Mahakama ya mafisadi itawaumbua CCM

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,898
Ni dhahiri sasa mahakama ya mafisadi inaanzishwa nchini. Mahakama hii itakuwa na kazi moja tu,kusikiliza kesi za mafisadi na kuwahukumu.

Kwa muda sasa CCM povu limekuwa likiwatoka kwa madai kuwa Lowassa ni gwiji la mafisadi nchini,na kwamba CHADEMA walipotoka kwa kumpokea Lowassa. Kwamba haiwezekani mtu ambae CHADEMA walipiga kelele miaka yote kuwa ni fisadi,iweje leo wampokee na kumpa nafasi ya kugombea urais? Povu liliwatoka kwelikweli.

Na jibu la CHADEMA lilikuwa moja tu,kwanini hamkumshitaki kipindi chote hicho? Kama ni fisadi ilikuwaje hajashtakiwa? Swali lilikuwa gumu sana kwa CCM. Tena ikafika kipindi Lowassa mwenyewe akasismama kwa kiburi na kuvimba akawaambia "mwenye ushahidi aende mahakamani". Sentensi hiyo ilikuwa ni msumali wa moto kwa CCM. Hawakwenda mahakamani hadi leo.

Sasa mahakama ya mafisadi imeanzishwa.CCM hawatakuwa na sababu tena ya povu kuwatoka kumtukana Lowassa kwenye mitandao ya kijamii. Tunategemea watafanya jambo moja tu,kumpeleka Lowassa katika mahakama hiyo. Kinyume na hapo hawatakuwa na "mandate" tena ya kumtukana Lowassa kwa sababu wananchi watawauliza "kama Lowassa ni fisadi mbona hapelekwi kwenye mahakama ya mafisadi? Hawatakuwa na cha kujibu. Kwa hiyo option pekee ya CCM na serikali yake ni kumfikisha Lowassa mahakamani,kinyume na hapo Lowassa atakuwa amewafunga goli la kisigino.

Kama wakimpeleka itabidi wawe na ushahidi wa kutosha kuweza kuthibitisha ufisadi wa Lowassa. Je ushahidi huo wanao? Kwa kitendo cha Lowassa kutamka kwa kujiamini kuwa mwenye ushahidi aende mahakamani,ni dhahiri ana uhakika hawana ushahidi huo. Kama hawatakuwa na ushahidi Lowassa atawabwaga katika kesi hiyo kuwaaibisha vibaya. Na huenda kupitia kesi hiyo wananchi tutamjua muhusika halisi wa Richmond alikuwa ni nani?

Mwanahabari Huru
 
Hii ninaifananisha na sumu iliyowekwa kuua kuku wa jirani wakati na wewe kuku wako ni wazururaji. Hapa tumejitega wenyewe na hukumu inaanzia ndani ya nyumba then nje. Hii mahakama inakwenda kusambaratisha chama fulani cha siasa hakuna ubishi kwani ndicho breeder mkuu wa mafisadi
 
Kelele za akina nape mwakyembe kwisha kazi
Tunataraji kupeleka kesi zadi ta 115 ambazo zaidi ya viongozi wa serikali maraisi wastaafu pamoja na huyu wa sasa watafikishwa mahakamani kwa tuhuma za ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka
Sasa kama watamzuia wasishtakiwe basi hakuna uhalali wac mahakama hi

Sizani kama kuna waziri
Mk mashirika ya umma
Igp
Wakurugenzj
Wizara ya ujenzi(hapa tutatumia ripot ya cag )
Afya
Aliekuwa amewaruhusu bandari kutofubga mashine za mita yaaan
Labda mniue
Ccm jiandaeni
 
Lowasa ni fisadi mkuu aliiba pesa za RICHMOND...Hata neno "fisadi " lilianzia kwa Lowasa...Lowasa hawezi epuka na kifungo...Muda si mrefu ataungana na mkwe wake Sioi Magereza Keko
 
Kelele za akina nape mwakyembe kwisha kazi
Tunataraji kupeleka kesi zadi ta 115 ambazo zaidi ya viongozi wa serikali maraisi wastaafu pamoja na huyu wa sasa watafikishwa mahakamani kwa tuhuma za ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka
Sasa kama watamzuia wasishtakiwe basi hakuna uhalali wac mahakama hi

Sizani kama kuna waziri
Mk mashirika ya umma
Igp
Wakurugenzj
Wizara ya ujenzi(hapa tutatumia ripot ya cag )
Afya
Aliekuwa amewaruhusu bandari kutofubga mashine za mita yaaan
Labda mniue
Ccm jiandaeni
Mahakama ya mafisadi itaanza na RICHMOND
 
Kesi zishaandaliwa zaidi ya 300 kuhusu haohao CCM so wajiandae
Hii ndo itakuwa mwisho wao
Sheria wanatunga wao na tutakuja kuwachapia nayo hiyo hiyo
Wakome kupeleka wabunge vilaza bungeni
Eti nae mtunga Sheria hahahahahahahaa kweli mmeishiwa
 
Kwani wewe ulifikiri mafisadi waliokuwa wanaingia mikataba mibovu walitoka UDP ama CUF? ama Magufuli alipokuwa anasema mafisadi wametafuna nchi hii alikuwa ana maana ya CUF na UDP ambao hawajawahi kuingia mikataba kwa niaba ya serikali? Mbona mnapenda kujilengesha kwa vitu vilivyo wazi. Mafisadi kwa 100% watakuwa wale waliowahi ama walio CCM maana ndo chama kimetawala mda wote. hii nayo inahitaji diploma kutuelezea?
 
Back
Top Bottom