Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Chama cha Madaktari Tanzania (MAT). Sababu za msingi amabazo zimepelekea Mahakama kuu kutoa amri hiyo upande mmoja ni pamoja na;

  • Iwapo mgomo huo utatokea utakuwa na kuwa amri hii isipotolewa madhara yake ni makubwa isiyoweza kufidiwa kwa namna yoyote ile kama vile kupoteza maisha n.k


  • Wajibu maombi, ambao ni MAT, inaundwa na Madaktari ambao wapo katika Sekta ambayo inatoa huduma mahsusi (essential service sector), Aidha Chama cha Madaktari Tanzania kimetangaza mgomo bila kufuatia taratibu zilizoanishwa katika Kifungu cha 76(1 na 2) cha Sheria ya Kazi (Employment and Labour Relations Act No 6 ya 2004).
  Masharti hayo ni


  • Kuzuia wafanyakazi walio katika Sekta Muhimu kugoma na kama wakigoma,
  • Kuwepo na makubalianao ya pamoja ya kutoa huduma za msingi wakati mgomo ukiendelea.
  Kwa misingi hii, Mahakama Kuu ya Tanzania, kwa Chama cha Madktari Nchini na wanachama wake kusitisha na kutoshiriki katika mgonmo huo.

  Source: http://www.wavuti.com/#ixzz1ybEcOCDs
   
 2. KUSHOKA

  KUSHOKA JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2012
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 468
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 60
  Kila kitu hakiko wazi mahakama wanazuia mgomo uliochini ya chama wakati madaktari wanagoma kupitia jumuia ya madaktari! yaan na full ABRAKADABRA.
   
 3. Mr.Professional

  Mr.Professional JF-Expert Member

  #3
  Jun 23, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,602
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kumbe tz kuna sarakasi zimeanza tena ngoja nijongee karibu na katelevision kangu sizitizame
   
Loading...