Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Ni dhahiri sasa mahakama ya mafisadi inaanzishwa nchini. Mahakama hii itakuwa na kazi moja tu,kusikiliza kesi za mafisadi na kuwahukumu.
Kwa muda sasa CCM povu limekuwa likiwatoka kwa madai kuwa Lowassa ni gwiji la mafisadi nchini,na kwamba CHADEMA walipotoka kwa kumpokea Lowassa. Kwamba haiwezekani mtu ambae CHADEMA walipiga kelele miaka yote kuwa ni fisadi,iweje leo wampokee na kumpa nafasi ya kugombea urais? Povu liliwatoka kwelikweli.
Na jibu la CHADEMA lilikuwa moja tu,kwanini hamkumshitaki kipindi chote hicho? Kama ni fisadi ilikuwaje hajashtakiwa? Swali lilikuwa gumu sana kwa CCM. Tena ikafika kipindi Lowassa mwenyewe akasismama kwa kiburi na kuvimba akawaambia "mwenye ushahidi aende mahakamani". Sentensi hiyo ilikuwa ni msumali wa moto kwa CCM. Hawakwenda mahakamani hadi leo.
Sasa mahakama ya mafisadi imeanzishwa.CCM hawatakuwa na sababu tena ya povu kuwatoka kumtukana Lowassa kwenye mitandao ya kijamii. Tunategemea watafanya jambo moja tu,kumpeleka Lowassa katika mahakama hiyo. Kinyume na hapo hawatakuwa na "mandate" tena ya kumtukana Lowassa kwa sababu wananchi watawauliza "kama Lowassa ni fisadi mbona hapelekwi kwenye mahakama ya mafisadi? Hawatakuwa na cha kujibu. Kwa hiyo option pekee ya CCM na serikali yake ni kumfikisha Lowassa mahakamani,kinyume na hapo Lowassa atakuwa amewafunga goli la kisigino.
Kama wakimpeleka itabidi wawe na ushahidi wa kutosha kuweza kuthibitisha ufisadi wa Lowassa. Je ushahidi huo wanao? Kwa kitendo cha Lowassa kutamka kwa kujiamini kuwa mwenye ushahidi aende mahakamani,ni dhahiri ana uhakika hawana ushahidi huo. Kama hawatakuwa na ushahidi Lowassa atawabwaga katika kesi hiyo kuwaaibisha vibaya. Na huenda kupitia kesi hiyo wananchi tutamjua muhusika halisi wa Richmond alikuwa ni nani?