Mahakama ya mafisadi itawaumbua CCM

Mahakama ya mafisadi itawaumbua CCM

Ushahidi wa ufisadi wa lowassa utatolewa na lema,mbowe,Mnyika,lissu na Slaa
Utakuwa umezaliwa jana, ushahidi utatolewa na Mwakyembe. Hao wote waliaminishwa hivyo na ripoti ya Mwakyembe hadi siku walipopewa maelezo yaliyokinzana na ya awali.
 
Mkuu awafunge wote hakuna cha kubagua tunachoomba sisi watanzania ni mh magufuli awafunge wote walio lifikisha taifa hapa tulipo


Mkuu umesahau kuwa ccm ni ile ile, na kwa kuhitimisha hilo amesema wazi atawalinda viongozi wastahafu kwa hiyo hapo hakuna jipya
 
Kwani wewe ulifikiri mafisadi waliokuwa wanaingia mikataba mibovu walitoka UDP ama CUF? ama Magufuli alipokuwa anasema mafisadi wametafuna nchi hii alikuwa ana maana ya CUF na UDP ambao hawajawahi kuingia mikataba kwa niaba ya serikali? Mbona mnapenda kujilengesha kwa vitu vilivyo wazi. Mafisadi kwa 100% watakuwa wale waliowahi ama walio CCM maana ndo chama kimetawala mda wote. hii nayo inahitaji diploma kutuelezea?
Mkuu umeongea ukweli mtupu ingawa utakuwa ni mwiba mchungu kwa baadhi ya watu ambao kwao kila kitu ni kushangilia tu
 
Mabehewa feki wajiandae kwenda kukaba lofu
 
Mkuu umesahau kuwa ccm ni ile ile, na kwa kuhitimisha hilo amesema wazi atawalinda viongozi wastahafu kwa hiyo hapo hakuna jipya
Ndio hapo ule usemi maarufu unao sema kinacho mponza kambale ni mdomo wake kufuata chambo kwenye ndoano,siyo siri ccm wamejipalia mkaa
 
Ndio hapo ule usemi maarufu unao sema kinacho mponza kambale ni mdomo wake kufuata chambo kwenye ndoano,siyo siri ccm wamejipalia mkaa


Nasubiri wampe Chama kwanza halafu nione watu ndani ya ccm wanavyong'olewa meno bila ganzi
 
Intelejensia inaonesha ukimpeleka lowassa mahakamani kutahatarisha amani kwahiyo tumeamua kutomshtaki
Unawaza kama mimi yaan lowasa ni mtaji kwa ccm, na itakuwa advantage kwao kwa kutowafikisha wengne mahakaman kwa kisingizio kuwa mbona lowasa ajaperekwa, tusubir tuone
 
Ni dhahiri sasa mahakama ya mafisadi inaanzishwa nchini. Mahakama hii itakuwa na kazi moja tu,kusikiliza kesi za mafisadi na kuwahukumu.

Kwa muda sasa CCM povu limekuwa likiwatoka kwa madai kuwa Lowassa ni gwiji la mafisadi nchini,na kwamba CHADEMA walipotoka kwa kumpokea Lowassa. Kwamba haiwezekani mtu ambae CHADEMA walipiga kelele miaka yote kuwa ni fisadi,iweje leo wampokee na kumpa nafasi ya kugombea urais? Povu liliwatoka kwelikweli.

Na jibu la CHADEMA lilikuwa moja tu,kwanini hamkumshitaki kipindi chote hicho? Kama ni fisadi ilikuwaje hajashtakiwa? Swali lilikuwa gumu sana kwa CCM. Tena ikafika kipindi Lowassa mwenyewe akasismama kwa kiburi na kuvimba akawaambia "mwenye ushahidi aende mahakamani". Sentensi hiyo ilikuwa ni msumali wa moto kwa CCM. Hawakwenda mahakamani hadi leo.

Sasa mahakama ya mafisadi imeanzishwa.CCM hawatakuwa na sababu tena ya povu kuwatoka kumtukana Lowassa kwenye mitandao ya kijamii. Tunategemea watafanya jambo moja tu,kumpeleka Lowassa katika mahakama hiyo. Kinyume na hapo hawatakuwa na "mandate" tena ya kumtukana Lowassa kwa sababu wananchi watawauliza "kama Lowassa ni fisadi mbona hapelekwi kwenye mahakama ya mafisadi? Hawatakuwa na cha kujibu. Kwa hiyo option pekee ya CCM na serikali yake ni kumfikisha Lowassa mahakamani,kinyume na hapo Lowassa atakuwa amewafunga goli la kisigino.

Kama wakimpeleka itabidi wawe na ushahidi wa kutosha kuweza kuthibitisha ufisadi wa Lowassa. Je ushahidi huo wanao? Kwa kitendo cha Lowassa kutamka kwa kujiamini kuwa mwenye ushahidi aende mahakamani,ni dhahiri ana uhakika hawana ushahidi huo. Kama hawatakuwa na ushahidi Lowassa atawabwaga katika kesi hiyo kuwaaibisha vibaya. Na huenda kupitia kesi hiyo wananchi tutamjua muhusika halisi wa Richmond alikuwa ni nani?

Mwanahabari Huru

mnahangaika sana kumsafisha, huyo hatakati hata kwa dodoki.
 
Mkuu keshasema hawezi kufukua makaburi atashindwa kuyafukia, ispokua atashughulika na watakaohujumu taifa wakati wa utawala wake. Hivyo mliotegemea ya RICHMOND,EPA, KOGODA,ESCROW,RADA na mengineyo endeleeni kumwombea.

Sisi tuliokwishayafahamu haya wala hatushangai kwani ndivyo tulivyotegemea.Hatujui wahujumu uchumi watarajiwa watakua akina nani! Huenda ndio wale wauza nyavu na wale watafunaji pesa za maafa ndio watakaofuata.
 
Baba kasema hawezi kufukua makaburi atashindwa kuyafukia. Ispokua yeye atashughulika na wahujumu wakati wa zama zake.
Sasa mnaolia na RICHMOND, KAGODA, MEREMETA,ESCROW, RADA, EPA na mengineyo endeleeni kuliombea taifa.
 
Baba kasema hawezi kufukua makaburi atashindwa kuyafukia. Ispokua yeye atashughulika na wahujumu wakati wa zama zake.
Sasa mnaolia na RICHMOND, KAGODA, MEREMETA,ESCROW, RADA, EPA na mengineyo endeleeni kuliombea taifa.
vikaburi tu alivifukua tu kidogo mmeanza kulia njaa. Sasa akiyafungua hayo makubwa si mtakimbia nchi kabisaa😀😀😀😀
 
hiyo mahakama ya mafisi-adi sahauni tu,
Mkuu mwenyewe anaogopa mafisadi, zilikua kick za kuombea kura tu,

Mliodanganyika poleni
 
Back
Top Bottom