Mahakama ya Rufaa Kenya Mfano wa Kuigwa East Africa

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
40,316
72,742
Nchini Kenya Mahakama ya Rufaa imewaachia huru viongozi 7 wa chama cha madaktari waliohukumiwa kifungo cha mwezi mmoja gerezani siku ya jumatatu kwa kukiuka maagizo ya mahakama ya kusitisha mgomo wa madaktari ulioanza mwanzoni mwa mwezi Desemba mwaka jana.

6dd31ba8b2d50925076c76e1a7cac455.jpg


Source: DW

My take:
Hii ndiyo namna ya kushughulikia kesi zenye maslahi ya umma. Ndani ya saa 48 appeal tayari imesikilizwa na kutolewa hukumu.

Ni wakati sasa na mahakama zetu kuliangalia hilo hapa kwetu hasa kwenye kesi zinazoleta malalamiko ya wengi na kuzifanyia hivyo na sio kukomoana kwa kitu kinachoweza kufanyiwa kazi within hours.
 
Sasa ukiangalia kama kesi ya Lema ya kuangalia upatikanaji wa dhamana ambao uko wazi kisheria kuna sababu gani kuchukua miezi mitatu?
 
Sasa ukiangalia kama kesi ya Lema ya kuangalia upatikanaji wa dhamana ambao uko wazi kisheria kuna sababu gani kuchukua miezi mitatu?
Kesi ya Lema haina public interest. Ni upuuzi alioufanya mwenyewe kutokana na ujinga wake. Mache aendelee kusota rumande. Asiyefunzwa na mamaye atafunzwa na ulimwengu
 
Sio vizuri mihimili hii kuwekwa mifukoni mwa matajiri lakini visiwekwe mifukoni mwa wanasiasa pia!
 
Kesi ya Lema haina public interest. Ni upuuzi alioufanya mwenyewe kutokana na ujinga wake. Mache aendelee kusota rumande. Asiyefunzwa na mamaye atafunzwa na ulimwengu
Halina public interest ? Sio kweli yule ni kiongozi wa watu wa Arusha. Halafu hilo la kusema ni ujinga wake, hapa hatuzungumzii kesi ya msingi bali dhamana yake
 
Jambo usilolijua ni kama usiku wa giza!


Hapa hatuzungumzii ukubwa wa tatizo la rushwa Bali ufanisi wa kazi katika speed ya kutoa maamuzi.
Waweza kuwa na kiwango cha chini cha rushwa lakini pia ujawa na kiwango cha juu cha ugoigoi na kukosa ufanisi
 
Huku Tz Tumetanguliza Matumbo Mbele.....akisimama jaji wa mahakama kuu unaweza dhani ni Mtoto wa chekechea au muingizaji
 
Back
Top Bottom