Mahakama ya Kisutu yafuta shtaka la kutakatisha fedha dhidi ya aliyekuwa bosi wa TRA, Harry Kitilya

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,500
3,481
KESI YA KITILYA: Korti Kisutu, Dar yafuta shtaka la kutakatisha fedha dhidi ya aliyekuwa bosi wa TRA, Harry Kitilya, wengine 2. Mawakili sasa wanaomba dhamana.

================

kitilya1.jpeg
Kamishna Mkuu Mstaafu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya (kushoto) akiwa na waliokuwa Wafanyakazi wa Benki ya StanBic Tanzania, Sioi Sumari (katikati) na Shose Sinare, wakiwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Jijini Dar es salaam.

Washitakiwa hao wanaokabiriwa na mashtaka nane likiwemo la utakatishaji Fedha kiasi cha Dola za Marekani milioni 6, ili kufanikisha mkopo kutoka Benki ya Stanbic kwenda Serikalini, walifikishwa Mahakamani hapo leo kusikiliza keshi yao, na walifanikiwa kufutiwa Shitaka moja la kutakatisha Fedha kati ya nane yaliyokuwa yakiwakabili, ambapo Washitakiwa hao walisomewa kufutwa kwa shitaka hilo kwa madai ya kukosa Vidhibitisho.

Baada ya kufutiwa shitaka hilo, DPP aliwasilisha hati ya mapendekezo ya kukata rufaa ya kupinga uamuzi wa kufuta shitaka namba nane la utakatishaji Fedha linalowakabili watuhumiwa hao, ambapo zoezi la dhamana liligonga mwamba na Washitakiwa hao wamerudishwa rumande mpaka April 29 2016 ambapo mahakama itatoa maamuzi kama watuhumiwa watapewa dhamana.


Chanzo: Michuzi
 
Hata kesi watashinda. Haiwezekani kumfunga bilionea katika nchi maskini kama Tanzania .

Sheria haina siasa ni vigezo na ushahidi wa kumtia mtu hatiani tu ndio havitakamilika ama kwa nguvu ya fedha au kwa ushahidi kukosekana kisheria.

Ni mpelelezi ,hakimu, mwendesha mashtaka au shahidi gani akishawishiwa na kuahidiwa kupewa milioni mia tano atakataa. Akiangalia umaskini uliomzunguka kwenye familia yake na hatma yake kimaisha?
Jibu ni hakuna mtu kama huyo.

Kwanza hivyo viupele vyote vilivyotumbuliwa vilitokana na majipu yaliyokuwepo ngazi za juu . Wao walitekeleza maelekezo tu.
 
Hamna figisu figisu kuna vigogo watakuwa wamelindwa aiwezekani wafunguliwe watu Wa upande mmoja tu yaani egma wakati kulikuwa Na viongozi Wa serikali pia
hakuna cha kulindwa hao egma ni wezi hawakustahili kupewa dhamana
 
Back
Top Bottom