Mahakama ya Rufaa yaondoa utata wa rufani za Mahakama ya Kazi

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
187,543
2,000
Uamuzi wa waheshimiwa Majaji 5 wakiongozwa na Kaimu Jaji Mkuu leo umeondoa utata juu ya rufani zitokazo Mahakama ya Kazi sasa rufani tajwa hazihitaji vibali za mahakama hiyo ya kazi kabla ya kufunguliwa Mahakama ya Rufaa chini ya kifungu cha 57 cha sheria ya Taasisi za Mahakama ya Kazi.


Baadhi ya Maamuzi ya Mahakama ya Rufaa yaliweka sharti la kibali kinyume na mahitaji cha kifungu cha 57 tajwa.

Wakiyabatilisha maamuzi tajwa Mahakama ya Rufaa ikiongozwa na Kaimu Jaji Mkuu imeweka wazi haki ya rufani haipo kwenye sheria moja tu ya Mamlaka ya Mahakama ya Rufaa au AJA(2002) bali haki tajwa imo kwenye sheria nyingi ikiwemo sheria ya Taasisi za Mahakama ya Kazi au LIA Labour Institutions Act.

Chini ya kifungu cha 57 cha LIA haki ya rufani tajwa iko wazi na hakuna kibali chochote kutoka Mahakama ya Kazi kinachohitajika.

Hongera sana waheshimiwa Majaji husika kwa kukataa tabia iliyoanza kujengeka ndani ya Mahakama ya Rufaa ya kuingilia uhuru wa Bunge kwa kujitungia sheria kazi ambayo siyo yao.

Uamuzi husika umeambatanishwa.
 

Attachments

Lexus SUV

JF-Expert Member
Sep 16, 2016
2,023
2,000
Sasa hii nini tena jamani!???

Nchi hii si hahina dini !? Nini hii!!?
 

Dragoon

JF-Expert Member
Nov 24, 2013
7,037
2,000
Daaa! Mkuu Rutashubanyuma Ahsante sana. sasa hapa hii ndio njia ya kufungua njia ya matakwa ya rufaa zinazotoka mahakama kuu na divisheni za ardhi na biashara ya kuhitaji kibali cha mahakama kabla ya kukata rufaa mahakama ya rufani.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom