Mahakama ya Kadhi: Wabunge wafanya vurugu wakati wa Semina

Gwajima hakuwa kanisani alikuwa kwenye uwanja wa wazi wa hadhara usio wa kidini wa Tanganyika packers.Akiwa kwenye jukwa la uwanja huo kwenye huo mkutano wa hadhara aliporomosha matusi ambayo yalisikiwa na kila mtu wakiwemo waislamu maderava wa daladala n.k waliokuwa maeneo ulipo huo uwanja,vibaka,wavuta bangi waliokuwa wamekaa eneo hilohilo la viwanja vya wazi
Ok. Kanisa kwako ni majengo???
 
Dini yenu ya kinafiki sana inamaana mnahofu kwamba kuna waislamu wengi wataipinga so mnaona muwape kibano kwa shuruti kupitia sheria. Anyway kwa alichoeleza pinda nimemuelewa vizuri you have got point, lakini vp kuhusu masharti mazito yaliyomo kwenye waraka wenu vp mnaweza kuyatolea ufafanuzi?

Wala mkuu halazimishwi mtu awae muislam au dini ile kwenda kwenye mahakama hii ni makubaliano yenu tu ila utakapofika katika mahakama hukumu yake ndo tunataka itambuliwe kisheria ndo hayo tu wewe unaetoka dini ya maana yenye wezi na wasio na huruma na wananchi ambao viongozi wenu walikua mstari wa mbele kuiba hela za Escrow
 
Mambo magumu yameibuka katika suala la kujadili uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi, baada ya kutokea malumbano makali na vurugu huku idadi kubwa ya wabunge wakiitaka serikali kuuondoa Muswada wa Mahakama ya Kadhi usiwasilishwe bungeni.


Wabunge wengi walisema kufanya hivyo kunaweza kusababisha mpasuko na kuvunjika kwa amani nchini.

Aidha, wamesema suala la Mahakama ya Kadhi linataka kufanywa kama mtaji wa kisiasa kwa baadhi ya viongozi wanaotaka kuwania urais katika uchaguzi mkuu mwaka huu ili kutafuta kura za Waislamu.

Mvutano huo uliibuka jana wakati wa semina ya wabunge kujadili Muswada wa Sheria mbalimbali wa mwaka 2014 ambao ndani yake kuna Muswada wa Mahakama ya Kadhi ambao umepangwa kuwasilishwa Aprili Mosi mwaka huu siku ya kuahirisha mkutano wa 19 wa Bunge.

Mbunge wa Ngara (CCM), Deogratias Ntukamazina, alisema Kamati ya Katiba Sheria na Utawala ilipowaita viongozi mbalimbali wa dini kuzungumzia suala hilo Waislamu walitofautiana katika suala la uteuzi wa Kadhi kufanywa na Mufti Mkuu wa Tanzania na wakataka waelewane kwanza kabla ya suala hilo kupelekwa bungeni.

Alisema katika mkutano huo makundi 11 ambayo hayakubaliana na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), walisema Muswada wa Mahakama ya Kadhi uletwe bungeni baada ya kuridhiana kwa sababu hawakubaliani na Bakwata ambalo kiongozi wake ni Mufti Mkuu wa Tanzania.

Walisema maaskofu walisema hawana tatizo na suala la Mahakama ya Kadhi, lakini isiwe na muundo kama wa mahakama nyingine na kwamba mawazo ya waasisi wa Taifa, hawakutaka serikali iwe na dini na ndiyo maana hawakuruhusu mahakama hiyo.

Mbunge wa Viti Maalumu (CUF), Rukia Kassimu, alihoji ni kwanini Mahakama ya Kadhi inataka kuundwa na kupewa jukumu Mufti ambaye anatoka Bakwata ambayo ni taasisi binafsi na imesajiliwa na Mamlaka ya Rita.

"Bakwata ni taasisi kama zilivyo taasisi nyingine, haikubaliki, Mheshimiwa Waziri Mkuu aliahidi suala la Mahakama ya Kadhi ili Waislamu wampigie kura kwa sababu anataka kugombea urais mwaka huu," alisema.

Rukia alisema ni marufuku serikali kuwalazimisha Waislamu kuwa chini ya Bakwata na kwamba Waziri Mkuu, Pinda anafahamu kwa kina suluhisho na mvutano huo wa Mahakama ya Kadhi.

Mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR), Moses Machali, alisema suala la kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi na kuingizwa katika mfumo wa mahakama za kawaida inajichanganya na ibara ya 19 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alisema mwaka 2011 Rais Jakaya Kikwete wakati anazindua msikiti wa Gadaf alisema suala la uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi lisihusishwe na serikali kwa sababu wapo watu wengine ambao kila mmoja ana imani yake.

Alisema hatua ya serikali kutaka kuuleta muswada huo wakati bado Waislamu wenyewe hawaelewani ni kuwakosea Waislamu na kwamba inawezekana Waziri alilizungumzia suala hili sababu ya malengo yake ya urais.

Machali alisema kama muswada huu utapelekwa Bungeni itatoa fursa kwa madhehebu mbalimbali kila moja kuanzisha mahakama yake hali itakayoleta machafuko nchini kwa kuwa nchi itakuwa katika mfumo wa mahakama za dini.

Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, alisema muswada unapendekeza kutambua kitu ambacho mfumo wa sheria za nchi hauna na kwamba uongo unaotumiwa na serikali ndiyo unafanya watu wawe na hofu.

Mbunge wa Nkasi Kusini (CCM), Ally Kessy, alisema: "Katika nguzo tano za Kiislamu Mahakama ya Kadhi haipo, nguzo sita za imani pia haipo, sasa inakuwaje wanadai kitu ambacho hakitambuliki katika nguzo za kiislamu."

Mbunge wa Sumve (CCM), Richard Ndassa, alisema muswada wa Mahakama ya Kadhi urudishwe ukaboreshwe badala ya kuharakisha kuupeleka bungeni wakati bado una utata hata kwa waislamu wenyewe.

Mbunge wa Tarime (CCM), Nyambali Nyangwine, alisema Muswada wa Mahakama ya Kadhi usimamishwe ukafanyiwe utafiti kwanza kwa sababu ndani ya Waislamu wenyewe hawaelewani.

Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini, alisema Wabunge wasipokuwa makini na suala la Mahakama ya Kadhi, Bunge litaingia katika historia kuvunjika kwa amani.

Selasini alisema serikali iachane na kutoa ‘jini' lililofungiwa na waasisi Mwalimu Nyerere na Karume na kwamba tukifanya mchezo nchi itabaki katika vipande vipande.

Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Dk. Mary Mwanjelwa, alisema jambo hili litaligawa Taifa na kwamba waasisi hawakuwa wajinga walipokataa serikali isiwe na dini.

Mbunge wa Gando (CUF), Khalifa Suleiman Khalifa, alisema nchi inaelekea kubaya kwani msingi wa kuleta Mahakama ya Kadhi ni kutaka kuwachota Waislamu kwa ajili ya uchaguzi mkuu.

"Serikali kama imedhamiria kuleta Mahakama ya Kadhi ilete katika utaratibu mzuri, lakini kwa huu utaratibu ni unafiki na mwenyezi Mungu hapendi unafiki, tusiwahadae Waislamu," alisema.

Khalifa alisema kwa hali ilivyo muswada huo haujaiva na kwamba usiletwe bungeni hadi hapo serikali itakapojipanga vizuri.

Mbunge wa Mbozi Magharibi (Chadema), David Silinde, alisema suala la imani siyo la chama cha kisiasa kwani suala la Mahakama ya Kadhi litaipeleka nchi kubaya na inawezekana ikawa ndio mwisho wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

"Mnataka kutuvurugia nchi sababu ya kutafuta kura za Waislamu, kwa hili Waziri Mkuu umechemka sana, nalisema hili kwa sababu wewe Waziri Mkuu ndiye uliyeahidi kuleta bungeni Muswada wa Mahakama ya Kadhi," alisema.


Mbunge wa Kisarawe (CCM), Suleiman Jafo, alisema yasifanyike masikhala mswaada huyo uwasilishwe bungeni.

Mbunge wa Mbeya Vijijini (CCM), Mchungaji Lackison Mwanjale, alisema serikali ikajipange upya katika suala la Mahakama ya Kadhi kabla ya kuuleta bungeni muswada kwani bado suala hilo halieleweki kwa jamii.

Mbunge wa Kilwa Kaskazini (CCM), Martaza Mangungu, alisema hakubaliani na suala la Mufti kupewa jukumu la kuchagua Kadhi Mkuu wakati Waislamu wengi hawakubaliani na Bakwata ambayo inaongozwa na Mufti.

Mbunge wa Lupa (CCM), Victor Mwambalaswa, alisema muswada wa Mahakama ya Kadhi wapelekewe wahusika kabla ya kuletwa bungeni ili wajadiliane na kukubaliana mambo ya msingi wanayoona yatawafaa katika uanzishwaji wa mahakama hayo.

Mbunge wa Igunga (CCM), Dk. Peter Kafumu, alisema serikali imeshindwa kusimamia vizuri suala la uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi kwa kushindwa kuwaelimisha wananchi jambo hilo.

Mbunge wa Chwaka (CCM), Yahaya Kassim Issa, alisema Waislamu wanataka Mahakama hiyo kwa kuwa wanakosa haki hivyo serikali iruhusu kuanzishwa kwake.

PINDA: TUTAFAKARI UPYA
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akihitimisha mjadala huo alisema kulingana na maoni yaliyotolewa na Wabunge ameelewa kwamba bado hakuna maelewano miongoni mwa Waislamu wenyewe na pia hakuna uelewa wa jamii kuhusu suala hilo.

Alisema mambo yaliyowasilishwa kuhusiana na muswada huo ni maamuzi ya Bunge Maalum la Katiba na siyo yake, bali anabebeshwa msalaba tu kwa sababu alikuwa anaiwakilisha serikali.


Pinda alisema kutokana na hali hiyo, serikali itakaa kushauriana tena na Spika pamoja na Rais waone wafanye nini katika jambo hilo.

VIJEMBE NA MATUSI
Mbunge wa Tabora Mjini (CCM), Ismail Aden Rage, wakati akichangia hoja hiyo alishindwa kuvumulia baada ya baadhi ya wabunge kuingilia mchango wake kwa kumzomea na kusema maneno yaliyomuudhi na kuamua kuwatolewa maneno ya kuudhi (matusi).

Mbunge wa Fuoni (CCM), Said Mussa Zubeir, aliwaita baadhi ya wabunge walikuwa wakimzomea wakati akizungumza kuwa ni ‘wapumbavu'.

Wakati wa majadiliano hayo ilipofika saa 8:17 wakati Mbunge wa Kisarawe, Jafo akiendelea kuchangia kulitokea vurugu ambazo nusura wabunge wapigane huku baadhi yao wakiamua kutoka ukumbini.

Kutokana na kutokuwapo hali ya utulivu ukumbini, baadhi ya askari pamoja na maofisa usalama waliokuwapo nje, walilazimika kuingia ndani kuhakikisha amani haivunjiki.

Spika wa Bunge, Anna Makinda, alituliza vurugu ukumbini kwa kuwataka wabunge wawe wavumilivu wakati wenzao wakichangia.

Katika majadiliano wabunge zaidi 30 walichangia na zaidi ya 20 walikataa muswada wa Mahakama ya Kadhi usiwasilishwe Bungeni siku ya Jumatano wiki hii.

Kabla ya kuanza majadiliano, Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia, alitoa hoja kwa Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge, Katiba, Sheria na Utawala, William Ngeleja, kwamba wakati wa majadiliano waandishi wa habari wasiwepo ukumbini kwa kile alichoeleza ni unyeti wa jambo hilo.

Hata hivyo, Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Kessy, alisema kama waandishi wataondolewa ukumbini naye atalazimika kuondoka huku Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, akisema hakuna sababu ya kuwaondoa waandishi kwa sababu jambo linalojadiliwa wananchi wanataka kulifahamu kupitia vyombo vya habari. Masaju akichangia wakati wa kujibu hoja za wabunge, alisema suala la mahakama ya kadhi halina tatizo wala halivunji katiba kama ilivyoelezwa na baadhi ya wabunge na kuwataka wabunge wamuheshimu wakati ana-zungumza.
CHANZO: NIPASHE

CC: Invisible Moderator
 
Last edited by a moderator:
Mh. Pinda ni pro hii mahakama kama kete ya kujitwalia urais na ndio maana ana fanya push kubwa sana kuhakikisha huu muswada unapita. Naamini asilimia kubwa ya waTZ hawahutaki huu mswada wa dini ya kiislam. Ni aibu iliyoje kwa serikali kuleta mambo yahusuyo dini fulani ndani ya jengo la bunge bila ku project consequences. Hali ikiendelea hivi tutajikuta tukitambuana kwa dini zetu katika maeneo yetu. Itafika mahali kila dini ikawa na usafiri wake, hoteli zake nk kutokana na kukosa busara kwa viongozi wetu
 
Kama issue ni maamuzi ya kadhi kutambuliwa na serikali kisheria, mtu akionewa na kadhi atakata rufaa kwenda wapi? Na Je, kama muislam naye ni mtz kwa nini asihukimiwe AMA kusaidiwa kwa mjibu wa sheria za nchi kuliko dini?
 
In conclution..hii nji igawanywe...waislam kwao na wakiristo kwao..full stop.
 
Bunge lina wawakilishi ambao tunaamini wengi ni waelewa na wavumilivu katika mijadala yenye mambo wasiyokubaliana nayo. Ikiwa wabunge wameshindwa kuvumiliana kwenye mjadala huu wenye hisia za kidini jaribu kufikiria mjadala huu utakapofika kwa wananchi wa kawaida ambao wanaamini kuwa wanabisha kwa niaba ya miungu wao! Naweza kuona vurugu za aina yake ikiwa huu mpango utaendelea.
 
Vurugu,kejeli na lugha za matusi miongoni mwa wabunge vimeibuka katika semina ya wabunge kuhusu muswaada wa mahakama ya kadhi.

Semina hiyo iliyohudhuriwa na waziri mkuu, imefanyika leo mkoani Dodoma ambayo iliongozwa na spika Makinda kama mwenyekiti ambae ameonekana kuwa na kazi ya ziada kutuliza hasira na jaziba za wabunge mfano mh.Machali.

Mh.Machali alionekana kuwa na hasira huku mwanasheria mkuu wa serikali akitoa vitisho kwa wabunge kuwa anaweza kutumia mamlaka yake mengine aliyonayo katika vurugu hizo huku Mbatia akimtaka mwanasheria huyo kuacha vitisho.

Vuruga hizo zilionekana kuwagawa wabunge hao kutokana na dini zao ambapo mbunge mmoja alisikika akiwataka wabunge wenzake wakisiilamu wakutane kwa majadiliano.

Waziri mkuu aliahidi kufanya mashauriona na raisi na wadau wengine kuhusu muswaada huo.

Chanzo:ITV

Hapa ndipo ninapopata kigugumizi dhidi ya wabunge wa Tz.

Kama wameweza kuzuia muswada hii wa Mahakama ya Qadhwi JE WALISHINDWAJE KUZUIA MUSWADA WA TAKWIMU NA HATA ULE WA HABARI?

Au ndio ile ile roho ya kikirosho kubainiana wenyewe kwa wenyewe.?
 
Hili suala la mahakama ya kadhi mnataka kulazimisha kulipeleka mahala pasipo pake. Ni suala la kidini tena zaidi mojawapo ya IBADA. Hatuwatendei haki Waislamu nao pia hawajitendei haki kupeleka suala la IBADA ya Kiislamu kujadiliwa na wasio waumini wa dini hii. Kujadili haki za makundi ya walemavu, wanawake, etc ni suala la KIJAMII ambalo mtu awe muumini ya dini yo yote ile, hata pagani, linamhusu.Mtu wa imani yo yote anaweza kuwa mwanamke, mwanamumu, mlemavu, nk.

hawa jamaa wakifanikiwa adhma yao ya kuliingiza hili jambo la IBADA yao kwenye katiba ujue nchi imesilimishwa, hivi wakija kudai tena suala la KWENDA KUSWALI MSIKITINI au KUHIJI MAKA kuwa ni IBADA yao nayo yaingizwe kwenye katiba mtawakatalia?
 
Teh teh teh

Maoni yake kwan alikuambia kwamba alikua anaongelea kanisani pale??

Alikuwa kwenye kikao rasmi cha kamati ya bunge.

Imekuuuma eeeh??

Teh teh teh
sasa hata ikiniuma kwani inasaidia nini wakati najua mahakama ya kadhi katu haitakuja kuwepo tz? usijipe moyo mzee. inakuwaje mahakama za al shabab, ISIS na boko haram ziingizwe kwenye katiba? ni mungu gani huyo chinjachinja mnayemwabudu na kutaka kutuwekea kwenye katiba yetu?ningekuwa mimni ningenyamaza. sharia yenyewe inawaita watu wengine makafiri, unataka maneno kafir yaingie kwenye katiba ya watu wote.hivyo katiba ya watz wote itakuwa inabagua wengine inawaita makafir na wengine sio makafiri, katiba ya wapi hiyo? si ya boko haram kabisa hiyo?
 
In conclution..hii nji igawanywe...waislam kwao na wakiristo kwao..full stop.

Kwa hali iliyofikia upande wa Tanganyika jambo hilo lipo karibuni sana. Kwani sasa kinacholinda ni Muungano tu na Znz.

kama muungano ukivunjika basi TGK laazima uongozi utagawanjwa kwa vigezo vya DINI mathalan kama raisi wa TGk akiwa mkristo basi waziri mkuu awe mwislam n.k.

Tuwe na subra tutaona mengi sana.

 
Kwa hali iliyofikia upande wa Tanganyika jambo hilo lipo karibuni sana. Kwani sasa kinacholinda ni Muungano tu na Znz.

kama muungano ukivunjika basi TGK laazima uongozi utagawanjwa kwa vigezo vya DINI mathalan kama raisi wa TGk akiwa mkristo basi waziri mkuu awe mwislam n.k.

Tuwe na subra tutaona mengi sana.


Kaka kilichobaki coz tushachoka sasa...hii nchi kila kitu lazima iangaliwe din..tumeshindwa kuvumiliana kama vp tugawane mbao tu...
 
Wala mkuu halazimishwi mtu awae muislam au dini ile kwenda kwenye mahakama hii ni makubaliano yenu tu ila utakapofika katika mahakama hukumu yake ndo tunataka itambuliwe kisheria ndo hayo tu wewe unaetoka dini ya maana yenye wezi na wasio na huruma na wananchi ambao viongozi wenu walikua mstari wa mbele kuiba hela za Escrow

Ndomana tunataka katiba yenye meno makali kuwawajabisha hao mafisadi haijalishi ni wakristo wenzangu. Ila nimekuuliza kuhusu waraka walioandika viongozi wenu wakisisitiza kadhi igharamiwe na serikali vp unalolote la kusema hapo?
 
assadsyria3 - Unakosa maana, hekima na utu wa kumstahi mwenzio. Lugha uliotumia haikubaliki kamwe. Imetokea wapi. Sielewi ufahamu wako uko kwa kiwango gani hata 'reasoning capacity" yako, hivyo punguza jazba zisizo na msingi.
We unavyowaita wenzako mashetani hiyo siyo kashfa na matusi.msipende kujifanya mna busara na hekma wakati tunaona post zako unavyotukana na kukashifu dini za wengine.huu ni unafiki
samahani mkuu Si wewe hii post nilimaanisha kwa mpuuzi mmoja hapa jukwaani username zinafanana.
 
Bunge lina wawakilishi ambao tunaamini wengi ni waelewa na wavumilivu katika mijadala yenye mambo wasiyokubaliana nayo. Ikiwa wabunge wameshindwa kuvumiliana kwenye mjadala huu wenye hisia za kidini jaribu kufikiria mjadala huu utakapofika kwa wananchi wa kawaida ambao wanaamini kuwa wanabisha kwa niaba ya miungu wao! Naweza kuona vurugu za aina yake ikiwa huu mpango utaendelea.

Hili bunge lililojaza wahuni unategemea liwe na busara hiyo unayoisema? Wengi wa wabunge wetu hawajachaguliwa kutokana na busara zao bali ni hela zao na namna wapiga kura wanavyowachukulia na sio kwamba ni watu wenye hekima hivyo ndugu yangu.
 
Back
Top Bottom