Mahakama yaombwa kuharakisha kesi za ugaidi zinazowakabili waislamu

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,884
pic+mahakama.jpg
Msemaji wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania, Sheikh Rajab Katimba

Dar es Salaam. Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania imezitaka mahakama kuharakisha kesi za ugaidi zinazowakabili waislamu mbalimbali nchini kwasababu wamekaa zaidi ya miaka mitatu jela.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, msemaji wa jumuiya hiyo, Sheikh Rajab Katimba amesema taasisi hiyo inapinga vitendo vya ughaidi ila wote walioshikiliwa wanatakiwa uchunguzi ukamilike ifahamike kama wamehusika au la.

"Masheikh na waumini mbalimbali wamekamatwa karibu kila mkoa nchini, inadaiwa uchunguzi unaendelea na miaka inaenda. Mahakama iharakishe kesi hizo," amesema Sheikh Katimba.

Chanzo:Mwananchi online
 
Kweli ni muda sasa mpaka ukweli ukidhibiti,kama si kweli siwatakuwa wameshataabika sana.Serikali inawajibu wa kuangalia hili na kulifanyia uharaka kupitia vyombo vyake vya sheria.
 
Kama wanahatia wakumiwe na kama hawana basi waachiwe, ili tuwe na imani na mahakama zetu, maana inawekana kuna mkono wa serekali hapa!
 
Imani na mahakama nilipotezaga kitambo sana utasemaje mahakama huru wakati viongozi wa mhimili huo wanateuliwa na mtu mmoja
 
Washikishwe adabu hatutaki viashiria vya ugaidi nchini kwetu

Pumzi zinakuhadaa, wako wakubwa zaidi ambao walikuwa na chuki na roho mbaya zaidi kuliko wewe sasa wameondoka imebaki fremu za mifupa kule Saudia Arabia imehifadhiwa watu wanaenda kutalii wakiiangalia.
 
Lkn lile lipuuzi lingine kiongozi wa Waislam Dar yy kulamba laba miguu tu ya watawala
Uamsho wao kwa sasa hawafikishwi Mahakamani
Kumpinga Dr Shein ZNZ inakuwa ugaidi
Waislam kuweni kitu kimoja la sivyo mtaumizwa kila siku
Sisi wa Roma Kadainali Pengo kawa kama Waziri serikalini,tunakula tu kuku kwa mrija!
 
Inabidi wachunguzwe kwa makini sana na Serikali ijiridhishe bila kuacha shaka.Gaidi sio binadamu maana anaweza kuteketeza halaiki ya watanzania.
 
Waislamu kitabu chao kina aya kabisa za kufanya ugaidi , kuwachukia wakristo na wayahudi, waacheni wakae hukohuko mahabusu...shenz kabisa
 
Back
Top Bottom