Mahakama ya Rufaa yasisitiza Mchechu kulipwa Sh Bilioni 2.5 na kampuni ya Mwananchi Communication Ltd

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,177
Reaction score
7,472
MAHAKAMA ya Rufani nchini, leo Tarehe 4 June 2025, imetupilia mbali maombi ya rufani namba 658 ya 2023 yaliofunguliwa na kampuni ya Mwananchi Communication na Mhariri wa Gazeti la The Citizen.

Kampuni ya Mwananchi Communication, ilikata rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu wa kumlipa fidia ya sh bilioni 2.5 Msajili wa Hazina, Nehemia Mchechu kwa kuandika habari iliyomchafua.
Screenshot 2025-06-04 214131.jpg
Katika habari hiyo iliyochapishwa na Gazeti la The Citizen tarehe 23 Machi mwaka 2018, iliripoti kuwa Mchechu wakati huo akiwa Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ni fisadi na alitumbuliwa na Rais John Magufuli, jambo ambalo sio kweli.

Rufaa hiyo ilipitiwa na majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa ambao ni Jaji Rehema Kerefu, Jaji Omar Othman Makungu na Jaji Dk. Benhajj Masoud.

Katika uamuzi wake jana chini ya jopo la Majaji watatu, Mahakama ya Rufaa imekubaliana na uamuzi wa Mahakama Kuu kwenye kesi namba 48 ya 2021 kwamba habari hiyo ilikuwa ya uongo na imechafua hadhi na heshima ya Mchechu ndani na nje ya nchi, hivyo tozo iliyotolewa ni sahihi.

Katika uamuzi wake, Mahakama ya Rufani iilipitia hoja tatu za msingi.
WhatsApp Image 2025-06-04 at 12.02.23.jpeg
Hoja ya kwanza ni je, Mahakama Kuu ilikuwa na uwezo kusikiliza shauli hili, pili mdai (Mchechu), aliweza kuthibitisha madai yake ya kudhalilishwa na hoja ya tatu ni kama Mahakama Kuu ilitumia utaratibu sahihi kutoa nafuu kwa walalamikiwa

Kwa mujibu wa uamuzi huo, jopo hilo la majaji walikubaliana na hoja za wakili wa utetezi, Aliko Harry Mwamanenge kwamba Mahakama Kuu ilikuwa na uwezo wa kusikiliza kesi hiyo na kwamba mjibu rufani alifanikiwa kuthibitisha madai yake.

Jopo hilo la majaji pia wamekubali kwamba Mahakama Kuu ilitumia utaratibu sahihi kufikia tuzo ambayo ilitoa.

Hivyo, Mahakama ya Rufani haikuona sababu ya kubatilisha au kubadilisha chochote kwenye maamuzi ya Mahakama Kuu na kuyabariki maamuzi hayo kama yalivyo.

Awali, Mahakama Kuu iliamuru Gazeti la The Citizen kumlipa Mchechu sh bilioni 2.5 kwa kuandika habari iliyomchafulia jina lake.

Katika adhabu hiyo, sh bilioni 2 ni kwa ajili ya kumlipa fidia kwa kuchafulia jina alilolijenga kwa muda mrefu na kumshushia heshima na sh milioni 500 kwa ajili ya kumsababishia hasara ya jumla.

Mbali ya kiasi hicho cha fedha, Gazeti la The Citizen limeamuriwa kulipa gharama zote za uendeshaji wa kesi kuandika habari ya kumwomba radhi katika ukurasa wake wa mbele kwa ukubwa ule ule na italipa fidia asilimi 12 kila mwaka endapo litashindwa kulipa fedha hizo kwa wakati kuanzia jana.

Katika hukumu hiyo, Mahakama Kuu pia imelionya Gazeti hilo kutomwandika tena Mchechu habari ya uongo na yenye kumchafulia jina kiasi hicho isipokuwa pale tu kunapokuwa na ukweli na ushahidi wa kutosha

Hukumu hiyo imetokana na kesi iliyofunguliwa na Mcheche dhidi ya Gazeti la The Citizen, akiiomba mahakama iliamuru Gazeti hilo limlipe fidia ya Sh bilioni tatu na kumwomba radhi, kwa madai ya kumchafulia jina na kushusha hadhi na heshima yake katika jamii.
 
MAHAKAMA ya Rufani nchini, leo Tarehe 4 June 2025, imetupilia mbali maombi ya rufani namba 658 ya 2023 yaliofunguliwa na kampuni ya Mwananchi Communication na Mhariri wa Gazeti la The Citizen.

Kampuni ya Mwananchi Communication, ilikata rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu wa kumlipa fidia ya sh bilioni 2.5 Msajili wa Hazina, Nehemia Mchechu kwa kuandika habari iliyomchafua.

Katika habari hiyo iliyochapishwa na Gazeti la The Citizen tarehe 23 Machi mwaka 2018, iliripoti kuwa Mchechu wakati huo akiwa Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ni fisadi na alitumbuliwa na Rais John Magufuli, jambo ambalo sio kweli

safi sana, ona ushenzi wa hawa wapuuzi eti magazeti, anayewatuma kuandika ujinga huu atawalipia

1749053184994.png

1749053206925.png
 
Siku hizi serikali watu hawaii kama zamani watu wanaiba kihalali kabisa kwa vifungu vya sheria.......unda kampuni jipe tenda kazi imeisha.

Huyu mchechu ana mzigo wa hatari...picha kinaanza nyumbani kwake kuna nyumba mbili kubwa na ndogo ukienda kajamba nani humuoni unaishia nyumba ndogo ucheze na walinzi.
 
MAHAKAMA ya Rufani nchini, leo Tarehe 4 June 2025, imetupilia mbali maombi ya rufani namba 658 ya 2023 yaliofunguliwa na kampuni ya Mwananchi Communication na Mhariri wa Gazeti la The Citizen.

Kampuni ya Mwananchi Communication, ilikata rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu wa kumlipa fidia ya sh bilioni 2.5 Msajili wa Hazina, Nehemia Mchechu kwa kuandika habari iliyomchafua.

Katika habari hiyo iliyochapishwa na Gazeti la The Citizen tarehe 23 Machi mwaka 2018, iliripoti kuwa Mchechu wakati huo akiwa Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ni fisadi na alitumbuliwa na Rais John Magufuli, jambo ambalo sio kweli
Rufaa hiyo ilipitiwa na majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa ambao ni Jaji Rehema Kerefu, Jaji Omar Othman Makungu na Jaji Dk. Benhajj Masoud.

Katika uamuzi wake jana chini ya jopo la Majaji watatu, Mahakama ya Rufaa imekubaliana na uamuzi wa Mahakama Kuu kwenye kesi namba 48 ya 2021 kwamba habari hiyo ilikuwa ya uongo na imechafua hadhi na heshima ya Mchechu ndani na nje ya nchi, hivyo tozo iliyotolewa ni sahihi.

Katika uamuzi wake, Mahakama ya Rufani iilipitia hoja tatu za msingi.

Hoja ya kwanza ni je, Mahakama Kuu ilikuwa na uwezo kusikiliza shauli hili, pili mdai (Mchechu), aliweza kuthibitisha madai yake ya kudhalilishwa na hoja ya tatu ni kama Mahakama Kuu ilitumia utaratibu sahihi kutoa nafuu kwa walalamikiwa

Kwa mujibu wa uamuzi huo, jopo hilo la majaji walikubaliana na hoja za wakili wa utetezi, Aliko Harry Mwamanenge kwamba Mahakama Kuu ilikuwa na uwezo wa kusikiliza kesi hiyo na kwamba mjibu rufani alifanikiwa kuthibitisha madai yake.

Jopo hilo la majaji pia wamekubali kwamba Mahakama Kuu ilitumia utaratibu sahihi kufikia tuzo ambayo ilitoa.

Hivyo, Mahakama ya Rufani haikuona sababu ya kubatilisha au kubadilisha chochote kwenye maamuzi ya Mahakama Kuu na kuyabariki maamuzi hayo kama yalivyo.

Awali, Mahakama Kuu iliamuru Gazeti la The Citizen kumlipa Mchechu sh bilioni 2.5 kwa kuandika habari iliyomchafulia jina lake.

Katika adhabu hiyo, sh bilioni 2 ni kwa ajili ya kumlipa fidia kwa kuchafulia jina alilolijenga kwa muda mrefu na kumshushia heshima na sh milioni 500 kwa ajili ya kumsababishia hasara ya jumla.

Mbali ya kiasi hicho cha fedha, Gazeti la The Citizen limeamuriwa kulipa gharama zote za uendeshaji wa kesi kuandika habari ya kumwomba radhi katika ukurasa wake wa mbele kwa ukubwa ule ule na italipa fidia asilimi 12 kila mwaka endapo litashindwa kulipa fedha hizo kwa wakati kuanzia jana.

Katika hukumu hiyo, Mahakama Kuu pia imelionya Gazeti hilo kutomwandika tena Mchechu habari ya uongo na yenye kumchafulia jina kiasi hicho isipokuwa pale tu kunapokuwa na ukweli na ushahidi wa kutosha

Hukumu hiyo imetokana na kesi iliyofunguliwa na Mcheche dhidi ya Gazeti la The Citizen, akiiomba mahakama iliamuru Gazeti hilo limlipe fidia ya Sh bilioni tatu na kumwomba radhi, kwa madai ya kumchafulia jina na kushusha hadhi na heshima yake katika jamii.
Wamlipe tu.
 
kama vile hukumu imechakachuliwa, sijaona serious evaluation of evidence. Wamebabia babia .. I stand to be corrected! Sidhani kama wana mgao, hawa wanaheshimika sana.

Hoja ya Time limitation haikuwa addressed ( au nime scan vibaya)
 
Attachments

Back
Top Bottom